KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu 'Molemo', ngoja nami nichangie mada hii ingawaje huenda nshachelewa.Asante kwa wazo
Kama ni kweli, CHADEMA wameweza kuongeza namba ya wanachama wao hadi milioni sita hivi sasa; na kama juhudi hizo zinatokana na kazi anayofanya Katibu aliyepo sasa, hiyo sio kazi ya kubezwa harakaharaka.
Nakumbuka hata mimi nilishazungumzia ukimya wa katibu aliyepo sasa ngugu Mashinji, kwa sababu sote tumezoea siasa za matukio ya papo kwa hapo. Kama ni mtendaji mzuri, hata kama hasikiki mara kwa mara, sioni sababu ya kumuengua katika nafasi hiyo.
Badala yake, ni kwa chama kufanya utaratibu wa kumpata wa kujibu mapigo, kwa mfano Katibu Mwenezi - hivi CHADEMA hawana nafasi hii?
Jambo la pili ni hili. Inaonekana CHADEMA imebadilika sana na ndio sababu wengi wetu, hasa huku kwenye mitandao tunaona kama imedhoofika. Chama kinachoongeza wanachama hakiwezi kuitwa 'kimedhoofu', na hasa ukichukulia dhoruba zinazoelekezwa kukihujumu.
Wengi wetu bado tunataka damu zichemke kwa kila uchokozi unaofanywa juu ya chama; kwa mfano, zile bendera kushushwa, wengi wetu tungetaka mahali pale pasitoshe!
Ukiangalia jinsi Chama kilivyochukulia tendo lile, hata yule aliyeamrisha bendera zishushwe atakuwa anajisikia vibaya kabisa kwa kutopata alichodhamiria kitokee.
Kwa matendo kama haya, CHADEMA sasa inajipambanua kwa wananchi kuwa imekomaa. Wanaweza kuhimiri michokozo yote na wakaibadilisha kuwa ya faida kwao mbele za wananchi.
Wakati huu atakayefaidika zaidi kwa CHADEMA kufanya vurugu ni CCM, pamoja na kwamba CCM wanafanya hivyo maksudi ili wawamalize CHADEMA.
Kwa hiyo, uwepo wa Katibu mkuu usichukuliwe kuwa ni lazima ajionyeshe hadharani kila mara kujibu mapigo. Ndani ya CHADEMA wapo wengi tu wanaoweza kufanya kazi hiyo ya 'kujibu mapigo' bila ya kumhusisha katibu mkuu.
John wawili, wote wanaweza kuteuliwa kwa nafasi maalum ya kufanya kazi ya 'kujibu mapigo'.