Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Hapo ndipo unapokosea. Sio lazima kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa chama unaona dhahiri kuwa anakokipeleka sio. Na mbaya zaidi anapokuonyesha kuwa hahitaji ushauri wako. Njia sahihi ni kujitoa kwenye chama ili kiweze kuendelea kutekeleza fikra sahihi za Mwenyekiti. Kubaki ndani ya chama ingekuwa unafik. Waliobaki ndani ya chama huu ndio wakati muafaka wa kukiunda kwa namna wanavyotaka wao. Kutaka kuwalazimisha waunde juhudi za chama ambacho kimeonyesha dhahiri kuwa hakiwataki utakuwa unafik. Sasa hivi wanaendelea kujipanga kwa chaguzi zijao ambazo bila shaka watashiriki. Nyie endeleeni na mbinu yenu ya kususia. Muda ndio utakaoonyesha nani alikuwa sahihi.Hiyo ndio chungu tamu ya democracy lazima mkubali, siku zote kushinda ni mbinu kwahiyo mbinu ya lisu ilikuwa hiyo nyie mlioshindwa tafuteni mbinu nyingine kwa uchaguzi ujao kwa sasa ungeni juhudi za mwenyekiti aliekuwepo mjenge chama
Hauwezi kumpangia mtu aina ya ushauri ambao anapaswa kuwapa. Tofauti na unavyosema ni upande wenu ndio unashinda ukimlaumu Mbowe ( mara kwa nini alihudhuria tamasha, au kwa nini hajaonekana Mahakamani) wakti sijamsikia Mbowe akilalamika popote. Wengi wa wale waliotofautiana na agenda za Mwenyekiti wa sasa hivi wamejitoa kwenye chama. Wao wanaeleza mpambano dhidi ya kukitoa CCM madarakani na nyie endeleeni na mbinu zenu. Wao wamesema wako wazi kushirikiana na chama kinine chochote ili kutimiza adhma hii. Nyinyi mnataka wa capitulate na kuwaunga mkono. Hiyo haitatokea. Kubalini hilo na waacheni waendelee na shughuli zao.Shusheni pumzi ondoeni lawama unganeni na walioshinda mtembeleeni mwenyekiti toeni ushauri kwa waliokuwepo madarakani (ushauri wa kujenga na sio lawama za mbowe) endelezeni mapambano aliyoyaanzisha mwenyekiti unganeni nae katika kuwauma jino kwa jino ccm mwisho mtafanikiwa kuitoa madarakani
Wana msimamo ndio maana wanakataa kuusujudia uongozi wa chama chao cha zamani kama ambavyo wanavyokataa kusujudia chama tawala. Haijalishi dikteta kavaa nguo gani, anabaki kuwa dikteta tu.Mwisho kuweni na misimamo sio kuwa vigeugeu
Amandla...