Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Hii ndio comment nilikuwa naitafuta. Chadema wanatakiwa kujenga vijana wazalendo wanaojua sheria na sio shari.Hao jamaa ni njaa tu, hawana nia ya kweli ya mageuzi…
This is a killer ya chadema, makapi na mamluki
Chakandumuz jizaeni upya by texturing youths wasiopenda matusi na vurugu - na wawe wanajiandaa kuwa viongozi kifikra, vitendo na falsafa
10 years down the road watachukua dola
Heche anawaamini hao watu? Yaani kama Heche awaamini waliokatwa atakuwa ni mjinga namba mojaMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa kwenye mchakato wa uteuzi wamekuwa wakimpigia simu wakilalamikia mwenendo wa chama hicho na kueleza matumaini yao kwa CHADEMA.
Akizungumza nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2025 mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, Heche amesema:
“Tupiganie haki kwa sababu hakuna aliye salama. Jana kuna watu wa CCM wamenipigia wanasema, ‘kwanini hampeleki chama kwenye uchaguzi, sisi tungekimbia kuja huku’. Hawa walikuwa kwenye utawala, lakini sasa wameonja maumivu, ndiyo wanajua kwamba CHADEMA ndiyo chombo cha kuwasaidia.”
Heche amesisitiza kuwa chama chao kitaendelea kupigania haki na kusimama na Tundu Lissu, akibainisha kuwa licha ya Lissu kuwa na haki ya kuwa huru, bado kuna mazingira yanayozuia maamuzi huru kufanyika mahakamani.
Video: Jambo TV
Hajasema kwamba anawaamini. Msisitizo wake ni namna hao watu walivyogundua kuwa ni kweli CCM haitendi haki. Period!Heche anawaamini hao watu? Yaani kama Heche awaamini waliokatwa atakuwa ni mjinga namba moja
CCM ni matapeli tupuHajasema kwamba anawaamini. Msisitizo wake ni namna hao watu walivyogundua kuwa ni kweli CCM haitendi haki. Period!
Amesema wanampigia na siyo kuwaaminiHeche anawaamini hao watu? Yaani kama Heche awaamini waliokatwa atakuwa ni mjinga namba moja
Kikwete hasikilizi mtuSi wakalalamike ndani ya CCM penyewe
Sasa wanampigia heche akiwa kama nani? Yn point ya hao ccm kumpigia Heche ni ipi?Amesema wanampigia na siyo kuwaamini
Matusi gani CHADEMA Huwa wanatukana?Hao jamaa ni njaa tu, hawana nia ya kweli ya mageuzi…
This is a killer ya chadema, makapi na mamluki
Chakandumuz jizaeni upya by texturing youths wasiopenda matusi na vurugu - na wawe wanajiandaa kuwa viongozi kifikra, vitendo na falsafa
10 years down the road watachukua dola
Hao vijana wapo nchi gani au mnataka wakawatoe Kenya.Hii ndio comment nilikuwa naitafuta. Chadema wanatakiwa kujenga vijana wazalendo wanaojua sheria na sio shari.
Vijana wenye mtazamo wa utulivu lakini ambao ni wabishi na wafanya maamuzi sampuli za akina Martin Luther king Jr.
Vijana wanatakiwa wasome sheria za inchi na kujieleza kwa kwa kuzijua lakini pia wajue madhaifu ya hizo sheria. Na ndani ya Chadema kuwa na shuffling ya uongozi kusiwe na sura zile zile kwenye uongozi miaka yote.
Wajitahidi pia hawa vijana wasiwe ni wahuni wawe wachapa kazi na wanaojua kujituma.
Wanaogopa tu mpama muda huu wangekuwa wameshahamia NRNE.Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokatwa kwenye mchakato wa uteuzi wamekuwa wakimpigia simu wakilalamikia mwenendo wa chama hicho na kueleza matumaini yao kwa CHADEMA.
Akizungumza nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2025 mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Lissu, Heche amesema:
“Tupiganie haki kwa sababu hakuna aliye salama. Jana kuna watu wa CCM wamenipigia wanasema, ‘kwanini hampeleki chama kwenye uchaguzi, sisi tungekimbia kuja huku’. Hawa walikuwa kwenye utawala, lakini sasa wameonja maumivu, ndiyo wanajua kwamba CHADEMA ndiyo chombo cha kuwasaidia.”
Heche amesisitiza kuwa chama chao kitaendelea kupigania haki na kusimama na Tundu Lissu, akibainisha kuwa licha ya Lissu kuwa na haki ya kuwa huru, bado kuna mazingira yanayozuia maamuzi huru kufanyika mahakamani.
Video: Jambo TV
Nakuelewa sana kiongozi,kuanzia ulipokuwa bungeni mpaka sasa.Hoja zako zina nguvu sana