Uchaguzi 2020 John Mnyika: CHADEMA haijakaa na Tume ya Uchaguzi(NEC) na haina mpango wa kuteua wabunge Viti Maalum

Uchaguzi 2020 John Mnyika: CHADEMA haijakaa na Tume ya Uchaguzi(NEC) na haina mpango wa kuteua wabunge Viti Maalum

Hata huyo wa Nkasi lazima ajue ni chama kilichombeba, na msimamo wa chama ni kutoyatambua matokeo yote, kama hakithamini chama na wanachama waliokufa kwa ajili yake anathamini pesa kwanini asiunge juhudi aungane na watesi hatokuwa wa kwanza.
Hata yeye mbunge wa Nkasi wapo walioumia kwa ajili yake
 
Ndio ipo hivyo. Sijajua idadi halisi ya kura za chadema walizopata kwenye ubunge ila nahisi wanavuka 10%, hivyo wanaweza kuwa na wabunge wasiopungua 15.
Shida ilipo ni, majina ya wagombea viti maalum yalishapelekwa hivyo kinachofanyika ni sasa hivi kamati kuu kuamua katika yale majina ni kina nani wapite. Sasa inavyoonekana ni kama kuna watu wanatakiwa kupitishwa ilihali hawakugombea viti maalum
Wa kwanza viti maalum ambaye amepita ni halima mdee, sababu ya nafasi yake ya mwenyekiti bawacha. Hii nafasi unapata viti maalum moja kwa moja
wanachaguliwa kwa namba mkuu, ina maana jina la kwanza mpaka la 15 ndio watakaopitishwa!
 
Mkuu serious kabsa unahisi jiwe anateteleka na kususa kwenu?
Najua yeye ni care free kwa sababu anauhakika wa maisha yake, sisi wananchi wa kawaida tunaotegemea uimara wa muhimili wa bunge tusipopiga kelele ndio tukataopata shida.
 
Yes ni busura pia coz kama hawatapeleka means

Chama chao hakitasikika kwa miaka 5
Mkuu na ww unaamini unasikika kwa kwenda bungeni? Bunge hili hili lililo chini ya serikali ya Magufuli? Kumbuka bunge lenyewe sio live bali liko gizani. Lisu hakuwa bungeni zaidi ya miaka mitatu, mbona karudi na amesomeka tu? Wananchi sasa hivi tuna uelewa wa kutosha, tunajua fika hakuna jipya kwenye hilo bunge kibogoyo.
 
Je Chadema inaitambua ruzuku iliyotokana na uchaguzi inayoukataa?

Msiwape hiyo ruzuku, kama mliweza kuagiza kura halisi zisitangazwe huko vituoni, na kuagiza wapinzani kibao waenguliwe ili ccm wapite bila kupingwa, kipi kitawashinda kutowapa ruzuku? Yule dada aliyeshinda uchaguzi aachwe aende bungeni, maana hiyo ni sehemu ya yeye kupata hela za kuendesha maisha yake, na maadamu kaanza lugha za sintofahamu, aachwe aende asije kutumika kuharibu msimamo wa chama. Hao viti maalum, cdm watangaze kutokushiriki, maana ni kuhalalisha ule uchaguzi wa maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Kuna tukio la uongo ukifanya kumbuka nyuma umefanya nini.

Watu tumeshinda kwa kishindo,haya nini tena kuteua wabunge wa Vyama Pinzani kwa mfumo wa viti maalumu, nani amewaambia kuwa wananchi tuna shida na wabunge pinzani hapo bungeni.

Hamkuona kura zetu za kishindo juu yenu.
Pangeni viti maalumu hao hao kwa upande wetu hatuwahitaji sisi.
 
Ndio maana nikasema, hao wabunge watakaoitwa "viti maalum wa Chadema" kama watateuliwa, watakuwa na maswali ya kujibu.
Kwenye viti maalumu kinachozingatiwa ni idadi ya kura za wabunge wote kwa pamoja na siyo idadi ya wabunge.
 
Ila kweli maafrika ni manyani,nimefuatilia uchaguzi wa us kuanzia kampeni hadi kutangazwa mshindi sjasikia kama kuna mtu kapigwa huko au kuuawa au figisu zozote kisa uchaguzi
Haujasikia mgombea wa Republican akipinga matokeo?

Haujasikia mgombea kujitangaza kabla zoezi la uhesabuji kura halijaisha?

Alafu acha kuwakosea adabu wazazi wako kwa kuwaita manyani.
 
Faida inayotazamwa ni ya Tanzania siyo kununuliwa kupitia ruzuku.

"Upinzani ruzuku" ndiyo CCM inaoutaka na si "Upinzani wa kushika dola".

Chama chochote kuliko kubaki kuwa "chama ruzuku" ni bora hicho chama kife!, maana kitakuwa hakina faida kwa Wananchi
Exactly, naona hivi vitisho vya ruzuku vinatumika sana ili kuwafanya cdm waingie kwenye mtego. Sasa hivi taasisi nyingi humu nchini zinaongozwa kwa weledi duni, kwakuwa viongozi wake huwa wanatishiwa kuwa eti watatolewa kwenye hizo nafasi zenye ulaji. Na yote hiyo inatokana na katiba mbovu, ambayo inampa rais nafasi ya kumchagua na kumtoa yoyote amtakaye. CUF ya Maalim Seif ilisusia ule uchaguzi wa kihuni, mbona waliendelea kuwepo mpaka walivyohamia ACT?

Siwashauri cdm kupeleka Mbunge yoyote kwenye hilo bunge kibogoyo, maana kuwapeleka sasa hivi ni kupata faida ya muda mfupi, huku wakipoteza faida ya muda mrefu wa siasa za nchi yetu.
 
Utopolo uliofanyika kwenye uchaguzi huu haukubaliki.
Haukubaliki kwa nani?
Uchaguzi ufutwe, iundwe tume huru ya uchaguzi, kisha uchaguzi huru na wa haki ufanyike.
Ufutwe kwa kuwa mmekataliwa kwa aibu na wananchi? Tume ni huru sana, ndiyo maana mligombaniana kwenda kuchukua fomu za kugombea...
Vinginevyo, bunge liwe la kijani mtindo mmoja
Na kwa akili zenu hapo ndo mnawakomoa CCM eti!🤔🤔
 
Back
Top Bottom