John Mnyika ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Benson Kigaila-NKM Bara na Salum Mwalimu NKM Zanzibar

Asante kwa wazo
Mkuu 'Molemo', ngoja nami nichangie mada hii ingawaje huenda nshachelewa.

Kama ni kweli, CHADEMA wameweza kuongeza namba ya wanachama wao hadi milioni sita hivi sasa; na kama juhudi hizo zinatokana na kazi anayofanya Katibu aliyepo sasa, hiyo sio kazi ya kubezwa harakaharaka.

Nakumbuka hata mimi nilishazungumzia ukimya wa katibu aliyepo sasa ngugu Mashinji, kwa sababu sote tumezoea siasa za matukio ya papo kwa hapo. Kama ni mtendaji mzuri, hata kama hasikiki mara kwa mara, sioni sababu ya kumuengua katika nafasi hiyo.

Badala yake, ni kwa chama kufanya utaratibu wa kumpata wa kujibu mapigo, kwa mfano Katibu Mwenezi - hivi CHADEMA hawana nafasi hii?

Jambo la pili ni hili. Inaonekana CHADEMA imebadilika sana na ndio sababu wengi wetu, hasa huku kwenye mitandao tunaona kama imedhoofika. Chama kinachoongeza wanachama hakiwezi kuitwa 'kimedhoofu', na hasa ukichukulia dhoruba zinazoelekezwa kukihujumu.
Wengi wetu bado tunataka damu zichemke kwa kila uchokozi unaofanywa juu ya chama; kwa mfano, zile bendera kushushwa, wengi wetu tungetaka mahali pale pasitoshe!

Ukiangalia jinsi Chama kilivyochukulia tendo lile, hata yule aliyeamrisha bendera zishushwe atakuwa anajisikia vibaya kabisa kwa kutopata alichodhamiria kitokee.
Kwa matendo kama haya, CHADEMA sasa inajipambanua kwa wananchi kuwa imekomaa. Wanaweza kuhimiri michokozo yote na wakaibadilisha kuwa ya faida kwao mbele za wananchi.

Wakati huu atakayefaidika zaidi kwa CHADEMA kufanya vurugu ni CCM, pamoja na kwamba CCM wanafanya hivyo maksudi ili wawamalize CHADEMA.

Kwa hiyo, uwepo wa Katibu mkuu usichukuliwe kuwa ni lazima ajionyeshe hadharani kila mara kujibu mapigo. Ndani ya CHADEMA wapo wengi tu wanaoweza kufanya kazi hiyo ya 'kujibu mapigo' bila ya kumhusisha katibu mkuu.

John wawili, wote wanaweza kuteuliwa kwa nafasi maalum ya kufanya kazi ya 'kujibu mapigo'.
 
Umeandika vema sana mkuu tena kwa Hisia.Naamini Mwenyekiti atafanya chaguo sahihi
 
Habari za Chadema zinachosha sisi tunajiandaa na majilio

Ndio ianayokubalika kwa ushawishi bila kutumia vyombo vya dola. Ukiona habari ya ccm au serikali inajadiliwa huku mitandaoni ni habari hasi, lakini nyingine zote hazina wachangiaji maana hamna mvuto, na mko madarakani bila ridhaa ya wananchi wengi.
 
Silinde is the right person

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hoja niliwahi itoa katika nyuz moja huko nyuma ...kuwa ni vema Katibu Mkuu au watendaji ndani ya vyama wasiwe wabunge ili uwajibikaji uonekane ...Kwangu Mimi Silinde n mzuri sana ...siasa anaijua vizuri na amekua kiongozi anafaa kuwa Katibu Mkuu..(A and I level alipiga division one ).
 
Kuna profesa mmoja anadai katokea jalalani ndio kabisaa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si lzima ila sema inafaa kuwa hivyo umri na uzoefu na ujengaji wa hoja nafikiri itakuwa sawa lakini vyovyote najua mwenyekiti ni mtu mwenye busara atakuwa amefanya mashuriano na Kamati kuu kabla maana pia unezateuwa mtu kamati kuu ikamltaa itakuwa fedheha.
 
Hii ni komenti ya mtu mzima kichwani, nimeipenda
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika vyema hata sina cha kuchangia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema ukweli mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…