John Mnyika, Sio rahisi CHADEMA kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani na kinachochochea maendeleo bila kuzingatia haya

CCM haiwezi kuwa Bora bila kuwa na upinzani imara
 
CCM watakuwa Bora iwapo upinzani utakuwa makini Basi. Upinzani ukilegalega CCM itakuwa goigoi
 
Hizo ni bla bla tu,baadhi ya yanayotendeka sasa ni kutokana na msukumo au nguvu kubwa ya upinzani imara ukiongozwa na CDM.Elimu bure,mafisadi n.k zilikuwa moja ya agenda ya CDM katika kampeni za 2010.Chama tawala imezichukuwa agenda hizo na kuzitekeleza(ambalo ni jambo jema) kwa kuwa waliona zilieleweka kwa wananchi.Japo inawezekana mkakati wa utekelezaji wa agenda hizo hauwezi ukawa sawa na walio ziasisi.
 
Iyo ilikuwa Chadema ya 2010, tunataka ya Sasa ifanye Kazi kwa Kasi ZAIDI sio kujipigania wao tu
 
Kwa upimbi wako lazima uwaze hivyo...ccm imeshaungana na Nccr cuf na tlp...tukutane October...sisi ni watu wa kusonga mbele tu
 
mrejesho oktoba.
 
CCM imepambana na ufisadi upi? Hebu thibitisha? CCM sasa kuna ufisadi mkubwa haujawahi kutokea. Najua ufisadi unaofanyika sasa pengine utakuja kuwa wazi zaidi baadaye. Kumekuwa na nguvu kubwa ya kudhibiti media ili mambo haya yasiwe hadharani, lakini hayatazuiwa muda wote milele. Takukuru kila siku inawakamata watia nia ndani ya CCM wakipeana rushwa, huu nao ni ushahidi mwingine kwamba ndani ya CCM rushwa ni ibada! Kuitenga CCM na ufisadi nao ni ufisadi. Kinachotokea ni makelele ya majukwaani yanayobadili fikra za watu wanaofikiri polepole!

Mnapenda sana kumtumia Dk. Slaa mnapoizungumzia Chadema, na kuonyesha kuwa baada ya kuondoka imeyumba na kwamba angekuwepo yeye ndipo ingezidi kuimarika. Hii ni hoja ya kichovu, na inaweza kutolewa na mtu anayefikiri polepole. Mazingira ambayo Chadema imepitishwa na serikali hii ya wamu ya tano, ni kukosa uzalendo kutowapongeza viongozi wake akiwemo Mbowe. Niliwapowaona wakiimba 'tumeuona mkono wa Bwana!' baada ya Bunge kuahirishwa hivi karibuni, mimi pia niliiitikia kile kibwagizo. Ni kweli Chadema wameuona mkono wa Bwana. Hivi kwa mfano, Dk. Slaa na mkewe wangeweza kuvumilia madhila ambayo Mbowe na familia yake wamekumbana nayo katika utawala huu wa mkono wa chuma? Kanitafutie jibu!

Tuhuma zako dhidi ya Mbowe kulamba bilioni nane, sijui msingi wake ni nini? Najua ni tuhuma zilizotolewa na akina Lijuakali baada ya kufurushwa, lakini angalau mimi na wewe tunafahamu kwamba Chadema ni taasisi ambayo ipo chini ya uangalizi wa vyombo vya serikali, akiwemo CAG. Je, tumwamini Lijuakali tuanze kujadili tuhuma anazozitoa? BTW, baada ya Bunge kumalizika Lijuakali anaendelea kulia?

Mwisho unadai Chadema inapukutika? Na bila shaka unatumia sample za akina Lijuakali, Silinde, Wilfred Rwakatare, Selasini,....endelea kuhesabu. Kwenye chama wenye nguvu sio hao akina Lijuakali ambao kila mtu ahata mjinga, alijua nini wanatafuta. Mwisho wa siku wajinga kati ya viongozi wa Chadema na watu akina ya Lijuakali wataonekana. lakini kikubwa ni kwamba, Chadema kina watu wengi kuliko unavyofikira, kampeni zikianza naomba tukutane hapa!
 

Post yako ina pointi za msingi sana, ila ujumbe halisi wa post yako ni hapo paragraph ya mwisho.
 
Haijawahi kuwa "wewe ndiye mwananchi na wengine sio wananchi"! Mwenye mbwa angehangaika na mgonjwa?
 
Naomba mawasiliano ya Mnyika maana sijui

Sina mawasiliano yake maana mimi sio mwanachama wa cdm, wala rafiki wa karibu wa Myika, bali shabiki wa kutupwa wa cdm. Ila kuna verified user ya Tumaini Makene na ya Chadema. Jaribu kuingia Inbox uwaombe watakupatia iwapo wataridhia.
 
Unapotoa hoja ukajibiwa kwa bunduki na kutekwa bado unahitaji kutumia hoja ?

Wewe unaweza kujenga hoja mbele ya bunduki na maji washa washa ya polisi?

Vijana wa ccm sijui huwa mnaongea mkiwa mmesahau vichwani vyenu chooni ?
 
Chadema kilinyimwa platform ya kujenga hizo hoja anazozitaka Alitaka wakajengee hoja zao vyumbani ?

Wewe Paschal ni mwandishi mkongwe unaona mazingira ya kisiasa ya serikali ya awamu ya tano yariruhusu hizo platform za wapinzani kusikika?

Kule Bungeni Speaker aliwashughulikia wabunge wa upinzani ikiwemo kuzuia hotuba zao zisisomwe au akazifanyie editing ziendane na anachokitaka hoja zao zingeweza kusikika vipi wakati walifungwa mdomo everywhere ?

Nje ya Bunge walishughulikiwa na polisi wengine kwa bunduki za watu wasiojulikana hizo hoja zao wangezitoa vipi at gun points ?

Mikutano ya siasa ya hadhara kwa wananchi walizuiwa na polisi wa ccm na hata vyombo vya habari vilipewa kibano kuwapa platform hizo hoja zao ulitaka waziwasilishe wapi na kwa njia gani ?

Vyombo vya habari vyote vilivyowapa platforms ama vimefungiwa au kufutiwa leseni hoja zao zingesikika vipi bila kuwa platform kama hii.?

Uchaguzi huu unakaribia kuanza vyama vya upinzani hasa CHADEMA wanafanyiwa hujuma za wazi ikiwemo bendera zao kushushwa na msajili wa vyama vya siasa yuko kimya, tume ya uchaguzi iko kimya, jeshi la polisi liko kimya mnataka wapinzani waanzishe vita ili muelewe kuwa mazingira ya kisiasa siyo rafiki kwa vyama vya upinzani ?

Hata kama ni makada wa ccm hamuoni hata aibu kupigana na mtu ambaye amefungwa kamba ??


Jaribuni kuwa objective walau hata kwa siku moja tu .
 
CCM ndiyo waliodidimiza nchi kwenye lindi la umaskini unataka CHADEMA wafuate ushauri wa watu waliofilisi nchi kwa ufisadi ?

CCM ndiyo baba wa siasa chafu na za kipumbavu unataka chadema nao wafanye siasa hizi za kipumbavu kama za ccm?
 
Pascal aibu iliishaga cku nyingi, ndo maana cku hz yuko kwenye list ya walamba viatu
 
Chama kitie sera zake wakati hata mikutano hakiruhusiwi kufanya?

Unamfunga kamba mtu mikono, unamuwekea sinia mbele yake, halafu unamwambia ale anavyotaka?
 
Hivi unajua ushindi wa Mandela ulichangiwa kwa kiwango kikubwa sana na civil disobedience na uungwaji mkono wa frontline states ?

Tatizo lenu mnapenda kutumia historia kujenga hoja potofu bila kujua hadhira unayoilenga inajua kuliko wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…