John Mnyika amuumbua Spika kwa kutoa ushahidi wa Ofisi ya Spika kupokea barua ya CHADEMA kuwavua ubunge wanachama wake

John Mnyika amuumbua Spika kwa kutoa ushahidi wa Ofisi ya Spika kupokea barua ya CHADEMA kuwavua ubunge wanachama wake

Spika Ndugai amesema uongo muda mchache uliopita haikuandika barua kwake kumtaarifu juu ya kuwafukuza uanachama wabunge waliofanya utovu wa nidhamu na kukiuka maadili ya chama. Huu ni ushahidi walipokea toka 14 Mei 2020.
Image

Chanzo:John Mnyika on twitter.
Sasa hiki kikaratasi hata mie si naweza nikakiandika tu sasa hivi na kukipost hapa?
Nyie watu vipi..
Alafu ishu kubwa inaandikwa kienyeji namna hii? Kama ndio kamemo hako ni dharau kwa spika ndio maana kakachania mbali..
 
Kinachomata ni maandishi yaliyomo katika hiyo karatasi na si quality ya karatasi husika.
 
Kinachomata ni maandishi yaliyomo katika hiyo karatasi na si quality ya karatasi husika.
Hata tundu lisu anaweza iandika sasa hivi na akaipost.. haina legitimacy yoyote...
Hongereni kwa kuiwasilisha bungeni kwa spika anyway...
 
Na ndio hawa wanaotuambia kuwa Mbowe alilewa kuanguka na kwamba hiyo ndio sababu ya Mbowe kuvunjika Mguu!!

Mods kwenye heading naomba mnisaidie isomeke kuwavua uanachama na si ubunge.
Thibitisha kuwa mbowe hakulewa
 
Sasa hiki kikaratasi hata mie si naweza nikakiandika tu sasa hivi na kukipost hapa?
Nyie watu vipi..
Alafu ishu kubwa inaandikwa kienyeji namna hii? Kama ndio kamemo hako ni dharau kwa spika ndio maana kakachania mbali..
Muogope Mungu ukiwa unakandamiza haki ya wanyonge
 
hili sio bunge bali genge la wahuni wa ccm walioko bungeni kusaidia ufisadi na uvunjifu wa sheria na katiba wa rais na viongozi wengine
 
Naona hujui maana ya dispatch. Anaepokea barua ndio anasaini kwenye dispatch ya yule aliyeleta barua kama uthibitisho kuwa amepokea. Kwa sababu hiyo ni sahihi kabisa kama hicho kitabu ni cha mbunge wa Kibamba. Dispatch ya Bunge inatumika kwa barua zilizotoka Bunge.

Amandla...
Bado hapo haija onesha uhalali au ukweli wowote kwamba hiyo picha ya dispatch ilikuwa dispatch halisi siyo ya kughushi.
Hata mimi naweza kughushi hizo sahihi nikaandika kama huyo jamaa kwenye dispatch yangu ya matumizi ya hapa nyumbani kwangu.
 
Tanzania kuna mambo ya ajabu sana.
Aliyeandika amesema ameandika na kufikisha.
Aliyeandikiwa anasema hajaandikiwa.
A lot of Nonsense!!! [emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani huwa tuna matatizo ya kutoelewa au kutotaka kuelewa. Sababu muandikiwa anakiri kuandikiwa, lakini uhalali kisheria wa kilichoandikwa ndicho anapinga uhalali wake.
 
Na ndio hawa wanaotuambia kuwa Mbowe alilewa kuanguka na kwamba hiyo ndio sababu ya Mbowe kuvunjika Mguu!!

Mods kwenye heading naomba mnisaidie isomeke kuwavua uanachama na si ubunge.
Kwa akili zako fupi, hiyo dispatch mtu hawezi kufoji? Yaani kitu gani kimekuthibitishia kwamba hiyo barua ilipokelewa Bunge? Mbona hajasema nani kasaini kupokea, aone kama hakuburuzwa mahakamani.
 
Spika Ndugai amesema uongo muda mchache uliopita haikuandika barua kwake kumtaarifu juu ya kuwafukuza uanachama wabunge waliofanya utovu wa nidhamu na kukiuka maadili ya chama. Huu ni ushahidi walipokea toka 14 Mei 2020.
Image

Chanzo:John Mnyika on twitter.
Hicho ki despatch hakina muhuri mtu yoyote anaweza kupokea
Afadhali hata angetuambia katuma kwa email rasmi ya spika kidogo tungeelewa,mfumo wa despatch ni wa kizamani sana
 
Spika Ndugai amesema uongo muda mchache uliopita haikuandika barua kwake kumtaarifu juu ya kuwafukuza uanachama wabunge waliofanya utovu wa nidhamu na kukiuka maadili ya chama. Huu ni ushahidi walipokea toka 14 Mei 2020.
Image

Chanzo:John Mnyika on twitter.

Ambao hawajui hawa wamevuliwa ni watu wajinga tu au wenye manufaa binafsi na sio ya nchi, bunge wala chama. Huu ndiyo ujinga ambao Mama anasema lazima uishe bunge linaonekana kama genge tu
 
Jamani...!! Mbona tunataniana??

Huo ndio ushahidi??

Jamani tuko mfongoni mtuache bhana!!
 
Mheshimiwa Mnyika, Katibu Mkuu Chadema:

Mara nyingi umekuwa unawaambia Watanzania kwamba wewe au kiongozi yeyote wa Chadema hamjawahi kusaini fomu za uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Sasa Naibu Spika amesema (na kwenye Hansard ya bunge kuna kumbukumbu) kwamba, hao wabunge mliosema mmewafukuza wameteuliwa na nyie.

Kwa nini ukiwa mtendaji mkuu wa Chadema, usipate barua ya uthibitisho kutoka bungeni kwamba hao wabunge husika walipeleka bungeni fomu za kuonyesha wameteuliwa na Chadema, na muombe nakala za hizo fomu?

Na mkishapata nakala, kama hamuwafungulii kesi ya kughushi fomu za ubunge ili kujipatia mshahara wa ubunge kitapeli, basi tutajua mmekuwa mnatudanganya na kwamba ni kweli mliwasainia hao wabunge hizo fomu.
 
Suala ya COVID-19 ni uhalifu ya kidola. Sasa hapo unamshtaki nani?

Umeshasahau yaliyotokea kwa Tundu Lissu alipoenda kumshtaki Speaker kuhusiana na stahiki zake ?
 
Kwani wakienda polisi kufungua kesi kwamba fomu zao zimeghushiwa na wahusika wanajipatia pesa kwa njia ya udanganyifu polisi wataacha kufungua jalada na kulipeleka mahakamani?

Kwani wewe, kama mfanyakazi wako akighushi nyaraka za ofisi au biashara yako huruhusiwi kupeleka hiyo issue polisi? Polisi wakikataa kuipeleka mahakamani hiyo issue ya Chadema, basi angalau watutangazie sisi wananchi tujue mambo yakoje !
 
Kama mwenyekiti Mbowe anaweza kuanguka kwa ulevi wa konyagi alafu akatangaza kwamba amepigwa na wasiojulikana unategemea nini?

Chama kimejaaa laana ya uongo kutoka juu hadi chini.
 
Back
Top Bottom