John Mnyika: Mambo CHADEMA tuliyozungumza na wenzetu wa CCM

Ona sasa SIASA haina uadui wa kudumu..hata sisi humu JF, wanazi wa sides zote kwanini tusifanye maridhiano? hivi tunagombania nini kwanza kwa faida ya nani.
 
Political giants kwa sasa JF hii ni CCM, CHADEMA NA SUKUMA GANG, fanyeni mauridhiano kuunga mkono maridhiano yanayoendelea..sabaya kuwa bailed out ni sehemu ya maridhiano pia na bado.
 
Mkutano ule wa Mei 20,2022 ,ni mwanzo wa mazungumzo ya timu mbili. Upande wetu CHADEMA tuliwasilisha ajenda mbili ya kwanza ni kurejeshwa kwa mchakato wa katiba ya nchi yetu na ya pili ni kujadili madhara ya miaka sita iliyogubikwa na ukiukwaji wa haki

Itakumbukwa Aprili 07, 2021 Mwenyekiti @freemanmbowetz alimuandikia barua Rais @SuluhuSamia, pamoja na mambo mengine alimweleza haja ya kufungua ukurasa mpya wa maridhiano na haki katika Taifa letu kupitia mazungumzo, pia akawasilisha ombi la CHADEMA kukutana naye Rais

CHADEMA na wananchi wengi tunaamini kuwa katiba mpya ni nyenzo ya kilipelekea Taifa letu mbele na kufungua ukurasa mpya wa kimfumo na kitaasisi katika nchi yetu, katika mkutano wetu Ikulu Dodoma tulitoa mapendekezo yetu ya jinsi yakukwamua mchakato wa katiba mpya

Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki

Kwa miaka sita ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepandikiza migogoro kwenye vyama takribani vitano, natoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumchukulia hatua msajili wa vyama vya siasa

Mambo mengine tuliyojadili ni kutaka kufutwa kwa kesi za kisiasa na kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa, uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake ikiwemo mikutano ya siasa, kufuta sheria kandamizi nchini kwetu, kufuatilia watu walioshughulikiwa kupotea au kuuawa

Jambo lingine tuliloongea ni juu ya hakikisho la usalama kwa viongozi wetu ambao kwa sasa ni wakimbizi katika nchi nyingine, kuondolewa bungeni kwa waliokuwa wanachama wetu 19

Mwanzo huu wa mazungumzo, utafuatiwa na hatua nyingine za mazungumzo, ombi langu kwa wana-CHADEMA na Watanzania kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu katika hatua hizi zilizoanza, kwa sababu mchakato wa mazungumzo, kujenga maridhiano na mwafaka sio tukio la siku moja

Hatma ya nchi hii, haiko kwa CCM na CHADEMA pekee hususan katika suala muhimu kama katiba, hatua kwa hatua umma utashirikishwa lengo likiwa ni kufika mwaka 2025 tukiwa na katiba mpya

Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO.

#MkutanonaWaandishiwaHabarileo
#MkutanonaWaandishiwaHabarileo
Kweli mwanasiasa ni mtu wa ajabu!!

Yote mliyojadili hasa ni ya miaka 6 iliyopita kuendelea kumchafua hayati ilihali mlilia hata kabla ya awamu ya 5 ila sa hivi mmeona hawezi kujitetea basi ni kama jalala mnatupa tu takataka, wafungwa wa kisiasa waachiwe huru. Mmeona wao ndo wanastahili kuwa huru hata kama walivunja sheria za nchi. Ko hali ya siasa ilikuwa njema before miaka 6 iliyopita. Kwa hiyo mnataka serikali iwalinde walioko uhamishoni na akitokea kibaka kawakaba muanze ugomvi kwa serikali.
 
Mbowe na Mnyika wapo Ikulu, Ndugai na genge lake wapo Kongwa
Wengine mishahara inaflow ila mwingine anavizia kahawa ikulu. Mwanaume wa kweli hatetereki acha litulie kongwa wa maridhiano ahudhurie ikulu, hivi documents za chadema taifa mnatunzia wapi maana naskia hamna ofisi za chama😁.
 
Mkataba wa kwanza aliosaini Mbowe mara ya kwanza Ikulu akiwa peke yake na Rais ni kuheshimiana

hizo lugha za kuita ma ccm wamebaki nazo Wakimbizi waliopo Ubelgiji na Canada

wa Tanzania wote ni ndugu na ndio sababu neno 'Wenzetu' alilotumia Ndugu John Mnyika ni neno Mujarrab kabisa
... "wenzetu" wa CCM? Hilo neno halijakaa sawasawa.
 
Kama nilivyosema ni mapema mno kutumia hiyo lugha given the experience with matendo ya CCM. Wanakuchekea lakini mioyoni wamejaa roho mbaya ya uuaji; uzoefu siku zote umeonesha hivyo.
 
Hongera Chadema, hongera Mnyika John John. Agenda zenu zimeshiba. Hata msipofanikisha zote, huo ni mwanzo mzuri.Muhimu mmedhihirisha kwamba nyie ni chama kikuu cha upinzani Tanzania na mnajitambua. Mmeweka mitego vizuri politically. Hiyo ndio siasa hai. Tanzania kwanza. Kila wakati. Hongera sana Rais kwa kusoma vyema alama za nyakati. Huo ndio uongozi sahihi. Tanzania kwanza.
 
Mkutano ule wa Mei 20,2022 ,ni mwanzo wa mazungumzo ya timu mbili. Upande wetu CHADEMA tuliwasilisha ajenda mbili ya kwanza ni kurejeshwa kwa mchakato wa katiba ya nchi yetu na ya pili ni kujadili madhara ya miaka sita iliyogubikwa na ukiukwaji wa haki

Itakumbukwa Aprili 07, 2021 Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Suluhu Samia, pamoja na mambo mengine alimweleza haja ya kufungua ukurasa mpya wa maridhiano na haki katika Taifa letu kupitia mazungumzo, pia akawasilisha ombi la CHADEMA kukutana naye Rais

CHADEMA na wananchi wengi tunaamini kuwa katiba mpya ni nyenzo ya kilipelekea Taifa letu mbele na kufungua ukurasa mpya wa kimfumo na kitaasisi katika nchi yetu, katika mkutano wetu Ikulu Dodoma tulitoa mapendekezo yetu ya jinsi yakukwamua mchakato wa katiba mpya

Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki

Kwa miaka sita ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepandikiza migogoro kwenye vyama takribani vitano, natoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumchukulia hatua msajili wa vyama vya siasa

Mambo mengine tuliyojadili ni kutaka kufutwa kwa kesi za kisiasa na kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa, uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake ikiwemo mikutano ya siasa, kufuta sheria kandamizi nchini kwetu, kufuatilia watu walioshughulikiwa kupotea au kuuawa

Jambo lingine tuliloongea ni juu ya hakikisho la usalama kwa viongozi wetu ambao kwa sasa ni wakimbizi katika nchi nyingine, kuondolewa bungeni kwa waliokuwa wanachama wetu 19

Mwanzo huu wa mazungumzo, utafuatiwa na hatua nyingine za mazungumzo, ombi langu kwa wana-CHADEMA na Watanzania kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu katika hatua hizi zilizoanza, kwa sababu mchakato wa mazungumzo, kujenga maridhiano na mwafaka sio tukio la siku moja

Hatma ya nchi hii, haiko kwa CCM na CHADEMA pekee hususan katika suala muhimu kama katiba, hatua kwa hatua umma utashirikishwa lengo likiwa ni kufika mwaka 2025 tukiwa na katiba mpya

Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO
Sasa mnazungumza na CCM wakati nyie nyote ni vyama vya siasa. Mnampaje tena madai yenu atekeleze ambapo wao ni wapinzani wenu kisiasa? Mnadhani watakupeni upendeleo ili muwe na upper hand?
 
... "wenzetu" wa CCM? Hilo neno halijakaa sawasawa.

Wote ni waTanzania, ni vyama vya siasa, ni wanaotofautiana!! “Wenzetu” haina maana ya kuwa wa aina moja au wanaofanana!!

Lakini kiukweli kabisa CCM na Chadema na hata vyama vingine wana mambo mengi yanayofanana kuliko wanayotofautiana!!
 
Maisha ni Dunia, alisikika siku moja akisema Askari mtoeni huyo Mara moja.Askari wakawa wanalinda heshima ya mbunge.Ndugai nyie ni askari kweli,toeni nje huyo.Meza pwapwapwaaaaaa.
"Mimi siyo wa mchezomchezo" watu huwa wananikadiria.
Ndugai ni kichaa ndiyo maana hospitali ya Mirembe ipo Dodoma
 
nakuonyesha tu hao unaowaabudu walivyo vinyonga hasa mbowe linapokuja suala la hela aisee ni noma ona sasa hivi kishaanza kuwafokea msiitukane serikali
You are too past Late
 
Mkataba wa kwanza aliosaini Mbowe mara ya kwanza Ikulu akiwa peke yake na Rais ni kuheshimiana

hizo lugha za kuita ma ccm wamebaki nazo Wakimbizi waliopo Ubelgiji na Canada

wa Tanzania wote ni ndugu na ndio sababu neno 'Wenzetu' alilotumia Ndugu John Mnyika ni neno Mujarrab kabisa
Mkuu
Hayo ni maandalizi ya serikali mseto!!!
TUSUBIRI
 
Hatma ya nchi hii, haiko kwa CCM na CHADEMA pekee hususan katika suala muhimu kama katiba, hatua kwa hatua umma utashirikishwa lengo likiwa ni kufika mwaka 2025 tukiwa na katiba mpya

Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO
Great Words From Great Men
 
Back
Top Bottom