John Heche vs Dkt. Slaa: Je, ni kweli utekaji, kupotea kwa watu na kupigwa risasi Tundu Lissu Septemba, 2017 ni 'INSIDE JOB' ya CHADEMA wenyewe?

Mimi siyo Mwanasheria, lakini kama nimevamiwa na Majambazi na kushambuliwa kwa risasi anayeshitaki shambulizi langu ni DPP au mimi mwenyewe ?
Wewe unaripoti tukio, polisi wanachunguza na kuandaa ushahidi. Then wanasukuma kwa DPP kufungua shauri baada ya kuona kuna kesi ya kujibu. Wewe unabaki shahidi tu.
 
Mimi siyo Mwanasheria, lakini kama nimevamiwa na Majambazi na kushambuliwa kwa risasi anayeshitaki shambulizi langu ni DPP au mimi mwenyewe ?
Tunakusaidia kuficha upumbavu

Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:

  • (i)Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
  • (ii)Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
  • (iii)Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
  • (iv)Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
  • (v)Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
  • (vi)Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenyetija katika mashtaka ya jinai;
  • (vii)Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
  • (viii)Kuteua na kutenguamamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
  • (ix)Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masualaya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
  • (x)Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
  • (xi)Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
  • (xii)Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiii)Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiv)Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
  • (xv)Kuandaa na kuwasilishakwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
  • (xvi)Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka.
 
Asipoelewa akatwe masikio au atandikwe bakora salasini na tisa shingoni.
 
Wewe unaripoti tukio, polisi wanachunguza na kuandaa ushahidi. Then wanasukuma kwa DPP kufungua shauri baada ya kuona kuna kesi ya kujibu. Wewe unabaki shahidi tu.

Na chadema/Tundu Lisu wameshafanya yepi mpaka sasa hivi kwenye hayo ulioyataja kwa maana Polisi wamesema chadema/Tundu Lisu hawatoi ushirikiano wowote kwa mfano aliyekuwepo kwenye tukio wamemficha na hawataki kuruhusu aje Polisi kuhojiwa sasa Polisi wafanye nini ?

Nimevamiwa na majambazi Polisi wanataka kunihoji nakataa na kukimbia kijificha, Polisi wafanyeje sasa ?
 
Hao polisi wamefanya jitihada gani za kuonana naye?Au wanatoa maneno tu kama utoavyo weye?
 
Haya matapishi yapeleke Facebook. Humu watu wenye IQ ndogo kama yako hawatakiwi.
 
Mara hii umehamisha magoli,hoja yako ilikuwa kwa nini chadema haiwashitaki
 
Msaliti aliyezoea usaliti ni ngumu kuuacha Hadi atambue kama ni kosa,kama hajaweza tambua bado ataendelea.
 
Hao polisi wamefanya jitihada gani za kuonana naye?Au wanatoa maneno tu kama utoavyo weye?

Tundu Lisu/chadema wamemchukuwa kwenda naye kwanza Nairobi halafu Ubelgiji kwa hiyo ulitaka Polisi waende Ubelgiji kumfwata wakati muhusika mwenyewe Tundu Lisu ndiyo anayemficha ? Polisi wana kazi nyingi za kufanya kama anayeshitaki hataki kutoa ushirikiano for whatever reason wanaendelea na mambo mengine ambayo ni mengi sana tu hata yanawazidia!
 
Nimekwambia hata zile empty heads za risasi waliokota CDM na kuondoka nazo? Kazi ya police forensic bureau ni nini kama siyo kuchunguza matukio complex kama yale? Footage za CCTV zingewaelekeza polisi kama walikuwa ba nia yoyote ya kujua undani wa like tukio. Kwa mfano Lissu angekufa wangemhoji nani? Uchunguzi usingefanyika kwa sababu victim kafa?
 
Alimchukua akaondoka naye?Hali yake uliifahamu ilikuwaje huyo Lissu?Angewezaje kufanya hayo?Kama polisi wana kazi nyingi basi ni vema waendelee nazo na waache kuulizauliza shauri hilo.Kama ni kweli na si kwamba unawasemea kama vile wao hawana ubongo.
 
Alimchukua akaondoka naye?Hali yake uliifahamu ilikuwaje huyo Lissu?Angewezaje kufanya hayo?Kama polisi wana kazi nyingi basi ni vema waendelee nazo na waache kuulizauliza shauri hilo.Kama ni kweli na si kwamba unawasemea kama vile wao hawana ubongo.

Chadema/Tundu Lisu walimchukuwa dereva kwenda naye kwanza Nairobi halafu Ubelgiji haya siyo maneno yangu nimesikia kupitia Tundu lisu mwenyewe!
 

Lakini dereva yupo hai na alikwepo kwenye tukio!
 
Kuna ugumu gani kumhoji sasa? Tuna interpol, tuna ubalozi kule kucoordinate hilo suala kama wangetaka.

Utamuhoji mtu usiyemuona ? Na kwa nini Polisi wapitie yote hayo kwani hawana kazi nyingine za kufanya ? Kama anayeshitaki hataki kutoa ushirikiano wanaendelea na kesi nyingine ambazo ni nyingi hata zimewazidia!
 
Utamuhoji mtu usiyemuona ? Na kwa nini Polisi wapitie yote hayo kwani hawana kazi nyingine za kufanya ? Kama anayeshitaki hataki kutoa ushirikiano wanaendelea na kesi nyingine ambazo ni nyingi hata zimewazidia!
Kazi ya polisi ni kutafuta ukweli kwenye tukio lolote na kuchukua hatua. Suppose kama CDM ilihusika polisi watapate ukweli bila kufanya uchunguzi kivyao? Kwamba polisi inaweza kunyamazia uhalifu simply because mhusika amekaa kimya?! Haipo namna hiyo. Katika kutafuta ushahidi wa tukio lolote la kihalifu polisi huwa hawabembelezi ikibidi hutumia nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…