John Mnyika ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Benson Kigaila-NKM Bara na Salum Mwalimu NKM Zanzibar

Mtakumbuka kipindi ambacho Mnyika alikuwa mwiba mkali kwa Bwana mwenyekiti wa kudumu kwa kuhoji mambo ya siri ambayo wengi wao hawayajui ndani ya chama hicho na kutopata majibu ya kuridhisha kutoka kwa TOP leaders hali iliyompelekea kuonekana yuko kinyume na chama.

Baada ya vurumai kuzidi kuwa kubwa ndani ya chama hicho, hawa jamaa (MNYIKA na wenzake wawili akiwemo HECHE ) walidhamiria kujiengua chamani na kwenda Kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, kitu ambacho kingekuwa mwiba wa utosi kwa Mzee Baba mwenye chama chake. Baada ya mwenye chama kujua hilo aliwaza na kukuna kichwa ni njia gani atumie ili "SIRI" wanazozijua hawa jamaa zisije zikatoka nje ya mipaka yake ndipo alipoamua kuwapa vyeo vya karibu yake kama njia ya kuwaweka karibu nae na awasuuze nafsi zao pamoja na kuwatoa PEPO la kuhama chama.

Fadhila hii pia ilimkuta Bwana LISSU, mtakumbuka hivi karibuni mipango ya snitch ZITTO KABWE kujikomba na kujipendekeza kwenda Ubelgiji kumsabahi jaamaangu wa Singida mashariki haikuwa ya bure. Kulikuwa na mipango na mikakati iliyofanikiwa kumshawishi LISSU kujiunga nae na kulikuwa na kila dalili za LISSU kujiunga na ACT Wazalendo kwa ahadi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais 2020 kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bwana mwenyekiti alivyoona hayo akaamua kumtoa KAFARA bwana PROF SAFARI ili kummezesha ndoano na kumpa fadhila bwana LISSU ili aendelee kusalia chamani. Hii ni njia aliyoitumia Mwenyekiti na kuwafunga midomo kabisa kuhoji mambo ya ndani kabisa ya chama. Kongole kwa Mwenyekiti wa kudumu kwa kuwamezesha ndoano jamaa hawa na lets hope watafunga midomo yao kuhoji mambo mazito ya chama.

Na hii ndio CHADEMA Mpya. Pipooooooo's
 
Mbowe amteua Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA. Mh Mbowe amesema kuwa amefanya uteuzi huu kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA.

- Mh. John John Mnyika Katibu Mkuu

- Mh. Singo Benson Kigaila Naibu Katibu Mkuu Bara

- Mh. Salimu Mwalimu ameendelea kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

- Mh John Heche ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu

View attachment 1297914
Kutoka Kushoto: NAIBU K/MKUU ZANZ - Salum Mwalim , MAKAMU MWKT ZANZ - Said Issa Mohamed, MWENYEKITI - Freeman Mbowe, KATIBU MKUU - John John Mnyika, NAIBU K/MKUU BARA - Benson S. Kigaila
Hongera Mnyika!
Hapana shaka chama kimeteua mtu makini sana!
Hofu yetu wanaCHADEMA "wale original" sijui kama utaendana na madili ya MWENYEKITI.
Ninavyokujua ili uendane na Mwenyekiti itabidi ucompromise PRINCIPLES zako nyingi sana!!!
Vinginevyo yatakukuta ya Dr Slaa.
Haya ni dhahiri yatatokea iwapo utaamua kusimama na kuibeba dhamana yako ya UKATIBU MKUU inavyopaswa.
 
Sinilisema mapema? Haya sasa hiyo nifadhira ya myika make anajua hana jimbo mwakani. Myika ni mbunge
Andika vizuri Basi eeh! Hili jukwaa limevamiwa na ngumbaro! Hebu jisome ulichokiandika, hata hueleweki!
 
Mtakumbuka kipindi ambacho Mnyika alikuwa mwiba mkali kwa Bwana mwenyekiti wa kudumu kwa kuhoji mambo ya siri ambayo wengi wao hawayajui ndani ya chama hicho na kutopata majibu ya kuridhisha kutoka kwa TOP leaders hali iliyompelekea kuonekana yuko kinyume na chama.

Baada ya vurumai kuzidi kuwa kubwa ndani ya chama hicho, hawa jamaa (MNYIKA na wenzake wawili akiwemo HECHE ) walidhamiria kujiengua chamani na kwenda Kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, kitu ambacho kingekuwa mwiba wa utosi kwa Mzee Baba mwenye chama chake. Baada ya mwenye chama kujua hilo aliwaza na kukuna kichwa ni njia gani atumie ili "SIRI" wanazozijua hawa jamaa zisije zikatoka nje ya mipaka yake ndipo alipoamua kuwapa vyeo vya karibu yake kama njia ya kuwaweka karibu nae na awasuuze nafsi zao pamoja na kuwatoa PEPO la kuhama chama.

Fadhila hii pia ilimkuta Bwana LISSU, mtakumbuka hivi karibuni mipango ya snitch ZITTO KABWE kujikomba na kujipendekeza kwenda Ubelgiji kumsabahi jaamaangu wa Singida mashariki haikuwa ya bure. Kulikuwa na mipango na mikakati iliyofanikiwa kumshawishi LISSU kujiunga nae na kulikuwa na kila dalili za LISSU kujiunga na ACT Wazalendo kwa ahadi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais 2020 kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bwana mwenyekiti alivyoona hayo akaamua kumtoa KAFARA bwana PROF SAFARI ili kummezesha ndoano na kumpa fadhila bwana LISSU ili aendelee kusalia chamani. Hii ni njia aliyoitumia Mwenyekiti na kuwafunga midomo kabisa kuhoji mambo ya ndani kabisa ya chama. Kongole kwa Mwenyekiti wa kudumu kwa kuwamezesha ndoano jamaa hawa na lets hope watafunga midomo yao kuhoji mambo mazito ya chama.

Na hii ndio CHADEMA Mpya. Pipooooooo's
Mkuu inawezekana sana ukawa unajua kuandika Uzi mrefu kiasi hichoooo lakini nikuhakikishie HUU UZI NI UONGO AMBAO HAUJAWAHI KUTOKEA..........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lissu Singida.
Acha ulofa wewe mnyika ni wa mwanza??? Mnyika ni wa kaskazini mpare huyo.Kanda ya ziwa hakuna jina mnyika iwe kwa kurya,jita,kerewe,zinza,haya,luo wala sukuma
 
Back
Top Bottom