Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche, ametoa wito mzito kwa vijana na wanaharakati nchini kuanzisha kampeni kabambe ya kudai uhuru wa Tundu Lissu.
Akizungumza leo Aprili 9, 2026, kupitia baraza la kidijitali, John Heche amesisitiza kuwa muda wa kulalamika chini kwa chini umekwisha na sasa ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti za kitaifa.
Kiongozi huyo amewataka vijana wanaodai kuunga mkono harakati hizo kuacha kusemea pembeni, badala yake waanzishe kampeni kubwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani.
Ameelekeza kuandikwa na kubandikwa kwa vipeperushi kila kona ya mtaa ili kuonyesha mshikamano kwa Lissu ambaye amekaa ndani kwa mwaka mzima kwa tuhuma za uhaini. Jambo hili John Heche ameliita kuwa ni kumvua haki kiongozi huyo aliyekuwa akiwapigania wananchi bila kuwa na hatia yoyote.
John Heche amebainisha kuwa kampeni hiyo inalenga kumpa Lissu nguvu na imani kuwa watu anaowapigania ni sahihi na wako naye. Hata hivyo, ametoa onyo kali kuwa iwapo sauti yao haitasikilizwa kupitia kampeni hiyo, basi CHADEMA wataanzisha maandamano makubwa nchi nzima. Amesisitiza kuwa hawawezi kuendelea kukaa kimya wakati kiongozi wao akiteseka gerezani kwa mwaka mzima, akiamini kuwa ni lazima nchi itikisike ili haki itendeke.