Sio kweli, zungumzia Majimbo mengine yawezekana sababu mimi sikuwepo. Lakini nilifuatilia Jimbo la Hai zaidi ya miezi 8 kabla ya uchaguzi. Siku tatu kabla ya uchaguzi nilikuwa Hai na Bi Mkubwa wangu kwao ni Lyamungo Sinde.
Nilitembelea kata zote za Jimbo la Hai kuanzia Kashinsha, Ivaery, Masama Kusini, Masama Magharibi, Ng'uni, Matikoni, Uroki, Nkira, Aishi, Nshana, Mamba,Kalali, Uraa, Kisiki, Nkoraya, Sonu, Kyeeri, Nkuu, Kisereni, Mwowe, Nkwarungo, Nkweseko, Matikoni. Vijiji 162 kwa hiyo ni eneo kwanza nalijua, na linanihusu.
Hakuna matayarisho yeyote ya maana ya kuonyesha Mwenyekiti anagombea Jimbo hili. Kuanzia party organisation within constituency mpaka mawakala.
Mgombea ameondoka bila kutayarisha nani anawalipa mawakala.
Hakuna mafunzo ya Mawakala na wamechukuli chukuliwa randomly wengine hata sio wana Chadema. Na Bwana Mkuba kajikata hata kuwalipa hakuna. Mawakala 35 kwa Lyamungo Sinde na Mwowe Msikitini na Nkwarungo nilipa mimi bila kutayarishwa, lakini haini sumbui ndio Ukamanda.
Mengine ni usanii tuu. Tuache tutavuana nguo tuu, hapa sio mahala pake.