John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

John Mnyika: Watu wenye silaha wamemchukua Mwanachama wa CHADEMA, Mdude Nyagali (Mdude CHADEMA)

W
Mbunge wa Kibamba kupitia CHADEMA, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Twitter amesema kuwa Chadema Mdude amechukuliwa na Watu wenye silaha

Aidha, yeye mwenyewe amesema CHADEMA inafuatiloa suala hilo na taarifa zaidi itatolewa muda si mrefu

======

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA ZA AWALI KUHUSU TUKIO LA MDUDE NYAGALI (MDUDE CHADEMA)


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika hali ya dharura, kinafuatilia kwa karibu, taarifa za Mdude Nyagali (Mdude Chadema) kuvamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawajatambulika, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, majira ya jioni ya leo (saa 12 kuelekea saa 1) yalifika magari mawili katika eneo la ofisini kwa Mdude, Vwawa mjini, kisha wakatelemka takriban watu wanne, ambao walimkamata kijana mmoja aliyekuwa nje ya ofisi hiyo wakampeleka kwenye mojawapo ya magari waliyokuja nayo huku wengine wakiingia ndani ya ofisi, alikokuwa Mdude.

Imedaiwa kuwa baada ya muda mfupi kulisikika purukushani, watu hao wakijaribu kumkamata Mdude huku wakimpiga na yeye akipiga kelele za kupinga kitendo hicho na kuomba msaada.

Taarifa za awali ambazo Chama kimezipata kutoka kwa mashuhuda hao zimedai kuwa baada ya kusikika kwa purukushani na kelele hizo, baadhi ya wananchi walijitokeza kutaka kujua kinachoendelea na kutoa msaada, ghafla watu hao waliokuwa wakimpiga Mdude wakatoa silaha aina ya bastola na kuwatishia wananchi hao, kitendo kilichowaogofya wananchi na kukimbia kwa hofu. Imedaiwa kuwa watu hao walimuingiza Mdude kwenye 'buti' ya mojawapo ya gari hizo, wakamuachia yule kijana mwingine kisha wakaondoka na Mdude kuelekea kusikojulikana.

Tayari CHADEMA kupitia kwa Viongozi wa Chama katika eneo husika na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Pascal Haonga, kimevitaarifu vyombo vya dola mkoani Mbeya, kwanza kutoa taarifa ya tukio hilo lenye mazingira ya utekaji pia kutaka kujua kama kuna askari waliopewa kazi ya kwenda kumkamata Mdude.

Hadi sasa haijulikani Mdude yuko wapi! Tupaze sauti zetu sote kulaani tukio hili na kutaka Mdude arudishwe au aachiliwe akiwa salama.

Katika hatua ya sasa, CHADEMA kwa nguvu zote kinalaani vikali tukio hilo. Tunavitaka vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi lenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, kufuatilia taarifa za tukio hilo kama zilivyoripotiwa kwa polisi katika eneo husika na kuhakikisha Mdude anapatikana na wahalifu waliotenda tukio hilo wanajulikana, kukamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.

Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

View attachment 1088177


Zaidi, soma;



watanzania bwana,kwa hiyo mwenzao amepakiwa kwenye buti wao huku wanakimbia wakiogopa risasi? Kwamba wamemuona Mdude hana miguu ya kukimbia- kwa style hii tutaendelea kufa na kupotea Sana tu
 
Watawakana kumteka kisha baada ya mwezi waseme alikua anahojiwa.

Wiki nzima wakili wa arusha alikua anatafutwa bila mafanikio, baada ya jamii kuanza kupiga kelele ndo wanajitokeza kusema hakutekwa bali ana hojiwa .

Kama nia yao ni nzuri kwanini wawavizie katka ukamataji. ? . Kwanini iwe siri. ? kwanini watumie magari yasiyo na namba za utambulisho? .


Kwanini serikali isihusishwe na utekaji. ?
Hivi wewe polisi wakimkamata mtu ni lazima watoe taarifa kwa umma kwamba tunaenda kumkamata mtu fulani? Hivi akili zenu huwa zinafikiria nini? Isitoshe huko arusha waliokamatwa walikua tisa including huyo wakili, lakini cha kushangaza anaepigiwa kelele ni huyo wakili. Kwasbbu tu anajihusisha na itikadi za chama fulani
 
Halafu bado wameenda kuripoti polisi. [emoji16][emoji16][emoji16] daah
 
Wana Arusha wamepiga kelele ndo wakili ikajulikna ameshikilia,watu wasipopiga kelele atapotea Jumla.
Kabisa,nilijua ipo siku atakamatwa au kutekwa maana serikali ya sasa haipendi watu wa aina yake
 
W
watanzania bwana,kwa hiyo mwenzao amepakiwa kwenye buti wao huku wanakimbia wakiogopa risasi? Kwamba wamemuona Mdude hana miguu ya kukimbia- kwa style hii tutaendelea kufa na kupotea Sana tu

Ingekuwa Tarime wasiojulikana wasingetoka wale wa zakaria wawashukuru sana polisi walishawekwa MTU kati ili watahiriwe nyepesi nyepesi mmoja alishavuta.
 
Hivi wewe polisi wakimkamata mtu ni lazima watoe taarifa kwa umma kwamba tunaenda kumkamata mtu fulani? Hivi akili zenu huwa zinafikiria nini? Isitoshe huko arusha waliokamatwa walikua tisa including huyo wakili, lakini cha kushangaza anaepigiwa kelele ni huyo wakili. Kwasbbu tu anajihusisha na itikadi za chama fulani

Soma Sheria za ukamataji we buku saba polisi wakikutaka awakukwapui,wakwapuaji ni wazee wa Nissan kila MTU anajua.
 
Soma Sheria za ukamataji we buku saba polisi wakikutaka awakukwapui,wakwapuaji ni wazee wa Nissan kila MTU anajua.
Wewe usidhani kila ni zwazwa kama wwe. Nimeuliza taarifa inatolewa kwa umma au kwa anaekamatwa?
 
Tarehe 24 mwezi March kijana mmoja aitwaye Abusadik Banzi alimtumia ujumbe ndugu Mdude kupitia ukurasa wa Facebook akimtishia maisha.

Baada ya vitisho hivyo Mdude aliripoti kituo cha Polisi Vwawa lakini polisi walisema hawamfahamu mtu huyo, na hawajui kama majina analotumia ni majina yake halisi, hivyo hawawezi kufungua jalada la uchunguzi.

Ikabidi Mdude na marafiki zake wachache kuingia kazini ili kuisaidia polisi. Baada ya wiki kadhaa tukapata 'clues' ambazo zingesaidia polisi kumkamata mtu huyo.

Ilibainika kwamba Abusadik Banzi ni majina halisi ya mtu huyo, na anaishi mjini Arusha, maeneo ya Kijenge juu (karibu na Matindigani). Kabila ni Mdigo wa mkoani Tanga, wilaya ya Handeni. Amezaliwa mwaka 1985.

Mwaka 2007 alijiunga na mafunzo ya awali ya JKT, na baadae kupelekwa katika kambi ya uzalishaji Chita mkoani Morogoro kabla ya kufurushwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Alirudi Arusha na kuajiriwa katika kampuni moja ya ulinzi. Mwaka 2012 aliondoka Arusha na kwenda mkoani Geita ambapo aliajiriwa kama mlinzi kwenye mgodi wa Geita Gold Minning kabla ya kuachishwa kazi mwaka 2016 na kurudi tena Arusha.

Kwa kipindi chote hicho Banzi ni mwanachama wa CCM na member wa kikosi cha ulinzi cha CCM kiitwacho Green Guard mwenye post code nambari 23106. Hata hivyo amekuwa akijitambulisha kuwa ni Afisa wa idara ya usalama wa taifa (TISS) maeneo mbalimbali ya jijini Arusha.

Polisi walipewa taarifa zote hizi lakini hawakuchukua hatua zozote, hadi leo Mdude alipotekwa na watu wasiojulikana. Inasikitisha sana. #BringBackMdudeAlive
 

Attachments

  • Screenshot_2019-05-04-22-20-29.png
    Screenshot_2019-05-04-22-20-29.png
    807.8 KB · Views: 21
Nawaambia hivi, imeandikwa haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wowote! Kuna namna utawala huu unaangamiza na kushusha taifa hili kwa matendo yao yasiyo haki!
 
Wewe usidhani kila ni zwazwa kama wwe. Nimeuliza taarifa inatolewa kwa umma au kwa anaekamatwa?

Inategemea kama ni MTU anayefahamika akizuiliwa na polisi umma ujulishwa,MTU wa kawaida uongozi wa mtaa na majirani ujua. Acheni kukwapua watu mtasaga meno mbele ni kujibu historia
 
Back
Top Bottom