John Obi Mikel: Familia za Kiafrika zinachangia kuwavuruga Wachezaji waliofanikiwa kifedha

Umesikiliza interview yake yote???
Jinsi familia yake ilivyompangia majukumu na wanavyo mfanya jamaa??
Utajiri wa huyo kijana ni Dola million 45, hii ni zaidi ya bilioni 100. kwetu sisi tuliozaliwa africa, hata ukitoa tu bilioni 10 out of 100 kusaidia ndugu zako, una hasara gani?

Unamkumbuka Chavez, yule wa Mancity, aliondoka kwenda uarabuni au china kama sikosei, kwa sababu tu ya pesa ndefu waliyomwahidi, akaipata, alienda kununua mtaa, akabadilisha nyumba zote zikawa za kisasa akagawia ndugu zake. hizo bilioni zote atakufa nazo?
 
Unahoja mkuu
 
Kuna ndugu yangu alienda Germany akaoa hukohuko akaileta familia yake bongo alipoondoka ndiyo mpaka leo inawezekana sababu ndiyo hiyohiyo: uchawa kwenye mafanikio ya watu mpaka watu wanajitoa kwenye ukoo, hahah!
 
"Mtegemea cha ngugu hufa masikini."

Kwanini upigie hesabu pesa ambazo haujazifanyia kazi? Mtu kuwa tajiri kwenye ukoo haimaanishi ndiyo wote mpeleke shida zenu kwake. Zipo familia nyingi tu unakuta kuna mtu ana uwezo mkubwa kifedha ila kila mtu na maisha yake, kusaidiana ni kwenye shida za kifamilia na siyo kupiga simu kila saa kuanza kusumbua watu na familia zao.
 
Afrika tumelaaniwa walah,sio wanasoka tu mtu yeyote akifanikiwa iwe kwenye kazi au biashara akionekana na unafuu wa maisha tu ndugu hata wale wenye undugu wa mbali wanaanza na wao kutaka haki ya kuwa sehemu ya mafanikio yako,mizinga haiishi nk
Huu ni utamaduni ambao tumeshauzoea. Kuondokana nao itachukuwa muda sana. Kwenye familia mmoja akifanikiwa wengine wote wanataka mgao.
 
Ndio maana Waafrika wakifika Ulaya, Marekani, Canada na nchi nyingine za wazungu wanapata shida sana kuishi,
Wenyewe wanasema hakuna maisha ya ujamaa na community!
Mfano mzuri ni Bill Gates ana utajiri unaokadiriwa kuwa ni $133 billion ila dada yake, Kristianne Gates ana $1 million.

Sasa Africa wanataka hizo $133b kila mwanafamilia apate mgao. Wenzetu wanaishi maisha ya kujitegemea sana kiasi kwamba watoto nao wanarithi mfumo huo wa maisha.
 
emmanuel adebayor aligombana mpka na mama yake mzazi na ndugu zake karibia wote.

ishu yake ilienda viral sana .
wengine ambao nimewahi wasikia
kuna
michael Essien
paul pogba nk
Samatta pia kwenye kipindi cha "Salama Na" alisema vizinga kutoka kwa ndugu ni vingi sana ikabidi amkatishe Salama hiyo mada akihofia itamletea matatizo na ndugu. 😁
 
Mkuu umesikiliza interview yake. Ishu sio msaada ishu ni majukumu.
Kapewa yeye. Ukute dada yako kazaa na wanaume 4 tofauti na wapo na maisha yao. Ila majukumu ya kulea umepewa wewe , why? Jibu hio.
Na ukute unadada 2 hapo au 3.
Unajua majukumu??
 
Ndo maisha ya waafrika mtu una hangaika , unateseka saa nyingine unakutana na kifo uso kwa uso kuyatafuta mafanikio.
La kushangaza ukisha yapata hayo mafanikio ndugu wanarazimisha yawe ya ukoo mzima.

Hapa Africa usipo kuwa mnonko utoboi.
Mbaya zaidi ukiwa umefanikiwa peke yako katika familia ya watoto kadhaa ni balaa. Utakuta wengine wanakuomba fedha eti Baba yetu alikusomesha. Sasa la kujiuliza, kwani ulimkataza Baba yako asiwapeleke shule? Kwa kweli Waafrika tunatakiwa tubadilike.
 
Hata huku tunaweza kuweka mifumo bora itakayotusaidia.

1. Elimu bora.

2. Dhana ya kuwa kila anayesoma lazima aajiriwe ibadilike vichwani mwa watu. Shule zianze kuandaa watu ktk fani zote: mitaala ya elimu iangaliwe upya.

3. Elimu ya fedha.

4. Watoto wafundishwe kujiamini (sna hakika kama hili ni somo). Ila kwa % kubwa Africa vijana wengi hawajiamini. Ndiyo tunaishia kuwa na taifa la watu wa kubahatisha. Mafanikio siyo bahati.

Ila vyote hivyo ni ngumu kutimia kama bado shule zetu za msingi zinaweza kutoa wahitimu wasiojua kusoma na kuandika.
 
100% truly.
 
Afrika tumelaaniwa walah,sio wanasoka tu mtu yeyote akifanikiwa iwe kwenye kazi au biashara akionekana na unafuu wa maisha tu ndugu hata wale wenye undugu wa mbali wanaanza na wao kutaka haki ya kuwa sehemu ya mafanikio yako,mizinga haiishi nk
Hatujalaaniwa, tumejilaani wenyewe. Hata hivyo jamii zinatofautiana sana hata hapa TZ. Kuna jamii ukioa huko umeoa ukoo mzima.
 
Inaonekana na wewe ni ombaomba kama anaowasema obi.
Chanzo cha umaskini wa Afrika ni utamaduni unaoutetea huwezi mtegemea mwenzako afanye kazi alafu wewe upewe tu ukimaliza unaomba tena huo ni utahira umaskini hauwezi kuisha
Unapumuliwa kisogoni? Wapi nimesema mtu awe omba omba. Afrika kutoboa ni kibahati sio kimfumo kwaiyo ukifanikiwa jitahidi kuwainua wengine nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…