John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

John Mnyika: Kiongozi wa CHADEMA Mzee Ali Mohamed Kibao, adaiwa kushushwa kwenye Basi na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana

Sasa watuchukuaje mtu kwenye basi halafu abiria wako mle mle? Na wamiliki wa basi wapo? Kwanini wasingeongozana mpaka kituo cha polisi ndio wakamuacha hapo? Kuna uwezekano watu wanatumia kivuli cha polisi kufanya utekaji na kulichafua jeshi la polisi.
 
Huu sasa ni ujinga.. basi linasimamishwa, mtu amafungwa pingu na watu wenye nguo za kiraia yeye anakubali tu? Abiria nao wanakubali tu?

Juzi dereva wa basi kauwawa huku abiria wake wakirekodi video wamekubali tu?

Watanganyika kwa ukondoo huu ni haki yenu kufanyiwa yanayofanywa na wenye mamlaka. Huu ni ujinga sio upole wala woga.
Inashangaza sana
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu, John Mnyika kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (Twitter)
---
John Mnyika kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (Twitter) anaripoti:

Nimetaarifiwa usiku huu kuwa Mzee Ali Mohamed Kibao Mtaalamu katika Sekretariati CHADEMA amechukuliwa na watu walijitambulisha kuwa ni polisi(bila uniforms).
Walizuia basi la Tashrif alilokuwa amependa kutoka DSM kwenda Tanga kwa gari za kawaida wakaingia na kumfunga pingu.
Tunaendelea kufuatilia kupata taarifa kamili ikiwemo wamempeleka wapi. Nimetoa taarifa hii ya awali ili iwapo kuna yoyote alikuwepo kwenye basi au ana taarifa zozote kuhusu alipopelekwa atupatie au kutupa ushirikiano wa haraka.

Huyu mzee picha yake haipo popote...?
 
Ngoja tusubiri labda polisi wameanzisha huduma ya kupokea watu kwenye vituo vya mabasi.
 
Wabadili mbinu!

Haiwezekani mtu mmoja anaumiza taifa Zima kwa kunyamazia wasiojulikana!
 
Fikiria kidunia zaidi

Ikiisha Teka Teka inakujaga chomachoma Shule we meku

Uwage mbele ya wakati meku 😂😂
Unasikitisha sana 'john'.
Wakati mwingine unaonekana kuwa kama mtu mwenye akili nzuri tu, na mtu mwenye kujuwa historia nzuri ya nchi hii; lakini mara moja bila kutabirika akili hiyo hiyo inabadilika na kuwa kama ya kichizi!

Mtu mzima, wa makamo sana; kama siyo mzee, utakuwaje na akili za aina hii?

Sasa kwa mfano angalia hayo uliyo andika hapo juu kama kuhalailisha ukichaa ulio kuingia ulipo weka habari tofauti kabisa na mada husika hapa.
WaTanzania kutekwa siyo jambo la kufanyia mzaha hata mara moja. Hata kama ni tofauti za kisiasa, hili haliwezi kamwe kuwa jambo la kufanyia dhihaka.

Niseme tu, unanisikitisha sana kuliko kunikasirisha.
 
Hajawahi kuwa na akili nzuri, Ni hivi hakuna Mwanaccm Mwenye akili nzuri
 
Chadema kwa kudeka, hivi makamanda wa wapi nyie
 
..Mnyika amesema Ali Mohammed Kibao, kiongozi wa Chadema, amekamatwa akiwa ktk basi la Tashrif la kutoka Dsm kwenda Tanga.

..bila shaka kuna wafanyakazi wa basi hilo, pamoja na abiria, wanaoweza kutoa taarifa zaidi kuhusu kilichotokea.
Hapo sasa!
 
Hajawahi kuwa na akili nzuri, Ni hivi hakuna Mwanaccm Mwenye akili nzuri
Hapana.

Mimi siamini hivyo hata mara moja.
Kuna waTanzania wengi sana ndani ya CCM ambao hawakubaliani na mambo ya namna hii; na uongozi wa hovyo kama huu.
 
mtu una dola una kila kitu bado unaogopa watu ambao hawana dola kisa maneno. afrika bado sanaaa ni dunia ya kima.
 
Back
Top Bottom