Abuu Kauthar
JF-Expert Member
- Jul 10, 2011
- 4,296
- 6,492
Kila siku wanapotea na hawarudi na wala hakuna mtu anayejali. Hatari sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yupo sahihiHivi we umekaa darasani kweli?
CHADEMA HAMUWAJUI WALIOMTEKA MDUDE KWELI? HAMUWAJUI TISS WANAOTEKA WOTE WANAOMKOSOA JPM?!!Mbunge wa Kibamba kupitia CHADEMA, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter amesema kuwa Chadema Mdude amechukuliwa na Watu wenye silaha
Aidha, yeye mwenyewe amesema CHADEMA inafuatiloa suala hilo na taarifa zaidi itatolewa muda si mrefu
______
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA ZA AWALI KUHUSU TUKIO LA MDUDE NYAGALI (MDUDE CHADEMA)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.
Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jioni ya leo (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.
Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.
Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu. Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.
Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.
Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.
Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
View attachment 1088177
Asiyefunzwa na wazazi hufunzwa na dunia.
Nissan ya Mbowe baada ya kumshughulikia Lisu kwa jina bandia imerudi kivingine tena?
Mwenzao kafa juzi Muhimbili pale.....we ngoja tuWasiojulikana kile kitengo maarufu cha Dikteta pale Ikulu ili kuwanyamazisha wanaomkosoa kwa kuwateka, kuwatesa na hata kuwaua kimeibuka tena kwa kasi ya kutisha.
Mojawapo ilitumika kumuua Akwilina!Amejiteka Kwa kujipiga risasi. Hivi Chadema Wana silaha za moto?
Unalaanije mtu alienda kula Bata Dubai!Mmh mbona serikali haitoi kauli ya kulaani ??
Mmeshindwa kujibu hoja mrudisheni Kijana wa watu.Nyie ma tiziccmHuyu kijana ana matusi sana..nadhan hakupata malezi mazuri
wameanza tena..........
Tutabakije salama wakati mtu mwenyewe hataki kuachia Uenyekiti!"Ukishaonja nyama ya mtu huachi," aliwahi kusema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP). Kwa sasa idadi ya walioonja nyama ya Watanzania wenzao yaonekana inaongezeka kwa kasi ya kutisha awamu hii..je kwa kasi hii tutabaki salama?
Kudadadek! kwanza walichelewa sana kumkamata, ana matusi sana huyo mdude wenu
Nissan ya Mbowe baada ya kumshughulikia Lisu kwa jina bandia imerudi kivingine tena?
Vita ya uenyekiti wa chama itamaliza wengi.
Hii ya awamu ya tano kiboko, Boss anaamuru MTU anayemfanyia fujo kwenye mkutano wake awekwe ndani, huku vijana wanaojulikana wanamteka kada kupelekwa ndani. Ila CHADEMA waki-survive awamu hii hakuna system itakayo wapoteza tena mpaka mwisho wa dahari.
Sawa mkuu, ila naomba utafakari methali ya kiswahili isemayo: "tumbili akisha miti, huja mwilini!" na "alieko juu, mngoje chini". Mambo hugeuka mkuu, kuna leo na kesho pia, mimi na wewe ya kesho hatuyajui!Atakuwa kadhulumu watu huyo, acha wamshikishe adabu
Vipi kuhusu musiba yye atafunzwa na naniAcha akafunzwe adabu akirudi atakuwa na nidhamu na wakubwa zake