PreGE2025 John Mnyika: Rais Samia hajasema ukweli kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi kuundwa kwa kuzingatia maoni ya Wadau wote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amaema kupitia ukurasa wake wa X kuwa Rais Samia amedanganya kwenye baraza la Eid kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi

Amesema “Rais Samia hajasema ukweli kwenye Baraza la Eid kwa kudai kuwa tayari Tume Huru ya Uchaguzi imeundwa kwa kuzingatia maoni ya wadau wote na kuwa wadau wote tulikubaliana.”

Ameendelea kuwa “Rais ajikumbushe ukweli kutoka kwenye mazungumzo naye Ikulu Chamwino 2022 mpaka kwenye mapendekezo yetu kwa Kamati ya Bunge ambayo yanaweza kusikilizwa hapa chini. Reforms zinazotakiwa kufanyika zinajulikana, hatua za haraka zinahitajika”

View attachment 3289758

Soma: Pre GE2025 - DSM - Rais Samia: Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa Haki, Falsafa ya 4R kuendelea kutumika
Mungu anasemaje kuhusu urongo jamani?
 
Ukiwa siyo mtu mnafiki, au ukiwa mkweli kabisa kabisa katika nafsi ya moyo wako, utakubaliana na Ukweli mchungu Sana kwamba huyu Mama Kamwe hawezi kupata Kura hata za Asilimia Kumi tu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao endapo kama kutakuwa na Tume ya Uchaguzi iliyo HURU kama ile iliyopo kule nchini Afrika Kusini.

Chini ya Tume ya Uchaguzi iliyo HURU kabisa kiutendaji:-
Kutakuwa na Demokrasia katika Uchaguzi,
Kura Zitapigwa Hadharani kila Mtu akiwa anaona kwa Macho yake yeye mwenyewe, Waandishi wa Habari wanaweza wakarekodi na kurusha mubashara kabisa mchakato wote kabisa wa Uchaguzi pamoja na zoezi zima la Upigaji kura na Uhesabiaji wake,
Wananchi wataweza Kuruhusiwa kuweza kuwepo katika Vituo vya Kupigia Kura ili waweze Kushuhudia kwa macho yao wenyewe jinsi zoezi la upigaji kura linavyoendelea na uhesabiaji wa Kura.

Endapo kama Mazingira ya Kidemokrasia ya namna hii yatakuwepo Kama vile inavyofanyika katika Chaguzi za kisiasa kule Afrika Kusini, basi naamini kwa dhati kabisa kwamba huyu Mama pamoja na Chama chake Kamwe hawataweza kushinda Uchaguzi na wala hawataweza kupata hata Asilimia Kumi tu za Kura kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.
 
Mkuu. Neno fyoko fyoko linaondoa Huru na Haki, inabaki shurti amri na utii na kukimbia na masanduku.
Kila kitu kina kikomo. Uhuru na haki vina kikomo. Vikizidi lazima Vidhibitiwe. Nenda White House bila suti uone kama utaingia! Ahahahahaha!!!
 
Ulichoandika ndiyo madai ya huyo mnyika. Kwamba 4R ni hadaa. Na tume huru ni uongo. Ulipaswa kutuambia hiyo tume iko wapi. Mkiwapiga hamjajibu tume wanayaoidai. Kipigo ndiyo tume.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amaema kupitia ukurasa wake wa X kuwa Rais Samia amedanganya kwenye baraza la Eid kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi

Amesema “Rais Samia hajasema ukweli kwenye Baraza la Eid kwa kudai kuwa tayari Tume Huru ya Uchaguzi imeundwa kwa kuzingatia maoni ya wadau wote na kuwa wadau wote tulikubaliana.”

Ameendelea kuwa “Rais ajikumbushe ukweli kutoka kwenye mazungumzo naye Ikulu Chamwino 2022 mpaka kwenye mapendekezo yetu kwa Kamati ya Bunge ambayo yanaweza kusikilizwa hapa chini. Reforms zinazotakiwa kufanyika zinajulikana, hatua za haraka zinahitajika”

View attachment 3289758

Soma: Pre GE2025 - DSM - Rais Samia: Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa Haki, Falsafa ya 4R kuendelea kutumika
sasa kama wewe ulisusia kikosi kazi utaonaje mabadiliko yakitokea? :pedroP:

enjoy faida za kususia sasa wakati waengine tunasonga mbele:pedroP:
 
Ulichoandika ndiyo madai ya huyo mnyika. Kwamba 4R ni hadaa. Na tume huru ni uongo. Ulipaswa kutuambia hiyo tume iko wapi. Mkiwapiga hamjajibu tume wanayaoidai. Kipigo ndiyo tume.
Sasa hivi inaitwa INEC, yaani Independent National Electoral Commission (INEC). Na hii imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mengine kasome kwenye website ya INEC.
 
Huo utapeli apeleke kizimkazi sio hapa.
Yeye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Kizimkazi ni kwao kama ambavyo Mtanzania yeyoyyule ana kwao. Lissu hajafukuzwa Mbeya, Iringa, Katavi Wala Rukwa alipopeleka ujinga wake wa No Reform, No Election. Walimvumilia kwasababu ni Mtanzania wa Ikungi, Singida!
 
..4R mbona hataki Reforms?

..bora aseme uchaguzi utafanyika kwa 3R.
Reforms ziliishafanyika kipindi kile mnasusa kukutana na Serikali vyama vyengine havikususa. Sasa hayo ndio madhara ya katoto kajinga kususa kula kakifiri katabembelezwa!
 
Sasa hivi inaitwa INEC, yaani Independent National Electoral Commission (INEC). Na hii imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mengine kasome kwenye website ya INEC.
Yule kio ngozi wake wa kubadilisha matokeo wa chaguzi za nyuma alioko NEC sasa yupo pia INEC. Wacha bwana! Ndio mnatuaminisha mabadiliko, mmetuchukulia waTz wote ni kama chekechea sio
 
Reforms ziliishafanyika kipindi kile mnasusa kukutana na Serikali vyama vyengine havikususa. Sasa hayo ndio madhara ya katoto kajinga kususa kula kakifiri katabembelezwa!

..hata ACT waliowaamini na kushirikiana na CCM mpaka mwisho wanalalamika kuwa reforms hazitoshi.

..Mama amekosea sana kuharibu uchaguzi wa serikali za mitaa.

..kungekuwa hakuna mauzauza ktk uchaguzi wa serikali za mitaa, CDM, na ACT, wasingekuwa wanalalamika.
 
Yule kio ngozi wake wa kubadilisha matokeo wa chaguzi za nyuma alioko NEC sasa yupo pia INEC. Wacha bwana! Ndio mnatuaminisha mabadiliko, mmetuchukulia waTz wote ni kama chekechea sio
Kama haukubaliana na hilo, ikiangia barabarani ukiwashe kama wewe ni mwanaume. Kama huwezi, basi kubali tu. Waingereza Wana msemo, "if you cannot fight them, join them". Karibu CCM!!
 
Back
Top Bottom