Nilimsikiliza Masoud Masoud ile siku... hakumbeza yeyote lakini alitamka wazi kwamba yeye anamkubali zaidi Ally Kiba... na hivi ndivyo ilivyo duniani kote... hakuna mwanamuziki hata mmoja duniani ambae alikubalika na kila mtu. Hilo moja, lakini lingine ukubwa wa mtu kimuziki unapimwa na mafanikio yake kwenye muziki... leo hii watu wanaposema Michael Jackson ndie King of Pop wanachoangalia ni mafanikio aliyopata kupitia muziki... hakuna kigezo cha nani anaimba vizuri wakati hakuna mashindano kama hayo unless kama tunataka kuzungumzia BSS!
Hapa Tanzania, kuna wanamuziki wengi wazuri... binafsi, huwezi kuamini, namkubali zaidi Amin (yule wa THT) kuliko huyo Diamond au Ally Kiba lakini sina tangible evidence ya kuthibitisha kwamba Amin ndo mkali kuliko Diamond au Ally Kiba! Msanii anapofanya vizuri kwenye soko, assumption ya kwanza ni kwamba kazi zake zinakubalika otherwise, why people should dare to pay for something worthless? Hoja za wengine ni kwamba promo ndio zinambeba Diamond... sasa kama kuna mtu ambae hafahamu umuhimu wa promo kwenye soko la burudani basi huyo ni wa kumuhurumia! Lakini kubwa zaidi, hata ukiingia You Tube, miongoni mwa watu wanaosifia kazi za Diamond wala sio Watanzania... ina maana promo za Diamond zinafika hadi huko? Kama promo zake zinafika hadi huko, then the guy is good na hii si kashfa bali ni jambo la kupendeza... niishie tu kusema kwamba duniani hakuna mashindano ya kuimba(tukiacha ya kusaka vipaji) kwahiyo kilamtu atapimwa kutokana na vile anavyokubalika katika jamii!