Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, John Mnyika kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (Twitter)
---
John Mnyika kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (Twitter) anaripoti:
Nimetaarifiwa usiku huu kuwa Mzee Ali Mohamed Kibao Mtaalamu katika Sekretariati CHADEMA amechukuliwa na watu walijitambulisha kuwa ni polisi(bila uniforms).
Walizuia basi la Tashrif alilokuwa amependa kutoka DSM kwenda Tanga kwa gari za kawaida wakaingia na kumfunga pingu.
Tunaendelea kufuatilia kupata taarifa kamili ikiwemo wamempeleka wapi. Nimetoa taarifa hii ya awali ili iwapo kuna yoyote alikuwepo kwenye basi au ana taarifa zozote kuhusu alipopelekwa atupatie au kutupa ushirikiano wa haraka.