Najuwa chama kina mambo mengi yanayokikabili; lakini maswala ya namna hii, ya viongozi na wanachama kupotea (mikononi mwa polisi) yanahitaji ufuatiliaji wa karibu zaidi ya kuyatamka tu kwenye mikutano au kwenye hadhara na familia athirika.
Ni muhimu uwepo ufuatiliaji wa karibu na wahusika, ili pawepo na kumbukumbu sahihi.
Viongozi wa chama ndani ya kanda hiyo au mkoa ni wajibu wao kufanya ufuatiliaji wa karibu zaidi.
Nyakati hizi maswala haya si ya kuyaacha tu yakielea, bila majibu.