John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

John Heche: Tusiposikilizwa, tutaitikisa nchi kwa maandamano; Lissu aachiwe huru

Watanzania na hasa watanganyika tuacheni uoga wa kutengenezewa. Tunaburuzwa sana pasi na sababu kwa kakikundi cha walafi wa mali na madaraka. Tuamkeni wote kwa umoja wetu kuupinga kwa nguvu zetu zote bila kujali itikadi na dini zetu tuukatae huu ukoloni wa mtu mweusi.
Kupitia Lissu tutajikomboa hakika. Amkeni.
 
Ko Lissu kashindwa kujipambania kwa ujuaji mwingi wa sheria?? 🤣🤣🤣
 
Lissu ataachiwa ila subirini dawa imuingie vizuri..... huwezi kushindana na serikali ukashinda. Si alisema anatoa masomo ya sheria mahamani sasa maandamano ya nini? Vijana msijindanganye mkaingia mkenge wa maandamano.
 
Inatakiwa sasa hiyo "ari" ionekane.

Hilo kundi ndani ya chama hicho, kama lipo, limepoa sana wakati huu. Heri hata lile la wanawake. Wamepigwa mabomu ya machozi; lakini wameonyesha kuwa wapo.

Humu JF ni kama hao vijana wanawaogopa sana akina Mshamba na vilaza wengine waliokuja humu kuvuruga mijadala.
Kuna tatizo; pengine linalotokana na uongozi wa kundi hilo, au msukumo ndani ya chama kulisimamia na kuwa mbele ya chama chao.

Wewe tazama mada kama hii inakosa uchangiaji wa kutosha. Kuna tatizo gani?
Kwa mtazamo wangu Chadema ya Mbowe ilikuwa na ari zaidi ya hii ya sasa. Hata wakati Mbowe amewekwa ndani waliendelea kupambana. Inawezekana kuwa ile ilikuwa zaidi ya ground wakati hii ya sasa ni ya matandao, wasomi n.k.

Ushauri wangu ni uongozi wa sasa ushirikiane na wale ambao walitoka kwenye chama hicho baada ya kutofautiana strategies. Ni wakati wa kukaa na watu kama Aisha Madoga, Yosepher Komba, Catherine Ruge, Sigrada, Susan Kiwanga ili washirikiane na waliokuwa wenzao ndani ya Bawacha kuongoza mpambano wa kudai haki nchini mwetu. Hata Halima anaweza kusaidia. Huu ni wakati wa kuunganisha nguvu za uongozi wa sasa wa Bawacha ili kurudisha moto wa watu kama Husna Said wa Chato n.k.

Amandla...
 
Kiungo muhimu wa chama na JF umebaki wewe na hawa wachache wanaoweka maswala ya chama na viongozi wao; kama huyu 'Waufukweni'.

Lakini siku za karibuni, ukaribu wako na yanayoendelea huko kwenye chama hauonekani sana; pengine kwa sababu zilizopo zinazokibana chama.
Kampeni hii, jipange vizuri.
Ni kweli Nilikuwa nje ya Nchi kwa muda, hata hivyo kupigwa pini kwa jf kulitikisa kidogo mtandao , unajua lengo letu la kuandika humu ni kufundisha wajinga ili wajue haki zao, sasa masikini Wengi wa ccm ambaol tuliwalenga hawaingii jf
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche, ametoa wito mzito kwa vijana na wanaharakati nchini kuanzisha kampeni kabambe ya kudai uhuru wa Tundu Lissu.

Akizungumza leo Aprili 9, 2026, kupitia baraza la kidijitali, John Heche amesisitiza kuwa muda wa kulalamika chini kwa chini umekwisha na sasa ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti za kitaifa.

Kiongozi huyo amewataka vijana wanaodai kuunga mkono harakati hizo kuacha kusemea pembeni, badala yake waanzishe kampeni kubwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani.

Ameelekeza kuandikwa na kubandikwa kwa vipeperushi kila kona ya mtaa ili kuonyesha mshikamano kwa Lissu ambaye amekaa ndani kwa mwaka mzima kwa tuhuma za uhaini. Jambo hili John Heche ameliita kuwa ni kumvua haki kiongozi huyo aliyekuwa akiwapigania wananchi bila kuwa na hatia yoyote.

John Heche amebainisha kuwa kampeni hiyo inalenga kumpa Lissu nguvu na imani kuwa watu anaowapigania ni sahihi na wako naye. Hata hivyo, ametoa onyo kali kuwa iwapo sauti yao haitasikilizwa kupitia kampeni hiyo, basi CHADEMA wataanzisha maandamano makubwa nchi nzima. Amesisitiza kuwa hawawezi kuendelea kukaa kimya wakati kiongozi wao akiteseka gerezani kwa mwaka mzima, akiamini kuwa ni lazima nchi itikisike ili haki itendeke.

Nani huyo wa kuacha mishe zake kahangaikie Wanasiasa? Labda kama hajitambui
 
Free Tundu Antiphas Lissu
 
Back
Top Bottom