John Wegesa Heche turufu pekee iliyosalia CHADEMA kuelekea kufutika kwake baada ya Chaguzi kuu za 2024 & 2025

Binafsi heche namkubali sana. Huwa anakuwa na hoja zenye mashiko sana
 
Bila tume huru ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
huyu ni jamaa mmoja ana hasira sana,na hana uvumilivu wa kusikiliza hoja za wenzie anataka hoja zake tu ndio zisikilizwe,ni udhaifu wake mkubwa
Kama ni kwel, hii sio sifa nzuri japo kuna muda ina faida zake..ila tatizo ni kwamba unaongiza watu wazima wenye akil hivyo utajikuta kama wanakupinga muda wote kumbe tu ni wewe usiyetaka kusukiliza mawazo yao
 
John Heche bado anatakiwa kuendelea kukua na kujiimarisha juu ya misingi ya chama na Taifa
 
John Heche bado anatakiwa kuendelea kukua na kujiimarisha juu ya misingi ya chama na Taifa
Sasa akue aende wapi?

Uongozi ni kibali tu sio kukua,

Mbona hao wakubwa ndio wanakiua chama Sasa?
 
Lakini mkuu, suala la chadema kufa mbona limetabiriwa siku nyingi tena enzi JPM lkn naona bado wanatamba na kuimarika zaidi
 
Lucas Mwashambwa ndo turufu yenu kuelekea 2025. Atawasaidia kuwanoa vijana
Aende akawanoe akina mama wenzie.
Lakini mkuu, suala la chadema kufa mbona limetabiriwa siku nyingi tena enzi JPM lkn naona bado wanatamba na kuimarika zaidi
JPM kaiacha inatamba,Job Ndugai kaihujumu akiwa Spika leo siyo Spika lakini CHADEMA bado inatamba.
 
Safisha nyumba yako ndugu. Ya Chadema yaache hayakuhusu. Kila siku wimbo ni huo huo eti Chadema inakufa. Uchaguzi ukifika , ccm mnaugeuza uchafuzi. Kipimo sahihi cha kujua Chadema iko hai au imekufa ni uchaguzi huru na wa haki. Mwingine naye aliapa kuiuwa Chadema matokeo yake kafa yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…