John Heche azuiliwa mpaka wa Sirari akiwa anaelekea Kenya kwenye mazishi ya Odinga

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Wegese Heche amezuiliwa kusafiri Kwenda nchini Kenya kuhudhuria Mazishi ya Raila Amolo Odinga, Mh Heche amezuiliwa Mpaka wa Tanzania na kenya (Sirari) Wilaya ya Tarime

Mpaka sasa uhamiaji wamechukua hati ya kusafiria ya Mh Heche na hawajatoa sababu zozote za kwanini wanamzuia kwenda nchini Kenya, Jana Serikali ya Tanzania ilikuwa na mwakilishi kwenye ibada maalum ya kuuga Mwili ya Mh Odinga na Wakilishi wa Tanzania waliongozwa na Makamu wa Rais Mh Philipo Mpango, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na wengineo.

Tunaendelea kufuatilia na taarifa rasmi itatolewa na Chama Makao Makuu

J. Mnyawami
Katibu kanda ya Serengeti
18/10/2025

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.


UPDATE: KUTOKA CHADEMA MAKAO MAKUU


TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuutangazia umma kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imemuweka kizuizini Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa John Wegesa Heche.

Mhe. Heche amekamatwa Saa Nane, mchana huu wa Jumamosi, Oktoba 18, 2025 mkoani Mara kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya huko Isibania One Stop Border alipokuwa anataka kuingia Kenya.

Ikumbukwe kuwa jana, tulitoa taarifa tukiutaarifu umma kuwa Mhe. Heche atakwenda nchini Kenya kukiwakilisha Chama hudhuria mazishi ya Mwanasiasa nguli wa Kenya, Raila Amolo Odinga.

Pamoja na kumuweka kizuizini, Mamlaka ya Uhamiaji Tanzania imemnyang'anya hati yake ya kusafiria (Passport) bila kueleza kwanini wamechukua uamuzi huo. Kumzuia Mhe. Heche kwenda kuwapa pole Wakenya ni kuwanyima raia wa nchi hiyo haki yao ya kufarijiwa wanapofikwa na majanga mbalimbali ikiwemo misiba.

Tunaitaka Serikali ya Tanzania imuachie mara moja Mhe. Heche na iache kuwanyanyasa viongozi wa Chama chetu, kuwapora haki yao ya kutoka nje ya nchi na kuingia kama inavyoelezwa kwenye Ibara ya 17(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa leo Jumamosi, tarehe 18 Oktoba 2025

Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi



​
 
Hivi kwa haya yanayoendelea,je CHADEMA kwa nini wasisalimu amri kwa muda ili wajipange upya?? Maana sioni mwisho mwema kwa kuvimbiana na serikali namna hii

Robert Heriel Mtibeli unasemaje juu ya hili?
 
Write your reply...safi sana anataka kutoroka kwa kutumia kisingizio cha msiba
 
China AID
 
Ni sawa ifatiliwe kama kweli ni halali na kama kweli mtu huyo ni raia wa Tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…