Inaonekana wewe siyo mfuatiliaji wa mambo haya. Ni aheri ungekaa kimya.
Siku zote watu walikuwa wanasema kuwa marehemu alikuwa anapeleka miradi mikubwa Chato isiyo na tija kwa wananchi walio wengi, wakati Chato ina huduma duni za afya na maji. Tena walikuwa wanasema kabisa kuwa badala ya kuwawekea taa za barabarani, angewapelekea maji.
Hakuna mtu ambaye angeweza kuhoji kama wananchi wa Chato wangekuwa wanapelekewa huduma muhimu, ambazo kwa sasa hawana. Uwanja wa ndege unawasaidia nini wananchi walio wengi ambao hawana hata huduma ya maji?