John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

Ni mwendo wa kuburuza kete kwa ground kete za rangi ya Simba zinaonekana zinatolewa supa na zile za yanga lakini kiuhalisia kete hizo zinatazamwa kwa matumaini makubwa ya kufika king ni vile tu katika uburuzaji hakuna kete muhimu iliyotangulia mbele

NB: Kama wataka maendeleo buruza kete za rangi ya yanga

Ila kama wapenda haki twende tuburuze kete za rangi ya Simba mwanakwetu kufika king ni lazima
 
Haswa.

Hauoni kuwa hiyo ni the pot calling the kettle black? Kuna tofauti gani kati ya mimi na wewe ambae hausikii wala kuona linapokuja suala la Lissu?
Huo udhalilishaji unaozungumzia wa Mbowe ulikuwa orchestrated na huyo unaemtetea? Kuanzia ku insinuate kuwa Mbowe ni corrupt aliyehongwa na wakina Abduli. Alipoambiwa atoe ushahidi akasema aliyemwambia ni RIP. Ali hint ( ni too much of a lawyer kusema moja kwa moja) kuwa Mbowe alitumia pesa za Abduli kumuengua Msigwa katika uongozi. Msigwa huyo huyo akakimbilia kwa wakina Abduli. Alisema Mbowe hatafanikisha uchaguzi huru na kudai kuwa tayari ameanza kuuhujumu. Alikataa kuhudhuria mikutano ya kamati kuu. Alikataa kushiriki katika kampeni za uchaguzi wa chama chake katika uchaguzi wa 2024. Alimsingizia Mbowe kuwa ametumia pesa za chama kujinunulia gari. Na mambo mengi ya ajabu ajabu. Mimi binafsi siwezi kumkubali mtu wa aina hiyo.

Aliweza sana kusimama na kumsema yule binti wa Nkasi. Aliweza sana kumtimua Catherine Ruge kwa sababu hakukubaliana nae. Aliweza kuhakikisha wote waliompinga wanashughulikiwa au wana nyamazishwa. Kiongozi mzuri anapimwa kwa hatua anazochukua mwanzo wa uongozi wake. Lissu alishindwa kwenye hilo kwa kushindwa kwake kuunganisha chama chake. Chadema imemgeuza Mbowe kuwa adui kuliko Samia. Mtu ambae alikipigania na kukifikisha chama mahali ambapo kilipo sasa hivi. Kwa mtazamo wangu ni kuwa ingawa sipingi kuwa Lissu ni courageous lakini ana chembe chembe za udikteta. It is either my way or the highway. Ni tofauti sana na Mbowe ambae alikuwa anakubali kukosolewa.

Heri kuwa partisan kuliko kuwa cultish.

Usiniwekee maneno mdomoni. Ishu hapo sio Mbowe kutokuwa kiongozi ( ingawa kama mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu anabakia kuwa kiongozi), la hasha. Mbowe alishindwa uchaguzi na Lissu fair and square. Kama vijana waliopo sasa wanashindwa kufanya yaliyokuwa yakifanywa wakati wa Mbowe, tatizo ni la uongozi wa sasa. Usingeendekeza visasi visivyo na maana yote haya yasingetokea.

Huo ni msimamo wako. Lakini mimi natofautiana na wewe maana wakati wote mambo yalipokuwa magumu alikuwa anapotea conveniently. Kama ilivyo kwa viongozi wengi wa sasa. Wengi walionekana katika maandamano yaliyoidhinishwa na serikali na mara chache katika ile ambayo haikuidhinishwa. Viongozi waliopota hawakusubiri idhini. Watu kama Husna walipandisha bendera ya Chadema Chato wakijua thika yatakayoweza kuwapata. Wa sasa hivi wanabakia kulalamika tu.

Mnacho sahau ni kuwa hamna kiongozi anaeweza kusimama mwenyewe. Anahitaji kuwa na timu yenye weledi na iliyokuwa huru kumpa ushauri sahihi. Ofisi ya Katibu Mkuu sio Mnyika peke yake, ni timu yote iliyokuwa nyuma yake. Mpaka sasa hivi siwezi kuilinganisha na timu aliyokuwa nayo wakati wa Mbowe.
Mbowe ana mapungufu yake lakini ni kiongozi aliyekuwa na uwezo wa kuwainua na kuwa inspire waliokuwa chini yake. Hilo halipingiki.

Naombea Lissu katika muda huu aliokaa ndani awe ameona hilo na awekeze juhudi zaidi katika kuwahakikishia wenye mapenzi na chama chake wana nafasi katika chama hicho hata kama hawakubaliani nae 100%.

Amandla...
Hii vita mngeiacha sasa haina maana yoyote kwa sasa maana wote ni wahanga wa ccm kubalini kutokukubaliana mambo yasonge
 
Hii vita mngeiacha sasa haina maana yoyote kwa sasa maana wote ni wahanga wa ccm kubalini kutokukubaliana mambo yasonge
Sio vita. Ni kubadilishana mawazo. Mijadala kama hii ilikuwa kawaida JF. Mnatofautiana kwa kuheshimiana. Shida siku hizi tukitofautiana ni lazima tutukanane. Na ndivyo ilivyo katika jamii yetu.

Amandla...
 
Hauoni kuwa hiyo ni the pot calling the kettle black? Kuna tofauti gani kati ya mimi na wewe ambae hausikii wala kuona linapokuja suala la Lissu?
Unilinganishe mimi na unazi ulionao wewe kwa Mbowe, mtu ambaye kapoteza hadhi yote aliyojijengea miaka yote?

Najuwa huwezi kuwa unasoma kila niliyokwishaandika humu JF; lakini ukitaka kujihakikishia unaweza kutafuta maandishi yangu kumhusu Lissu humu na utakuta kwamba sina ushabiki wa kinazi kwa mtu yeyote.

Pamoja na mapungufu yote aliyonayo Tundu Lissu; huwezi kumwondolea sifa ya kuwa na msimamo usioyumba katika kupigania HAKI za watu, hasa wanaoonewa.
Matatizo yooote aliyokutana nayo huko nyuma na hadi sasa yanatokana na msimamo wake huo imara; na hajarubuniwa kipumbavu kabisa kama alivyofanya Mbowe.

hiyo mizungushano yako mingine ya mabandiko marefu nilishasema huwa sina muda wa kupoteza nayo.
 
Mbona Octoba hukutoka mkuu? au uko nje ya nchi. Ungevunjwa hata mguu tungeona kweli uko serious!! 🤣
Unajuwa vipi kuwa sikutoka.
Na hata kama sikutoka; kazi ya kuwashughulisha wapuuzi nyie siyo ya "kutoka" pekee; lakini ulivyo nguruwe wewe huwezi kulijuwa hilo.
 
Nilikuwa sikusoma hadi huku chini; na bado humo katikati sijui umeweka nini.

Haya uliyoweka hapa yakitokea tena, hiyo itakuwa siyo CHADEMA tena; siyo ile ya Mbowe kabla ya kukengeuka, na wala haitakuwa CHADEMA ya Tundu Lissu kabla ya kusafisha chama na kuondoa takataka zote.

Ikitokea hayo unayoyatamani wewe, basi hakutakuwepo tofauti yoyote kati ya CCM na hilo dubwasha unaloliota wewe.
 
Wewe ulikwenda mitaani kuwaua waTanzania, ndiyo maana upo humu leo?
Hivi vitisho usifikiri ndiyo kinga itakayowaacha salama nyie.
Kelele hizi ungekuwa unajitokeza na kwenye maandamano bila shaka ungeshaikomboa nchi
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche, ametoa wito mzito kwa vijana na wanaharakati nchini kuanzisha kampeni kabambe ya kudai uhuru wa Tundu Lissu.

Akizungumza leo Aprili 9, 2026, kupitia baraza la kidijitali, John Heche amesisitiza kuwa muda wa kulalamika chini kwa chini umekwisha na sasa ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti za kitaifa.

Kiongozi huyo amewataka vijana wanaodai kuunga mkono harakati hizo kuacha kusemea pembeni, badala yake waanzishe kampeni kubwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani.

Ameelekeza kuandikwa na kubandikwa kwa vipeperushi kila kona ya mtaa ili kuonyesha mshikamano kwa Lissu ambaye amekaa ndani kwa mwaka mzima kwa tuhuma za uhaini. Jambo hili John Heche ameliita kuwa ni kumvua haki kiongozi huyo aliyekuwa akiwapigania wananchi bila kuwa na hatia yoyote.

John Heche amebainisha kuwa kampeni hiyo inalenga kumpa Lissu nguvu na imani kuwa watu anaowapigania ni sahihi na wako naye. Hata hivyo, ametoa onyo kali kuwa iwapo sauti yao haitasikilizwa kupitia kampeni hiyo, basi CHADEMA wataanzisha maandamano makubwa nchi nzima. Amesisitiza kuwa hawawezi kuendelea kukaa kimya wakati kiongozi wao akiteseka gerezani kwa mwaka mzima, akiamini kuwa ni lazima nchi itikisike ili haki itendeke.

Nonsense
 
Unilinganishe mimi na unazi ulionao wewe kwa Mbowe, mtu ambaye kapoteza hadhi yote aliyojijengea miaka yote?
Wanasema ukimnyooshea mtu kidole vinne vinakunyooshea mwenyewe. Inawezekana kuwa Mbowe amepoteza hadhi machoni mwako lakini bado kuna watu wengi bado wanamheshimu. Kutaka mtazamo wako uwe wa wote ni ishara ya kuwa uko kwenye cult na unazi mpofu. Wewe sio msemaji wa jamii.
Najuwa huwezi kuwa unasoma kila niliyokwishaandika humu JF; lakini ukitaka kujihakikishia unaweza kutafuta maandishi yangu kumhusu Lissu humu na utakuta kwamba sina ushabiki wa kinazi kwa mtu yeyote.
Ni kweli siwezi kusoma yote uliyoandika kama vile wewe hauwezi kusoma yote niliyoandika. Mimi najibu uliyoandika leo na hivi karibuni ulipokuwa unajadiliana na mimi kuhusu Lissu. Kwangu mimi, pasipo shaka, wewe ni mshabiki kipofu wa Lissu.
Pamoja na mapungufu yote aliyonayo Tundu Lissu; huwezi kumwondolea sifa ya kuwa na msimamo usioyumba katika kupigania HAKI za watu, hasa wanaoonewa.
Naam. Lakini hilo halimzuii kuwa dikteta kwa wale ambao anatofautiana nao. Yeye sio Mungu na kuna wakati anakosea. Kuendekeza visasi na kupenda kutukuzwa ni unyonge wake. Nyerere alikuwa na msimamo thabiti kwenye kutetea haki ya wananchi wake. Lakini hiyo haiondoi ukweli hakuwatendea haki watu wengi ambao walitofautiana nae. Jina la haambiliki halikutokea tu hewani.
Matatizo yooote aliyokutana nayo huko nyuma na hadi sasa yanatokana na msimamo wake huo imara; na hajarubuniwa kipumbavu kabisa kama alivyofanya Mbowe.
Msimamo upi shupavu? Na Mbowe karubuniwa kipumbavu kwenye lipi? Huko unakosema kurubuniwa ndio kumemfanya Lissu aweze kurudi na wanachama wengi wa Chadema waliokuwa ndani kutolewa gerezani na kufutiwa kesi zao. Huko kurubuniwa kipumbafu ndio kumeiwezesha Chadema kuweza kuwa na Makao Makuu. Unaweza kusema kuwa yeye ndie aliyerubuniwa na watu kama Lissu na Heche ambao pamoja na kuona mchango wa Mbowe kwa macho yao leo wanaangalia tu anapozodolewa na watu kama nyie? Wamefikia hatua ya kujaribu kukana mchango wa Mbowe katika kuokoa maisha ya Lissu alipopigwa risasi?

Mbowe amefungwa mara nyingi kuliko Lissu lakini leo mmesahau yote hayo? Mbowe amenyang'anywa na kupoteza mali nyingi kwa ajili ya kupigania watanzania lakini leo bila aibu mnajifanya hamkushuhudia yote hayo. Hata ukweli kuwa bila yeye uchaguzi uliompa Uenyekiti Lissu usingefanyika mnataka kuukana?

Mimi nilipoteza imani na Lissu nilipoona ananyamazia kampeni chafu iliyokuwa ikifanywa dhidi ya Mbowe na kujaribu kujifanya kuwa hakuhusika katika maamuzi mengi wakati yeye ndie aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na Makamu Mwenyekiti wake.
Alifikia hatua ya kutunga uongo kuhusu Wenje na Abduli kutaka kumhonga yeye na kumuonyesha orodha ya watu waliohongwa na Abduli! Lakini watu kama nyinyi mnashindwa kudai ushahidi kwa sababu ya unazi wenu. Sisi tulinusa panya tulipomsikia akimshukuru Abduli na kumwambia atakuwa rafiki yake wa maisha! Na mpaka leo hamna ushahidi zaidi uliotolewa wakati Sekretariati ya Chama iko chini yake! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mumpe.
hiyo mizungushano yako mingine ya mabandiko marefu nilishasema huwa sina muda wa kupoteza nayo.
Sasa kwa nini unaijibu? Wewe siku zote unaujua uandishi wangu sasa kwa nini unajibu mabandiko yangu kama hauna muda nao.

Ungenipotezea na kujikita kwenye sound bites wala nisingekusumbua. Lakini hauwezi kwa sababu unajua nasema ukweli na kuwa mimi sio bendera inayofuata upepo.

Tofauti yangu na wewe ni kuwa pamoja na mtazamo wangu kuhusu Lissu sisiti kusema amewekwa ndani kwa kuonewa.

Nitashukuru sana kama hautanijibu ili nisilazimike kuandika gazeti lingine.

Amandla...
 
owe amepoteza hadhi machoni mwako lakini bado kuna watu wengi bado wanamheshimu. Kutaka mtazamo wako uwe wa wote ni ishara ya kuwa uko kwenye cult na unazi mpofu. Wewe sio msemaji wa jamii.
Kwa kipimo chochote kile unachoweza kukitumia, hadhi ya Mbowe kama kiongozi ndani ya taifa hili ilipotea kabisa baada ya kununuliwa kijinga kabisa na huyo mwanamke ambaye ni zero kabisa.
 
Kwa kipimo chochote kile unachoweza kukitumia, hadhi ya Mbowe kama kiongozi ndani ya taifa hili ilipotea kabisa baada ya kununuliwa kijinga kabisa na huyo mwanamke ambaye ni zero kabisa.
Hayo ni maoni yako. Sio yangu. Mpaka sasa hivi haujaweza kutoa ushahidi wowote wa kununuliwa kwa Mbowe isipkuwa kuregurgitate tropes ambazo kwa mawazo yangu mimi binafsi zinaonyesha ulivyo cultist.

Amandla...
 
Huu ni mwiko kwangu.
Nikiona takataka yoyote popote nitaigusa nitakavyoona inafaa. Siwezi kuamrishwa nifanye nini.
Hauoni unavyo ji contradict? Mimi sijakuamrisha usisome wala kujibu bandiko langu. Wewe ndie uliyesema kuwa hauna muda wa kusoma ninachoandika. Mimi sina tatizo kabisa na wewe kusoma na kujibu mabandiko yangu ambayo bila shaka inakutia kichefuchefu. Hivyo hivyo, mimi nitakujibu nikiona unachoandika sio ingawa wakati mwingine huwa naamua kunyamaza tu. Hizo ni hazi zetu, wewe na mimi. Hakuna anaye muamrisha mwingine.
Ingawa hauwezi kuamini, mimi siko kwenye cult ya Mbowe ila siwezi kukubali achafuliwe kwa sababu tu watu wanamuabudu mtu mwingine. Kwenye hili, hamumtendei haki Mbowe.

Amandla...
 
"Mbowe achafuliwe"?
Naona hata hujui maana ya kuchafuliwa ni nini.
Mbowe kajichafua mwenyewe; hakuna aliyemchafua.
Tunarudia pale pale, kajichafua vipi? Kwa kukubali mualiko wa Samia kwenda Ikulu baada ya kutoka rumande? Huko alikozungumzia suala la haki? Na hamna anayepinga kuwa alipotoka kule aliwaeleza viongozi wenzake ( wakiwemo Lissu na Heche ambae alimuingiza kwenye Kamati Kuu pamoja na kuwa alishindwa katika uchaguzi wa Uenyekiti wa kanda yake) kuhusu yaliyojiri.
Kwa kuanza mchakato wa maridhiano? Ambao ulipitishwa na Kamati Kuu ya Chadema na mmoja wa wajumbe wa Chadema alikuwa Heche!
Alijiadhiri kwa kukazania kuwa hamna maridhiano bila Lissu, Lema n.k. kuhakikishiwa usalama wao wakirudi nchini? Au bila zuio la mikutano ya hadhara kuondolewa? Au bila wafuasi wa Chadema waliokuwa ndani kuachiliwa?
Alijidhalilisha alipoita maandamano na kuhudhuria ingawa serikali ilikuwa imeweka zuio? Hauoni hiyo ni tofauti na hii ya wakina Heche ambao wanasubiri kibali cha serikali kufanya maandamano?
Alijidhalilisha alipotoa pesa nyingi kuwezesha Mkutano Mkuu wa Chama chake kufanyika na kuhakikisha unafanyika katika mazingira ya uwazi na haki. Hiyo na pamoja na wakina Lema kutoa shutma za uongo na wakina Lissu ku insinuate kuwa hatukuwa wa haki?
Alijidhalilisha kwa kukubali kushindwa na kumpa pongezi aliyeshinda?
Alijidhalilisha kwa kukaa pembeni katika masuala ya chama chake ili kutokuwa beacon ya wanaotofautiana na uongozi wa sasa?

Alijidhalilisha kwa kutowajibu wakina Newton wanapomsemea ovyo au anapoona wazi wale waliokuwa kwenye kambi yake wakinyanyaswa?

Hapana, hizo juhudi zenu za kumchafua zitafanikiwa kwa wale watu wanaoamini kuwa kuna watu wanaoiba nyeti zao na wengine kama wao. Sio sisi wengine.

Natumaini kama kawaida hautasoma hili bandikokwa sababu ni refu.

Amandla...
 
Tunarudia pale pale, kajichafua vipi? Kwa kukubali mualiko wa Samia kwenda Ikulu baada ya kutoka rumande? Huko alikozungumzia suala la haki? Na hamna anayepinga kuwa alipotoka kule aliwaeleza viongozi wenzake ( wakiwemo Lissu na Heche ambae alimuingiza kwenye Kamati Kuu pamoja na kuwa alishindwa katika uchaguzi wa Uenyekiti wa kanda yake) kuhusu yaliyojiri.
Utakuwa na matatizo ya mahaba kama huelewi alivyojichafua Mbowe.

Hatuwezi kuwa tunarudiarudia kueleza mambo yale yale kwa mtu ambaye akili yake imezibwa kwa mahaba ya anayemshabikia.

Mbowe si alishindwa kwenye kura za uongozi wa chama. Hilo pekee halitoshi kukueleza kuwa walioshiriki kwenye uchaguzi huo waliona dosari za mabadiliko yasiyokuwa ya kawaida katika historia ya uongozi wake?

Unataka tuzungukezunguke tuuu humo humo kuelezana mambo ambayo kila mara tumeyasema?

Hii nayo ni mbinu ya kuchoshana kwenye mijadala, au ni kitu gani hiki!
 
Back
Top Bottom