John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

inshu ya huko SUDAN nilikuwa najiuliza hivi wakati wa utawala wake hapakuwa na watu wanaomkubali na kutamani atawale milele au kusema anachapa kazi vzuri. !??

kama walikuwepo imekuwaje kaangushwa na sasa aibu iko juu yake!!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA YA AWALI KUHUSU TUKIO LA MDUDE NYAGALI (MDUDE CHADEMA)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jioni ya leo (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.

Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.

Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu. Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.

Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Mfalme ameshindwa kuvumilia maneno ya mwananchi wake.
Huwa anakometi maneno ambayo jiwe hayapendi.
 
inshu ya huko SUDAN nilikuwa najiuliza hivi wakati wa utawala wake hapakuwa na watu wanaomkubali na kutamani atawale milele au kusema anachapa kazi vzuri. !??

kama walikuwepo imekuwaje kaangushwa na sasa aibu iko juu yake!!

Siku Ndumba ikiexpire miti yote uteleza hata jeshi haliwezi kukuokoa
 
Magari mawili aina ya Nissan Patrol na Toyota Landcruzer (yasiyo na namba za usajili) yakiwa na watu kadhaa wenye silaha za moto wamevamia eneo la kazi la Ndugu Mpaluka Mdude Nyagali, maarufu kama Mdude Chadema dakika chache zilizopita. Mdude ni fundi wa Computer na masuala ya IT na ofisi yake ipo maeneo ya Vwawa, huko Mbozi.

Watu hao wamefyatua risasi moja hewani na kuwaamuru watu wote waliokuwemo kulala chini kisha wakamchukua Mdude na kuondoka nae kwa mwendo wa kasi. Baada ya kuondoka mashuhuda wa tukio hilo wameenda kutoa taarifa kituo cha polisi Vwawa lakini bado hawajachukua hatua yoyote.

Nimezungumza na baadhi ya mashuhuda waliokua eneo la tukio, Mbunge wa Viti maalumu Songwe mama Sophia Mwakagenda, na Mgombea ubunge wa Vwawa Ndg.Fanuel Mkisi ambao wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Tunaomba tupaze sauti kwa nguvu ili Mdude apatikane akiwa salama.!
Mkuu ungeleta na baadhi ya miandiko yake either kanma alikuwa anakosoa serikali yetu ama viongozi ama kutetea wananchi ama anachochea kitu fulani ama Jambo fulani.
 
Chadema badala ya kujenga viwanda wameatamia ngada tu ,unategemea nini?

Huyo Mdude walimchelewesha ana matusi sana .

Kwenye nchi hii anayeogopwa na Mdude ni Mbowe tu.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA YA AWALI KUHUSU TUKIO LA MDUDE NYAGALI (MDUDE CHADEMA)

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jioni ya leo (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.

Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.

Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu. Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.

Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Ndugu wanachadema nawashangaeni sana kwakutochukua tahadhar wakati mnajua mnapambana na jiwe ambalo ni humanless,nashaur tembeeni na kila aina ya silaa ili siku tusikie wasiojulikana wamecharazwa mapanga kwa kuvamia watu hamuwez kila siku kulaania,shetani anashughurikiwa kwa moto
Pole kwa mhusika lakin jitahid kuchukua tahadhari na huu utawala wa kimafia
 
Back
Top Bottom