John Heche: Chokochoko siyo neno la kistaarabu

John Heche: Chokochoko siyo neno la kistaarabu

  • Amewahi kuwa makamu wa rais,
  • Amewahi kuwa Waziri Mkuu,
  • Amewahi kuwa mwenyekiti wa time ya mabadiliko ya KATIBA .

Kwahiyo huyu akiongea wewe msafisha viatu wa kwa Mtogole ama huko Ibinzamata unapaswa kunyamaza
Sawa.....

Kuwa kwake na vyeo vyote hivyo si ngao ya kutomkosoa pale atelezapo....

Nami wa Mtogole nina haki ya kutoa mawazo yangu kuwa KATIBA TULIYONAYO haina ombwe lolote la kisiasa...

Wanasiasa wanalazimisha tuamini tu katika iitwayo TUME HURU YA UCHAGUZI.....

Ikumbukwe demokrasia inaweza kutafsiriwa na ada ya nchi husika....

Ada yetu watanzania ni historia yetu...rejea haiwezi kutoka KENYA...

Katiba ya Jaji Warioba ilipendekeza SERIKALI 3 ambazo kimantiki ni kwenda kujitia kitanzi cha kuuvunja MUUNGANO pale ambapo kutakuwa na inuko la watu aina ya wale G55......

#KaziIendelee
#KatibaYetuNiBora
 
Kama kuomba katiba mpya ni chokochoko, basi JK, Waryoba, Butiku, Augustin Ramadhani, Samia Suluhu (wa wakati ule) na wengine, walifanya uhaini kwa kujadili kabisa rasimu ya katiba mpya!
 
Kama kuoomba katiba mpya ni chokochoko, basi JK, Waryoba, Butiku, Augustin Ramadhani, Samia Suluhu (wa wakati ule) na wengine, walifanya uhaini kwa kujadili kabisa rasimu ya katiba mpya!
CHOKOCHOKO si Uhuru wa kuongea.....

CHOKOCHOKO ni MAANDAMANO YA VURUGU ambayo CHADEMA wamenuia KUYAITISHA NCHI NZIMA....
 
Kwani SSH alisema hataki katiba mpya?
Ndiyo. Hukumsikia siku ile anasema mpk ajenge uchumi kwanza??

Ni suala la kutumia akili tu mkuu.
Hivi ukipewa ahadi kama hiyo si sawa na kunyimwa tu? Maana hata Marekani bado wanajenga uchumi wao.
 
Ndiyo. Hukumsikia siku ile anasema mpk ajenge uchumi kwanza??

Ni suala la kutumia akili tu mkuu.
Hivi ukipewa ahadi kama hiyo si sawa na kunyimwa tu? Maana hata Marekani bado wanajenga uchumi wao.
Katiba mpya si takwa la watanzania walio wengi.....

Ni takwa la wanasiasa wenye uchu wa madaraka wanaotaka muungano UVUNJIKE......
 
Sawa.....

Kuwa kwake na vyeo vyote hivyo si ngao ya kutomkosoa pale atelezapo....

Nami wa Mtogole nina haki ya kutoa mawazo yangu kuwa KATIBA TULIYONAYO haina ombwe lolote la kisiasa...

Wanasiasa wanalazimisha tuamini tu katika iitwayo TUME HURU YA UCHAGUZI.....

Ikumbukwe demokrasia inaweza kutafsiriwa na ada ya nchi husika....

Ada yetu watanzania ni historia yetu...rejea haiwezi kutoka KENYA...

Katiba ya Jaji Warioba ilipendekeza SERIKALI 3 ambazo kimantiki ni kwenda kujitia kitanzi cha kuuvunja MUUNGANO pale ambapo kutakuwa na inuko la watu aina ya wale G55......

#KaziIendelee
#KatibaYetuNiBora
Hayo ya tume huru umeyasema wewe. Mzee Warioba kwa nafasi yake na umri wake wala hana haja ya kugombea cheo chochote kinachosimamiwa na tume.

Hayo ya kufanya rejea ya Kenya ndiyo nayasikia kwako. Mzee Warioba Wala hajayasema.

Na ni kweli kwamba hata wewe wa kwa Mtogole una haki ya kutoa maoni. Lkn huna locus (ama authority) ya kupinga mawazo ya gwiji la siasa kama Warioba.
 
Kama kuomba katiba mpya ni chokochoko, basi JK, Waryoba, Butiku, Augustin Ramadhani, Samia Suluhu (wa wakati ule) na wengine, walifanya uhaini kwa kujadili kabisa rasimu ya katiba mpya!
Bhaeleze! Bhaaambie bhaelewe. Maana Hawa uvccm wa miaka hii ni bendera fuata upepo. Hawana wanacho kisimamia.
 
Hayo ya tume huru umeyasema wewe. Mzee Warioba kwa nafasi yake na umri wake wala hana haja ya kugombea cheo chochote kinachosimamiwa na tume.

Hayo ya kufanya rejea ya Kenya ndiyo nayasikia kwako. Mzee Warioba Wala hajayasema.

Na ni kweli kwamba hata wewe wa kwa Mtogole una haki ya kutoa maoni. Lkn huna locus (ama authority) ya kupinga mawazo ya gwiji la siasa kama Warioba.
Umesema WARIOBA ni gwiji la siasa...uko sahihi ....

Ila katiba si "msahafu tu" wa matakwa ya kisiasa.....

Ndani yake kuna TURATHI ZA TUNU NA TAMADUNI za watanzania....

Wanasiasa pekee si wahodhi wa KATIBA YA NCHI.....

Mathalani wako wanasiasa wanaotaka SERIKALI 3....je ni takwa la watanzania wote?!!!

G55 na "aila" yao wanazilenga NAFASI ZA KIUONGOZI NA KIUTAWALA pale itakapopatikana TANGANYIKA......

Ikipatikana TANGANYIKA ,watu aina ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan kamwe hawatokuwa tena VIONGOZI WAKUBWA WA TANGANYIKA.....

Japo kutoka kwangu kwa MTOGOLE kumenifanya unione "fulafula" mbele ya "macho yako" ila ninatanguliza shukrani kwa kutonipoka haki yangu ya kutoa maoni na kusikilizwa....
 
Hauoni kuwa kwa kusema hivi una maanisha kuwa aliingia kifungoni kwa "hisani"?
Fundi,

Hisani ni wema. Ni moyo wa kumtendea mtu mazuri.

Mtu anaweza kweli kuingia kifungoni kwa ‘hisani’?

Nadhani hapo neno linalofaa ni ‘hila’ au ‘ghiliba’.
 
Kwi Kwi Kwi , nimepiga kwenye mshono kudadeki !
Sasa mshono upi ?!!

Yaani RBC bado unang'ang'ana kuwa KIFO ni adhabu kwa binadamu ?!!!!

Magufuli ameishi na ametenda yake.....

Sisi tutamkumbuka kwa mengi mazuri ...mengi mnooo......
Nyinyi mkumbukeni kwa MABAYA....

Magufuli bado yu hai....yu hai kwa MATENDO YAKE MEMA KWA TAIFA HILI....

Magufuli yuko nasi....

Yuko nasi pale UBUNGO FLYOVER....
Yuko nasi pale MFUGALE FLYOVER.....
Yuko nasi kule darajani KAGONGO NA BUSISI....
Yuko nasi JIJINI DODOMA....
Yuko nasi sana kule MTUMBA...si muda mrefu balozi za nchi za kigeni zitajenga pale MAGUFULI CITY......
Magufuli yu nasi kule MWALIMU NYERERE HEPP....
Magufuli yu nasi katika SGR....

HAYO NI MACHACHE....

MAGUFULI ANAISHI NASI!!!

#KaziIendelee
 
Japo kutoka kwangu kwa MTOGOLE kumenifanya unione "fulafula" mbele ya "macho yako" ila ninatanguliza shukrani kwa kutonipoka haki yangu ya kutoa maoni na kusikilizwa....
Basi nami ngoja "nikwinye" mbawa zangu nirudi zangu "mtema". Kama utahitaji somo zaidi nitamtafuta "mgandi" twende mandhari "akupute" kutu.
 
Back
Top Bottom