Pre GE2025 John Mrema: Wanataka kunifukuza uanachama. Wameshinda uchaguzi sasa hawataki wengine tuseme

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nathan ni vzur wakuache uongee maana awali ulikua huongei ulkua kmya maana ulkua na tonge la ugali na nyama mdomon na sio utamaduni wa kiafrika mtu kuongea akiwa na chakula mdomon ,kama sa hiv hakipo nadhan wakuache uongee
 
Tatizo kubwa ni rushwa. Na TL aliahidi na kujitanaibisha mapema kabisa kuwa akichukua uongozi atasafisha chama. Jaribu kufikiria kama yeye alikuwa mkuu wa nidhamu ndani ya chama je mangapi anayajua?
Naam kama ni Rushwa si kuna Sheria, Taratibu na Kamati za Nidhamu n.k., Hivyo kama kweli akionekana ana kosa basi ashughulikiwe kama Chama walivyojipangia kumshughulikia mtu kama huyu akifanya kama hayo...,
 
Huyu ni mmoja wa waliomuumiza MSIGWA ,hastaili kuwepo kwenye chama hadi muda huu.
Ndiyo maana tumesema kuwe na Tume ya mapatanisho - kila upande umeumizwa ; ukiruhusu haya ya kufukuzana CDM haifiki mbali - muda ni mchache sana kuelekea uchaguzi Mkuu. Msiwape nafasi maadui wetu wapumue, inatakiwa pressing inanze kwa umoja wote, yaani ni kukabia juu.
 
Mahali popote ukiingia uongozi mpya kuna wale mafundi wa majungu wanakimbilia kuuweka sawa. Na kwa vile uongozi huu unaendekeza fitna basi wataumia wengi.

Lema alimpigia simu Lissu kumuombia kuwa watu wananyimwa vitambulisho, wameambiwa watavipata kesho yake. Waandishi wa habari wakamkuta Kigaila anaendelea zoezi zima na hamna aliyenyimwa kitambulisho. Wakasingizia kuwa watu wanapewa rushwa vyooni kumbe ni maofisa kutoka kanda walikuwa wanawapa watu posho na nauli zao!

Hawa sio wa kuwaamini.

Amandla...
 
Huyo Msigwa ni Mungu wa Chadema? mbona anatajwa tajwa sana?
Msigwa ni rafiki yao Lissu, Lema na Heche. Heche peke yake ndie aliyelaani vikali juhudi zake za kukichafua chama. Mimi nawashangaa wale ambao wanakomalia wakina Halima wasirudi lakini wanampigia debe Msigwa na Slaa.
Wakina Halima hawajawahi kukisema vibaya CDM au viongozi wake.

Amandla...
 
Lissu angeonyesha ukomavu wa hali ya juu kama angewapa mkono Wenje, Ntobi na Nyerere na kuwahakikishia usalama wa nafasi zao katika chama. Yeye mbona alimuita Mbowe muongo lakini alimpa mkono?

Amandla...
 
Kama ni kweli anachoongea Mrema basi ni makosa, CHADEMA tunatakiwa tuheshimu freedom of Speech kwa vitendo.
Mrema leo ni mtu wa kulalamikia viongozi wa Chadema Tawi?! Mkubwa huoni fishy agenda in his claims?
 
Ngese lingine hili. Hapa mi CCM inaanza kutumia plan B kununua mamluki na kuweka fitna.
 
Anatunga hayo kuchafua chama. Hamna mwenye mpango nae.
 
Ulichagua upande, Africa ukichagua upande wewe ni tatizo labda ujifiche au kuwa mstaarab.

Ulichagua upande na ukawa unavimba, boni yai mwenzio alikuwa mwepesi muda wote tofauti na mwanzo alivyokuwa yeye na Yerico mengele
Sasa yule mweye kiti wa BAWACHA anajisikiaje maana alisha jinasibisha kabisa ila kwa kuwa TUNDU LISSU anajua kutatua matatizo ya ndani ya chama atamaliza hiyo shida
 

Si walisema baada ya uchagizi Mwamba na wafuasi wake watachukua hatua?



Muda wao wa kukaa kwa kutulia dawa iwaingie.

Habari ziwafikie chawa wote.
 
Kawaida tu mtu akiingia madarakani anaangalia nani bora kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…