John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

Mimi naamini kuwa hamna mtu anaogopwa na CCM kama Mbowe. Na wale wanaofanya juhudi za kumchafua ni ama wanafanya kazi ya CCM bila kujua au wako ndani ya CCM.

Hawa watu walishindwa kustuka pale wafuasi wa CCM walipokuwa wakifanya kampeni za wazi ili achaguliwe badala ya Lissu. Wanadhani CCM ni wajinga kiasi kuwa wafuasi wa Chadema watampigia kura mtu wanae mpigia debe?

Lengo lilikuwa ni wanachama wa Chadema kumkimbia Mbowe kama ukoma kwa kuhofia kuwa atakuwa kibaraka na hivyo kumpigia kura waliyemtaka. Na ndivyo ilivyo tokea.

Na kweli aliyeshinda haku wa disappoint. Matamko yake yaliwapa sababu ( ingawa haikuwa na mashiko) kumtia ndani. Kukaza shingo kuhusu kusaini miongozo ya uchaguzi ukawapa loophole ya kukiondoa chama katika uchaguzi. Kutoshiriki kwao kumewaondolea njia moja ya kupata pesa za kuendesha chama na kuweza kujiandaa kwa ajili ya chaguzi za 2029 na 2030.

Kile kiburi cha kujiona wanajua kila kitu ndio kimewaponza. Walisahau kuwa unapopambana na chama dola unatakiwa kuwa strategic.

Amandla...
 
Kuna Kenge washaanza kusema ati hawataki maandamano kisa kesi ipo mahakamani tusubiri.

Kama mnavyojua CCM washaanza kupitisha hela aka ngawila kwa baadhi ya makada wa CDM - kipindi cha mavuno kishaanza, neema imefinuliwa.
 
Utakuwa na matatizo ya mahaba kama huelewi alivyojichafua Mbowe.
Nilijua hauwezi kujizuia kunisoma.
Hatuwezi kuwa tunarudiarudia kueleza mambo yale yale kwa mtu ambaye akili yake imezibwa kwa mahaba ya anayemshabikia.
Hapo hatuna tofauti maana hata wewe hautaki kusikia lolote dhidi ya unaemshabikia.
Mbowe si alishindwa kwenye kura za uongozi wa chama. Hilo pekee halitoshi kukueleza kuwa walioshiriki kwenye uchaguzi huo waliona dosari za mabadiliko yasiyokuwa ya kawaida katika historia ya uongozi wake?
Tangu lini kushindwa kwenye uchaguzi ni kudhalilika. Trump alishinda kwa kishindo na sasa hivi wako wengi wanaojutia kura zao. Na unasahau kuwa tofauti ya kura kati yake na Lissu haikuzidi 10. Ule uchaguzi haukuwa full throated endorsement ya Lissu. Lissu alitakiwa kutambua kuwa kuna idadi ya kutosha iliyokuwa inamuunga mkono. Kuongoza kama vile alipata 98% ya kura ndio kumemponza.
Unataka tuzungukezunguke tuuu humo humo kuelezana mambo ambayo kila mara tumeyasema?

Hii nayo ni mbinu ya kuchoshana kwenye mijadala, au ni kitu gani hiki!
Mimi narudia kwa sababu naona unachosema hakina mashiko. Sina uwezo wa kukulazimisha kuendelea na mjadala. Kama umechoka uko huru kuachana nao.

BTW haujajibu hata hoja moja niliyoileta zaidi ya kusema tu kuwa Mbowe alijidhalilisha. Nilitegemea zaidi kutoka kwako. Unfortunately, unaongea kama chawa katika hili suala.

Amandla...
 
Kuna Kenge washaanza kusema ati hawataki maandamano kisa kesi ipo mahakamani tusubiri.

Kama mnavyojua CCM washaanza kupitisha hela aka ngawila kwa baadhi ya makada wa CDM - kipindi cha mavuno kishaanza, neema imefinuliwa.
Chadema sio waandamanaji. Bila kupewa kibali na serikali hawajitokezi.

Amandla...
 
Haujajibu. Kusema kuwa umejibu hakumaanishi kuwa umejibu. Au haujaeleweka. Ili kukata mzizi wa fitna weka quotes za mahali ulipojibu.

Amandla...
Huko unakokuita kukata mizizi kwa mtu kama wewe hakupo inapomhusu Mbowe, hili nililitambua toka siku nyingi humu.
 
Huko unakokuita kukata mizizi kwa mtu kama wewe hakupo inapomhusu Mbowe, hili nililitambua toka siku nyingi humu.
Hauna ushahidi. Haujawahi kuweka kitu kama hicho. Una rudia rudia tu yanayoandikwa na cultists wengine. Ungekuwa nao ungeweka ili kuninyamazisha.

Amandla...
 
Sio vita. Ni kubadilishana mawazo. Mijadala kama hii ilikuwa kawaida JF. Mnatofautiana kwa kuheshimiana. Shida siku hizi tukitofautiana ni lazima tutukanane. Na ndivyo ilivyo katika jamii yetu.

Amandla...
Mambo ya mbowe vs lissu yashaisha nguvu zielekezwe sehemu moja maana hata mjadili vipi lisu ndio mwenyekiti na mbowe ni mstaafu kwa sasa nguvu zielekezwe against ccm ndo wahanga wa vyama pinzani vyote nchini
 
Ulitoka ukaandamana jf.
Na sasa unataka waende field wengine wewe urudi hapa kuripoti
Wewe unaonaje? Itapendeza sana ukanipa location na picha yako nikufuatilie siku utakayoandamana ili nikufanyie coverage.
 
Mambo ya mbowe vs lissu yashaisha nguvu zielekezwe sehemu moja maana hata mjadili vipi lisu ndio mwenyekiti na mbowe ni mstaafu kwa sasa nguvu zielekezwe against ccm ndo wahanga wa vyama pinzani vyote nchini
Uko sahihi. Lakini ukweli ni kuwa Chadema haiwezi kuing'oa CCM bila kuunganisha nguvu na wale waliotofautiana nao. Imefika mahali Chadema iko tayari CCM ishinde uchaguzi kuliko Ruge ashinde.

Majeraha hayatapona kama Chadema inaendelea kukaa kimya ( na wakati mwingine kuunga mkono) pale waliokuwa wanachama wao na hata Mwenyekiti aliyeshindwa uchaguzi wanapozodolewa na kutukanwa. Mshindi mara zote atakuwa CCM.

Inaelekea kwa Chadema ya sasa ni heri CCM aendelee kutawala kuliko Chaumma au ACT-WAZALENDO washinde uchaguzi. Hapo ndipo ninaposhindwa kuwaelewa.

Amandla...
 
Uko sahihi. Lakini ukweli ni kuwa Chadema haiwezi kuing'oa CCM bila kuunganisha na wale waliotofautiana nao. Imefika mahali Chadema iko tayari CCM ishinde uchaguzi kuliko Ruge ashinde. Majeraha hayatapona kama Chadema inaendelea kukaa kimya ( na wakati mwingine kuunga mkono) pale waliokuwa wanachama wao na hata Mwenyekiti aliyeshindwa uchaguzi wanapozodolewa na kutukanwa. Mshindi mara zote atakuwa CCM.

Inaelekea kwa Chadema ya sasa ni heri CCM aendelee kutawala kuliko Chaumma au ACT-WAZALENDO washinde uchaguzi. Hapo ndipo ninaposhindwa kuwaelewa.

Amandla...
Hiyo ndio chungu tamu ya democracy lazima mkubali, siku zote kushinda ni mbinu kwahiyo mbinu ya lisu ilikuwa hiyo nyie mlioshindwa tafuteni mbinu nyingine kwa uchaguzi ujao kwa sasa ungeni juhudi za mwenyekiti aliekuwepo mjenge chama

Shusheni pumzi ondoeni lawama unganeni na walioshinda mtembeleeni mwenyekiti toeni ushauri kwa waliokuwepo madarakani (ushauri wa kujenga na sio lawama za mbowe) endelezeni mapambano aliyoyaanzisha mwenyekiti unganeni nae katika kuwauma jino kwa jino ccm mwisho mtafanikiwa kuitoa madarakani

Mwisho kuweni na misimamo sio kuwa vigeugeu
 
Back
Top Bottom