Uwezo wa Mh Jokate kiuongozi ni mkubwa sana ambapo naamini anakwenda kuipa nguvu kubwa sana jumuiya ya akina mama. Uongozi siyo umri bali ni uwezo wa kuongoza unaochagizwa na Elimu au maarifa,hekima,busara,maono, Utulivu, uvumilivu, kifua na nidhamu katika kuuchunga na kuulinda ulimi wako. Jiulize mwalimu Nyerere alishika uongozi wa Tanu na uwaziri mkuu wa nchi yetu akiwa na miaka mingapi? Emmanueli macron aliingia na kushika uwaziri pamoja na Urais baadaye akiwa na miaka mingapi? Salimu hamed salimu alipewa ubalozi akiwa na miaka mingapi? Unafahamu hadhi ya ubalozi? Barack Obama au John F Kennedy was marekani walishika urais wakiwa na miaka mingapi kwa Taifa kubwa kama lile? Mzee Warioba alishika na kuanza uongozi mkubwa akiwa na umri wa uzee?
Jokate ni nyota Ing'aayo Gizani na kuwamulikia watu na kuwapatia matumaini. Mh Jokate atafika mbali sana kiuongozi katika Taifa letu.Ni kijana msomi na mchapa kazi sana.Ni kijana mbunifu na mwenye maono ya mbali.