Jose Chameleone: Siko katika Levo ya Kuomba Collabo na Diamond Platnumz

Jose Chameleone: Siko katika Levo ya Kuomba Collabo na Diamond Platnumz

Soma between the lines utaona tofauti kati ya kuomba na kuhangaikia (of course, kama yaliyoandikwa ndo yaliyosemwa). Kama kasema kuhangaikia, he is damn right.
You're right lakini mie nimezungumzia suala la kuomba kolabo kwa ujumla wake. Waanzilishi wa hili suala (bigeye.ug) walitumia neno "beg..." inawezekana ndio maana jamaa akaja juu...
 
Tatizo la Diamond akisimama na msanii mkubwa basi wapambe wa Diamond wanaanza kuzusha huyo msanii anataka collabo.Rejea ya Mafikizolo South Africa.
Sasa ndugu yangu, ile nyimbo ni ya Mafikizolo, yaani hapo bado unatarajia kwamba ni Diamond ndie kaomba afanye nyimbo na Mafikizolo wakati nyimbo si ya kwake? Unaanzaje... let me guess: "Hoya Mafikizolo, nyie hamtaki kuimba nyimbo itakayokamata Tanzania? Imbeni halafu nishirikisheni mimi....!" Does it make any sense? Kwanini unadhani Mafikizolo hawawezi kumuomba Diamond wafanye nae kolabo? Haya mambo nimeshasema mara kadhaa na nitaendelea kusema... mtu kutaka au kuomba kolabo haimaanishi kwamba huyo mtu ameishiwa... kollabo ni njia moja wapo tu ya kutaka kuteka soko la kule ambako wewe huna ushawishi mkubwa! Leo hii, msanii yeyote wa nje ya East Africa akiamua kupenya East Africa, moja ya watu ambao ataomba kufanya nao kazi ni Diamond... hakuna tatizo!!! Jambo lingine mtu unaamua kufanya kolabo na mtu mwingine kwa ajili ya kuleta ladha tofauti... tatizo liko wapi? As far as ile nyimbo ni ya Mafikizolo, basi sina shaka ni hao Mafikizolo ndio waliomba Kolabo na Diamond! Look, Djibouti ni kanchi kadogo sana... lakini mathalani leo hii mtu kama Diamond au yeyote yule akiamua kupenya Djbout, ata-opt kuomba kolabo na mtu wa huko hata kama mtu mwenyewe anafahamika ndani ya mipaka ya Djibouti peke yake!
 
Labda ningepata mtaalam wa muziki kama mzee Masoud Masoud,ili anifafanulie ukubwa wake kimuziki,ila mara ya mwisho aliubeza uwezo wa diamond kimuziki ukimlinganisha na King Kiba.
Nilimsikiliza Masoud Masoud ile siku... hakumbeza yeyote lakini alitamka wazi kwamba yeye anamkubali zaidi Ally Kiba... na hivi ndivyo ilivyo duniani kote... hakuna mwanamuziki hata mmoja duniani ambae alikubalika na kila mtu. Hilo moja, lakini lingine ukubwa wa mtu kimuziki unapimwa na mafanikio yake kwenye muziki... leo hii watu wanaposema Michael Jackson ndie King of Pop wanachoangalia ni mafanikio aliyopata kupitia muziki... hakuna kigezo cha nani anaimba vizuri wakati hakuna mashindano kama hayo unless kama tunataka kuzungumzia BSS!

Hapa Tanzania, kuna wanamuziki wengi wazuri... binafsi, huwezi kuamini, namkubali zaidi Amin (yule wa THT) kuliko huyo Diamond au Ally Kiba lakini sina tangible evidence ya kuthibitisha kwamba Amin ndo mkali kuliko Diamond au Ally Kiba! Msanii anapofanya vizuri kwenye soko, assumption ya kwanza ni kwamba kazi zake zinakubalika otherwise, why people should dare to pay for something worthless? Hoja za wengine ni kwamba promo ndio zinambeba Diamond... sasa kama kuna mtu ambae hafahamu umuhimu wa promo kwenye soko la burudani basi huyo ni wa kumuhurumia! Lakini kubwa zaidi, hata ukiingia You Tube, miongoni mwa watu wanaosifia kazi za Diamond wala sio Watanzania... ina maana promo za Diamond zinafika hadi huko? Kama promo zake zinafika hadi huko, then the guy is good na hii si kashfa bali ni jambo la kupendeza... niishie tu kusema kwamba duniani hakuna mashindano ya kuimba(tukiacha ya kusaka vipaji) kwahiyo kilamtu atapimwa kutokana na vile anavyokubalika katika jamii!
 
Muuza Sura

Huyo niliyemwakia hapo juu mara kibao sana alikuwa ananitukana lakini nilikuwa nampotezea hadi siku nilipomwambia leo mwisho... mtu akinizingua hata baada ya kumkanya, simwachi na huwa siangalii jinsia!! Nazungumza hilo la jinsia coz' jamvi la celebrities limejaa mademu na wana lugha chafu ajabu lakini ukiwakanya inakuwa ndo kama umewaambia wazidishe... ukiwageuzia kibao utawasikia "mwanaume mzima unagombana na mademu...!" utafikiri wao ndo wamepewa leseni ya kuwatolea wenzao maneno machafu!!!
 
Last edited by a moderator:
Kuomba kolabo haina maana kwamba hujui au ni msanii mdogo... unaweza kuomba kolabo kwa ajili ya kuchanganya ladha au kuteka soko la eneo fulani ambako unaamini mwenzako (hata kama ni mdogo kwako) anakubalika zaidi kuliko unavyokubalika wewe!!!

Ye anaweza tu na anakubalika vibaya sana.
 
Mi nilishasemaga kwenye moja ya thread zangu kuhusu huyu mtotot aliyekosa malezi bora aka Ndomo kuhusu kuombwa namba na Chris Brown huyu huyu wa With You, eti ameombwa namba ya simu ili wafanye collabo!
Yaani nilimshangaa sana Ndomondo!
Ulimsikia Diamond akisema au uliuziwa maneno na hawa jamaa hapa : Awatia Kiwewe!.jpg
 
Muuza Sura

Huyo niliyemwakia hapo juu mara kibao sana alikuwa ananitukana lakini nilikuwa nampotezea hadi siku nilipomwambia leo mwisho... mtu akinizingua hata baada ya kumkanya, simwachi na huwa siangalii jinsia!! Nazungumza hilo la jinsia coz' jamvi la celebrities limejaa mademu na wana lugha chafu ajabu lakini ukiwakanya inakuwa ndo kama umewaambia wazidishe... ukiwageuzia kibao utawasikia "mwanaume mzima unagombana na mademu...!" utafikiri wao ndo wamepewa leseni ya kuwatolea wenzao maneno machafu!!!

be calm please japo tunapishanaga kauli ila potezea wangu vitu vidogo tu hivi fake ids zisikunyime usingizi
pole sana
 
Last edited by a moderator:
Nilimsikiliza Masoud Masoud ile siku... hakumbeza yeyote lakini alitamka wazi kwamba yeye anamkubali zaidi Ally Kiba... na hivi ndivyo ilivyo duniani kote... hakuna mwanamuziki hata mmoja duniani ambae alikubalika na kila mtu. Hilo moja, lakini lingine ukubwa wa mtu kimuziki unapimwa na mafanikio yake kwenye muziki... leo hii watu wanaposema Michael Jackson ndie King of Pop wanachoangalia ni mafanikio aliyopata kupitia muziki... hakuna kigezo cha nani anaimba vizuri wakati hakuna mashindano kama hayo unless kama tunataka kuzungumzia BSS!

Hapa Tanzania, kuna wanamuziki wengi wazuri... binafsi, huwezi kuamini, namkubali zaidi Amin (yule wa THT) kuliko huyo Diamond au Ally Kiba lakini sina tangible evidence ya kuthibitisha kwamba Amin ndo mkali kuliko Diamond au Ally Kiba! Msanii anapofanya vizuri kwenye soko, assumption ya kwanza ni kwamba kazi zake zinakubalika otherwise, why people should dare to pay for something worthless? Hoja za wengine ni kwamba promo ndio zinambeba Diamond... sasa kama kuna mtu ambae hafahamu umuhimu wa promo kwenye soko la burudani basi huyo ni wa kumuhurumia! Lakini kubwa zaidi, hata ukiingia You Tube, miongoni mwa watu wanaosifia kazi za Diamond wala sio Watanzania... ina maana promo za Diamond zinafika hadi huko? Kama promo zake zinafika hadi huko, then the guy is good na hii si kashfa bali ni jambo la kupendeza... niishie tu kusema kwamba duniani hakuna mashindano ya kuimba(tukiacha ya kusaka vipaji) kwahiyo kilamtu atapimwa kutokana na vile anavyokubalika katika jamii!
Kamsikilize tena yule mzee,pia uache ujuaji lasivyo utaishia kuwalalamikia mods kila siku,endelea kumpikia diamond.
 
be calm please japo tunapishanaga kauli ila potezea wangu vitu vidogo tu hivi fake ids zisikunyime usingizi
pole sana

Hizi fake ids raha yake ni kwamba unaweza ukawa unatukanana na Mshua au Mtoto wako. au unaweza kukuta mtu mwenye miaka 40+ unajibisha na kitoto cha U-18 Mhimu ni kuwa wavumilivu tu
 
Hizi fake ids raha yake ni kwamba unaweza ukawa unatukanana na Mshua au Mtoto wako. au unaweza kukuta mtu mwenye miaka 40+ unajibisha na kitoto cha U-18 Mhimu ni kuwa wavumilivu tu

umeona eeeh...!!!
mi ndo maana napuuzaga japo sometimes inakera kweli
 
be calm please japo tunapishanaga kauli ila potezea wangu vitu vidogo tu hivi fake ids zisikunyime usingizi pole sana
Kupishana kauli wangu mbona kawaida sana... tena nikupe siri moja manake tumefahamiana hivi majuzi tu... suala la kupishana kauli kwangu nimeshalizoea sana tu... huku celebrities mie nakujaga kucheki watoto wazuri kama nyinyi tu lakini jukwaa langu ni la siasa... kule sina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu kwavile mawazo yangu yapo too independent... leo nitakufurahisha kesho nitakuboa! Na ajabu zaidi, watu ambao mara kwa mara huwa na-mingle nao humu jamvini ni JokaKuu na Mwita Maranya.... hawa wote mara nyingi kama sio zote huwa tunatofautiana lakini tunatofautiana kwa hoja na sio matusi!!! Sasa inakera mtu anavyoibuka from nowhere anaanza kukushambulia tena kwa matusi lakini hata ukimuonya bado anazidi.. come on geniviros, am not that good boy who can act like angel! Nikuambie kitu kimoja... in those old days I think I was a good boy, mtu hata akinitukana, namjibu "thanks God, I was raised by mom nd my mom would never accept me to react back with this...!" baada ya hapo, ningekula rundo la like... mwenyewe bichwa hilo!

Anyway, but thank you for your beautiful advice ila na wewe uache tabia ya kuingia Instagram na kuanza kumchamba Mange... just kidding but niitie Avemaria manake nimemshitukia... kumbe she's old friend of mine lakini akahamia mtaa wa pili bila kunijulisha!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kamsikilize tena yule mzee,pia uache ujuaji lasivyo utaishia kuwalalamikia mods kila siku,endelea kumpikia diamond.
Watu wengine bhana... sasa habari za Mods hapa zinatoka wapi au suala la kujifanya kujua linatoka wapi?? Kwahiyo unataka lazima nikubali unachosema wewe sio? Labda tuweke mambo sawa... let's assume huyo Masoud ndo kasema hivyo, so what?!
 
Back
Top Bottom