John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

Kwa mtazamo wangu Chadema ya Mbowe ilikuwa na ari zaidi ya hii ya sasa. Hata wakati Mbowe amewekwa ndani waliendelea kupambana. Inawezekana kuwa ile ilikuwa zaidi ya ground wakati hii ya sasa ni ya matandao, wasomi n.k.
Nilipoandika hayo maneno uliyo 'quote', nilikuwa na maana hiyo hiyo ya "ari" unayoizungumzia wewe hapa; hata bila ya kutaka kumtaja Mbowe moja kwa moja. Usisahau mchango wa makatibu wakuu waliosimamia hali hiyo kuwepo.

Uko sahihi kabisa, hali ya namna hiyo ya vijana wa wakati huo ndiyo hasa inayotakiwa kuwepo wakati huu. Naamini kabisa kuwa vijana hao wapo huko 'ground' na hata katika wasomi makundi ambayo wewe umeyabainisha.
Ni swala la kuwaongoza tu na kuweka mipango sahihi ya utekelezaji wa majukumu yao.

Hii ndiyo kazi inayotakiwa kufanywa na viongozi wa chama waliopo.

BTW: Nimeoma mawazo yako mengine huko juu. Nimeyanyamazia kwa matumaini.
 
Watanzania na hasa watanganyika tuacheni uoga wa kutengenezewa. Tunaburuzwa sana pasi na sababu kwa kakikundi cha walafi wa mali na madaraka. Tuamkeni wote kwa umoja wetu kuupinga kwa nguvu zetu zote bila kujali itikadi na dini zetu tuukatae huu ukoloni wa mtu mweusi.
Kupitia Lissu tutajikomboa hakika. Amkeni.
Oktoba 29 lakni?
Au ndo walewale keyboard worriers!
 
Nilipoandika hayo maneno uliyo 'quote', nilikuwa na maana hiyo hiyo ya "ari" unayoizungumzia wewe hapa; hata bila ya kutaka kumtaja Mbowe moja kwa moja. Usisahau mchango wa makatibu wakuu waliosimamia hali hiyo kuwepo.
Mbona Mnyika bado yupo? Nini kimempata?
Uko sahihi kabisa, hali ya namna hiyo ya vijana wa wakati huo ndiyo hasa inayotakiwa kuwepo wakati huu. Naamini kabisa kuwa vijana hao wapo huko 'ground' na hata katika wasomi makundi ambayo wewe umeyabainisha.
Vijana kama Heche, Ruge, yule dada wa Njombe, Husna, Aisha walikomazwa na Mbowe. Mbowe aliwawezesha kwa sababu hakuongoza tu bali nae alipigwa na kulala nao lupango. Ilichukua muda kufikia walipofikia. Hawa waliokuwepo sasa hawana huo uvumilivu.
Ni swala la kuwaongoza tu na kuweka mipango sahihi ya utekelezaji wa majukumu yao.
Inabidi kwanza wengi wao wajifunze adabu na wawe wanyenyekevu kwa walio watangulia. Nilishangaa walivyokuwa wanatoa maneno ya shombo dhidi ya Mbowe wakati wa msiba wa mkwe wake. Na viongozi wao wanawaangalia tu.

Hii ndiyo kazi inayotakiwa kufanywa na viongozi wa chama waliopo.
Unfortunately, sidhani kama wana huo uwezo.
BTW: Nimeoma mawazo yako mengine huko juu. Nimeyanyamazia kwa matumaini.
Ungeongea tu.

Amandla...
 
Mbona Mnyika bado yupo? Nini kimempata?

Vijana kama Heche, Ruge, yule dada wa Njombe, Husna, Aisha walikomazwa na Mbowe. Mbowe aliwawezesha kwa sababu hakuongoza tu bali nae alipigwa na kulala nao lupango. Ilichukua muda kufikia walipofikia. Hawa waliokuwepo sasa hawana huo uvumilivu.

Inabidi kwanza wengi wao wajifunze adabu na wawe wanyenyekevu kwa walio watangulia. Nilishangaa walivyokuwa wanatoa maneno ya shombo dhidi ya Mbowe wakati wa msiba wa mkwe wake. Na viongozi wao wanawaangalia tu.

Unfortunately, sidhani kama wana huo uwezo.

Ungeongea tu.

Amandla...
Unaongea nini mzee wakati ule wa Mbowe yupo ndani na wakati huu ni tofauti sana

Wakati huu vijana wengi sana watekekwa na kupotezwa kwa wingi sana, mauaji yaliyofanyika oktoba 29 yanatisha,

Alafu wakati ule wa Mbowe Chama akikufungiwa kama sasa na kuzuiwa kutumia mali za Chama

Mbowe alitoka kwa kuwalamba miguu viongozi wa CCM.

Mbowe ndo muasisi wa haya yanayompata Lissu kama mbowe Angekaza CCM wasingetumia njia hii tena ila kwakua ilitumika kwa Lissu ikatiki wameona wairudie kwa Lissu ambae hataki kusikia kuachiwa kwa mashariti

Waendelee na Kesi mahakamani waache janjajanja kesi imewapalia
 
Huyo nae ni bwabwa la Sultan Mbowe wana hasira sana na Lissu
 
Unaongea nini mzee wakati ule wa Mbowe yupo ndani na wakati huu ni tofauti sana
Tofauti zipi hizo? Kumbuka ni mwaka mmoja tu toka Mbowe ashindwe uchaguzi.
Wakati huu vijana wengi sana watekekwa na kupotezwa kwa wingi sana, mauaji yaliyofanyika oktoba 29 yanatisha,
Wakina Soka walipotea wakati gani? Mzee Kibao aliuawa wakati gani? Wakati Mbowe yuko ndani mamia ya wanachama wa Chadema walikuwa wamefunguliwa kesi mbaya ikiwa pamoja na za mauaji. Nakubali kuwa mauaji ya Oktoba 29 yanatisha. Lakini kumbuka jinsi mlivyomsusia Mbowe alipoita maandamano dhidi ya utekaji na kupotea kwa watu kusikoeleweka. Hata viongozi wenu wa sasa waliingia mitini wakamuacha Mbowe aandamane pamoja na binti yake. Hao wanaotamba sasa hivi walijificha kwa uoga. Ni wakina mama wa Bawacha peke yao ndio walidiriki kuja Dar kuunga mkono juhudi zake.
Alafu wakati ule wa Mbowe Chama akikufungiwa kama sasa na kuzuiwa kutumia mali za Chama
Chama kilizuiwa kufanya mikutano ya hadhara. Hata walipofanya vikao vya ndani walishughulikiwa. Mbowe alikamatwa Mwanza akiwa ameenda kuhudhuria mkutano wa ndani. Pamoja na mazuio yote hayo waliendelea kupambana. Wanawake wa Chadema walikaa sana ndani. Mbowe na wenzie walikaa jela mpaka umma ulipowalipia faini. Mbowe alikataa kutoka jela mpaka wenzake wote walipotoka.
Hawa wa sasa wanakaa kimya ati kwa sababu wamezuiwa kutumia rasilimali za chama wakati rasilimali kubwa ni wanachama ambao hawawezi kuzuiwa wakiamua kufanya siasa.
Mbowe alitoka kwa kuwalamba miguu viongozi wa CCM.
Hapo ndipo mnapo kosea. Mbowe hakumlamba kiongozi yeyote wa CCM. Ingekuwa hivyo pasingekuwa na sababu ya yeye kuweka masharti kama wakina Lissu waachiwe warudi kwa amani, kesi dhidi ya wafuasi wake zifutwe, mikutano ya hadhara iruhusiwe n.k.
Mbowe ndo muasisi wa haya yanayompata Lissu kama mbowe Angekaza CCM wasingetumia njia hii tena ila kwakua ilitumika kwa Lissu ikatiki wameona wairudie kwa Lissu ambae hataki kusikia kuachiwa kwa mashariti
Ulitaka Mbowe akaze vipi? Ang'ang'anie kubaki rumande wakati serikali imesema haina nia ya kuendelea na kesi dhidi yake? Au ulitaka akaze ili wakina Lissu washindwe kurudi? Serikali haitaki tu kumuachia Lissu na sio kwa sababu amekataa masharti kama mashabiki mnavyo dai. Wapinzani wa Chadema wanajua kuwa hamna kiongozi zaidi ya Lissu. Wakimshikilia Lissu chama wanakifanya chama kikose muelekeo. Wakati wa Mbowe wigo ulikuwa mkubwa na walijua hata wangeendelea kumshikilia chama kingeendelea kuwatesa. Hii ndio sababu ya kutotaka Mbowe ashinde maana walijua hataingia katika mtego aliotegewa Lissu.
Waendelee na Kesi mahakamani waache janjajanja kesi imewapalia
Wasipoendelea na kesi mtawafanya nini? Hapa mnaonyeshwa kuwa nyinyi si lolote si chochote. Mlitakiwa kujipanga upya na kuja na strategy nyingine. Wenye huo uwezo wa kuwapa ushauri wapo lakini mmekaza shingo. You have been played.

Amandla...
 
Ungeongea tu.
Nimeongea kikamilifu kabisa katika mstari huo. Naona hilo limekupita pembeni.

Hayo mengine uliyoweka huko juu ya lawama; utakapoachana na 'mentality' ya namna hiyo utakuwa na mawazo yasiyofungwa na mapenzi kwa mtu ambaye amejidhalilisha sana katika hatua za mwisho wa uongozi wake ambao huko nyuma ulionekana kuwa mzuri.

Hawa viongozi wapya wa hicho chama, kama Tundu Lissu, utakuwa na ujasiri gani wa kuanza kumlaumu kushindwa kuongoza wakati tokea achukue nafasi hiyo hajapata nafasi ya kuongoza!

Ni fikra za aina hii ndizo zinazokufanya uonekane kuwa 'partisan' asiyekuwa na fikra za wazi

Utalalamikia vipi hawa viongozi wakati huu kushindwa kufanya kama yale yaliyofanywa ; tena na hao hao vijana uliowataja hapo..., kwa sababu tu ya kwamba Mbowe hayupo sasa hivi katika uongozi? wa chama?

Sina hata chembe ndogo ya kutilia mashaka wala kuhoji juu ya uwezo wa John Mnyika na dhamira yake juu ya mstakabali wa taifa hili.
 
chadema wasicheze na uchumi hakuna mtanzania atawafungia macho awamu hii
Hili siyo swala la CHADEMA pekee.
Kama wewe unadhani hao akina Samia hawana damu za kuvuja na kufa; basi omba yasije kutokea zaidi ya yale ya Oktoba.
Usifikiri hiyo mitutu ya bunduki inayowazunguka hao waovu ni kinga ya kudumu ya kuitumia kwa wengine na kwao isiwarudie.

Hayo uliyoona Oktoba, hayatarudiwa tena katika mtindo huo. Na watu kama wewe hapo yatakuhusu.
 
Watoto cku hiyo mlale ndani mtuachie watu wazima tuandamane ili mjifunze kutoka kwetu. Hii vita sasa n ya watu wazima. Nimepita nikasikia mtu mmoja akiwa kashikilia chupa kubwa akitoa hiyo kauli
 
Nimeongea kikamilifu kabisa katika mstari huo. Naona hilo limekupita pembeni.
Haswa.
Hayo mengine uliyoweka huko juu ya lawama; utakapoachana na 'mentality' ya namna hiyo utakuwa na mawazo yasiyofungwa na mapenzi kwa mtu ambaye amejidhalilisha sana katika hatua za mwisho wa uongozi wake ambao huko nyuma ulionekana kuwa mzuri.
Hauoni kuwa hiyo ni the pot calling the kettle black? Kuna tofauti gani kati ya mimi na wewe ambae hausikii wala kuona linapokuja suala la Lissu?
Huo udhalilishaji unaozungumzia wa Mbowe ulikuwa orchestrated na huyo unaemtetea? Kuanzia ku insinuate kuwa Mbowe ni corrupt aliyehongwa na wakina Abduli. Alipoambiwa atoe ushahidi akasema aliyemwambia ni RIP. Ali hint ( ni too much of a lawyer kusema moja kwa moja) kuwa Mbowe alitumia pesa za Abduli kumuengua Msigwa katika uongozi. Msigwa huyo huyo akakimbilia kwa wakina Abduli. Alisema Mbowe hatafanikisha uchaguzi huru na kudai kuwa tayari ameanza kuuhujumu. Alikataa kuhudhuria mikutano ya kamati kuu. Alikataa kushiriki katika kampeni za uchaguzi wa chama chake katika uchaguzi wa 2024. Alimsingizia Mbowe kuwa ametumia pesa za chama kujinunulia gari. Na mambo mengi ya ajabu ajabu. Mimi binafsi siwezi kumkubali mtu wa aina hiyo.
Hawa viongozi wapya wa hicho chama, kama Tundu Lissu, utakuwa na ujasiri gani wa kuanza kumlaumu kushindwa kuongoza wakati tokea achukue nafasi hiyo hajapata nafasi ya kuongoza!
Aliweza sana kusimama na kumsema yule binti wa Nkasi. Aliweza sana kumtimua Catherine Ruge kwa sababu hakukubaliana nae. Aliweza kuhakikisha wote waliompinga wanashughulikiwa au wana nyamazishwa. Kiongozi mzuri anapimwa kwa hatua anazochukua mwanzo wa uongozi wake. Lissu alishindwa kwenye hilo kwa kushindwa kwake kuunganisha chama chake. Chadema imemgeuza Mbowe kuwa adui kuliko Samia. Mtu ambae alikipigania na kukifikisha chama mahali ambapo kilipo sasa hivi. Kwa mtazamo wangu ni kuwa ingawa sipingi kuwa Lissu ni courageous lakini ana chembe chembe za udikteta. It is either my way or the highway. Ni tofauti sana na Mbowe ambae alikuwa anakubali kukosolewa.
Ni fikra za aina hii ndizo zinazokufanya uonekane kuwa 'partisan' asiyekuwa na fikra za wazi
Heri kuwa partisan kuliko kuwa cultish.
Utalalamikia vipi hawa viongozi wakati huu kushindwa kufanya kama yale yaliyofanywa ; tena na hao hao vijana uliowataja hapo..., kwa sababu tu ya kwamba Mbowe hayupo sasa hivi katika uongozi? wa chama?
Usiniwekee maneno mdomoni. Ishu hapo sio Mbowe kutokuwa kiongozi ( ingawa kama mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu anabakia kuwa kiongozi), la hasha. Mbowe alishindwa uchaguzi na Lissu fair and square. Kama vijana waliopo sasa wanashindwa kufanya yaliyokuwa yakifanywa wakati wa Mbowe, tatizo ni la uongozi wa sasa. Usingeendekeza visasi visivyo na maana yote haya yasingetokea.
Sina hata chembe ndogo ya kutilia mashaka wala kuhoji juu ya uwezo wa John Mnyika na dhamira yake juu ya mstakabali wa taifa hili.
Huo ni msimamo wako. Lakini mimi natofautiana na wewe maana wakati wote mambo yalipokuwa magumu alikuwa anapotea conveniently. Kama ilivyo kwa viongozi wengi wa sasa. Wengi walionekana katika maandamano yaliyoidhinishwa na serikali na mara chache katika ile ambayo haikuidhinishwa. Viongozi waliopota hawakusubiri idhini. Watu kama Husna walipandisha bendera ya Chadema Chato wakijua thika yatakayoweza kuwapata. Wa sasa hivi wanabakia kulalamika tu.

Mnacho sahau ni kuwa hamna kiongozi anaeweza kusimama mwenyewe. Anahitaji kuwa na timu yenye weledi na iliyokuwa huru kumpa ushauri sahihi. Ofisi ya Katibu Mkuu sio Mnyika peke yake, ni timu yote iliyokuwa nyuma yake. Mpaka sasa hivi siwezi kuilinganisha na timu aliyokuwa nayo wakati wa Mbowe.
Mbowe ana mapungufu yake lakini ni kiongozi aliyekuwa na uwezo wa kuwainua na kuwa inspire waliokuwa chini yake. Hilo halipingiki.

Naombea Lissu katika muda huu aliokaa ndani awe ameona hilo na awekeze juhudi zaidi katika kuwahakikishia wenye mapenzi na chama chake wana nafasi katika chama hicho hata kama hawakubaliani nae 100%.

Amandla...
 
Hili siyo swala la CHADEMA pekee.
Kama wewe unadhani hao akina Samia hawana damu za kuvuja na kufa; basi omba yasije kutokea zaidi ya yale ya Oktoba.
Usifikiri hiyo mitutu ya bunduki inayowazunguka hao waovu ni kinga ya kudumu ya kuitumia kwa wengine na kwao isiwarudie.

Hayo uliyoona Oktoba, hayatarudiwa tena katika mtindo huo. Na watu kama wewe hapo yatakuhusu.
Mbona Octoba hukutoka mkuu? au uko nje ya nchi. Ungevunjwa hata mguu tungeona kweli uko serious!! 🤣
 
Lissu ataachiwa ila subirini dawa imuingie vizuri..... huwezi kushindana na serikali ukashinda. Si alisema anatoa masomo ya sheria mahamani sasa maandamano ya nini? Vijana msijindanganye mkaingia mkenge wa maandamano.
We Mjinga, subiri hayo maandamano yatangazwe uone ni nani ambaye dawa itamuingia vizuri.
 
Mimi sio mtaalamu wa uchukuaji wa picha mnato na mjongeo, ila ukiweka kamera karibu kama hivyo pua ya mzungumzaji inakuwa kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom