Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Lakini tunataka wauaji na waliowatumwa wakamatwe na kuwekwa nguvuni.

Kuuwa kwa kumtoboa mtu macho asiye na hatia macho ni unyama mkubwa kuzidi wa Idi Amin
 
Mungu atulinde
 

Sidhani kama ni wavuta bangi. Ni watu na akili zao ambao wamedhamiria kutishia umma wasijihusishe na siasa za upinzani.
Kuna kosa gani kuwa na mawazo tofauti, kama mtu havunji sheria na taratibu? Haya mambo ya kulazimisha kila mtu awe anaunga mkono juhudi, yalifanya USSR isambaratike. Maana nguvu zote walikuwa nazo watu wachache na walizitumia vibaya.
Putin mpaka leo anateseka na ndoto na ujinga ule. Anataka USSR irudi ilhali ilishaenda na ujinga wake. Jamii yetu isijiingize kwenye mtego kama ule. Tujenge nchi yenye kuheshimiana na kuheshimu sherai na taratibu.
Na hakuna mtu aliye juu ya sheria. Hata ukiwa unafanya kazi gani, bado hakuna aliyekupa mamlaka juu ya sheria. Tusijisahaulishe au kujizima data, tukaiharibu nchi yetu kwa ujinga wetyu wenyewe
 
Nchi nyingi zinazoelekea kwenye machafuko dalili zake huwa ni extrajudicial killings na kupotezwa kwa raia na mambo kama hayo.
Bangladesh ni mfano mmojawapo na mwishoe waziri mkuu Hasina akasepa.

Katika utawala wa Hasina, watu watatu tu kati ya 150 ndo walopatikana baada ya kutekwa na kupelekwa kusojulikana.

Leo hii kasepa watu hao watatu wamepatikana na wameungana na familia zao huku wale 147 ambao wamepotezwa mazima wakiwa ni historia.

Bangladesh wao wana magereza ya siri (secret prisons) zinoangaliwa na wanajeshi wa Military Intelligence na watu zaidi ya 700 walipotelea huko.

Na hawa wahindi weusi wana roho mbaya kupita kiasi na siku walipoingia barabarani Hasina hakuwa na chance akasepa na chopa kwenda India hadi leo yuko huko.
 
Au kwa lugha nyingine , tutawashngaa TISS, Polisi na hata Jeshi letu(kwa kiasi) wasipowaleta hadharani hawa wauaji.
Na kama hawatapatikana basi je, Kiongozi yeyote wa kitaifa akitekwa itakuwepo picha ipi?
 
Ndio mzee Butiku kawaasa wanahabari kwenda kumuuliza Spika kwanini alisema huvyo?

Kifupi Mzee Butiku kasema "Watanzania ni waoga", "Waandishi wa habari ni waoga"
Kasema Kwa uwazi kabisa. Hoja kuntu kama hii nashangaa watu hawajaiona.

Kawaambia waandishi wanapenda "kuambaa pembeni pembeni" πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Tukiahirisha kufikiri kizalendo tunawaita wasiojulikana, yaani unawajua lakini unajizima data na kusema huwajui, kwakuwaita wasiojulikana
 
Mbona taarifa nyingi

Vyombo vya ulinzi vipewe nafasi vifanye uchunguzi vilete taarifa

Wameshasema wanachunguza sasa jamii itulie isubiri taarifa

Matamko yanatosha sasa
Acha upuuzi wako ! Walikuwa wapi kufanya uchunguzi mpaka Rais awaagize!
Matamko ni muhimu na yanapaswa kuendelea kutolewa kwa nguvu na ukali zaidi ili vyombo hivyo vijue watu wamechoka na uzembe wao wa kuliaibisha Taifa hili !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…