John Mnyika: Mambo CHADEMA tuliyozungumza na wenzetu wa CCM

John Mnyika: Mambo CHADEMA tuliyozungumza na wenzetu wa CCM

Mkutano ule wa Mei 20,2022 ,ni mwanzo wa mazungumzo ya timu mbili. Upande wetu CHADEMA tuliwasilisha ajenda mbili ya kwanza ni kurejeshwa kwa mchakato wa katiba ya nchi yetu na ya pili ni kujadili madhara ya miaka sita iliyogubikwa na ukiukwaji wa haki

Itakumbukwa Aprili 07, 2021 Mwenyekiti @freemanmbowetz alimuandikia barua Rais @SuluhuSamia, pamoja na mambo mengine alimweleza haja ya kufungua ukurasa mpya wa maridhiano na haki katika Taifa letu kupitia mazungumzo, pia akawasilisha ombi la CHADEMA kukutana naye Rais

CHADEMA na wananchi wengi tunaamini kuwa katiba mpya ni nyenzo ya kilipelekea Taifa letu mbele na kufungua ukurasa mpya wa kimfumo na kitaasisi katika nchi yetu, katika mkutano wetu Ikulu Dodoma tulitoa mapendekezo yetu ya jinsi yakukwamua mchakato wa katiba mpya

Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki

Kwa miaka sita ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepandikiza migogoro kwenye vyama takribani vitano, natoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumchukulia hatua msajili wa vyama vya siasa

Mambo mengine tuliyojadili ni kutaka kufutwa kwa kesi za kisiasa na kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa, uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake ikiwemo mikutano ya siasa, kufuta sheria kandamizi nchini kwetu, kufuatilia watu walioshughulikiwa kupotea au kuuawa

Jambo lingine tuliloongea ni juu ya hakikisho la usalama kwa viongozi wetu ambao kwa sasa ni wakimbizi katika nchi nyingine, kuondolewa bungeni kwa waliokuwa wanachama wetu 19

Mwanzo huu wa mazungumzo, utafuatiwa na hatua nyingine za mazungumzo, ombi langu kwa wana-CHADEMA na Watanzania kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu katika hatua hizi zilizoanza, kwa sababu mchakato wa mazungumzo, kujenga maridhiano na mwafaka sio tukio la siku moja

Hatma ya nchi hii, haiko kwa CCM na CHADEMA pekee hususan katika suala muhimu kama katiba, hatua kwa hatua umma utashirikishwa lengo likiwa ni kufika mwaka 2025 tukiwa na katiba mpya

Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO.

#MkutanonaWaandishiwaHabarileo
#MkutanonaWaandishiwaHabarileo
Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki[emoji1534]
 
chadema sasa ndiyo mwisho wao jpm alikuwa anatumia nguvi kuwatoa kwenye reli mama anatumia ulimi kuwatoa kwenye reli na tayari wameshaanza kuchochora pembeni kwisha habari ya chadema
 
Kwa miaka sita ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepandikiza migogoro kwenye vyama takribani vitano, natoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumchukulia hatua msajili wa vyama vya siasa[emoji1534][emoji1545]
 
Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO.[emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1533]
 
Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki[emoji1534]
hayo hayatekelezeki muangalie mambo mengine huwezi anza uchunguzi wa vitu kama hivyo ccm ikiwemo madarakani never
 
Kuwa mpole kukipambazuka utajua hujui
1653308416266.png


sikuhizi tushawajuwa ni njaa tu zinawasumbua

2878995_images_9.jpeg
 
2012 Wassira alisema Chadema itakufa ndani ya mwaka mmoja, Magufuli akasema 2020 ataifuta Chadema wewe unasema mama ataifuta. Kesheni mkiomba hilo.
Na yule Mwandishi nguli kabaki anaweweseka tu ili kujiliwaza kajibanza kwa covi19.
 
Ukizisoma hizo hoja za maridhiano za chadema its as if baba anamwagiza mwana kwamba ninataka hivi fanya hivi. Hapa baba ni chadema na mwana sijui ndie atakuwa Rais Samia?

Nirudie tena kusema kwamba chadema kinaonekana hakina uwezo kabisa wa kujitathmini , kujirekebisha na kugeuka. Wapo stuck kwenye mazingira ya kisiasa ya 2005-2015 wanafikiri na sisi wananchi tumeziacha akili zetu kule. Hivi kwa akili za hata mbayuwayu unawezaje kusimama na kurusha lawama kwa msajiliwa vyama kuhusu migogoro yenu? Aaaargh!
 
chadema sasa ndiyo mwisho wao jpm alikuwa anatumia nguvi kuwatoa kwenye reli mama anatumia ulimi kuwatoa kwenye reli na tayari wameshaanza kuchochora pembeni kwisha habari ya chadema
Kaungane na Wassira kutabiri.
 
Back
Top Bottom