Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amewaomba watanzania kushirikiana kupinga vitendo vibaya vya ulawiti, kuteka na kuuawa kwa watanzania vinavyoendelea nchini.

Amesema taifa letu si la wauwaji na wahuni, bali wananchi wanaishi kwa kufuata na kutiii katiba na sheria na wahalifu wanajulikana.

Amedai vyombo vya ulinzi na usalama vina nyenzo za kutosha kubaini wahalifu, na viongozi wa vyombo hivi wasituambie kwamba hawajui kinachoendelea nchini.
Hapa ndio nimeelewa kidogo alichokuwa amekikusudia kukifikisha kwa Wananchi na kwa Serikali Mzee Butiku !
Mzee Butiku na Taasisi yake wameanza kuona kuwa huko tunakotaka kuelekea kama Taifa siko kabisa. !
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amewaomba watanzania kushirikiana kupinga vitendo vibaya vya ulawiti, kuteka na kuuawa kwa watanzania vinavyoendelea nchini.

Amesema taifa letu si la wauwaji na wahuni, bali wananchi wanaishi kwa kufuata na kutiii katiba na sheria na wahalifu wanajulikana.

Amedai vyombo vya ulinzi na usalama vina nyenzo za kutosha kubaini wahalifu, na viongozi wa vyombo hivi wasituambie kwamba hawajui kinachoendelea nchini.
Hili lilipofika linahitaji mjadala wa kitaifa labda katiba yetu inaruhusu baadhi ya watu wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data
 
Hii ina maana kuna kundi la paramilitari linaloongozwa na wahuni likiitwa task force, maalumu kulinda chama na serikali linalofanya kazi zake kwa kificho.

Kiasi jeshi la polisi, usalama wa taifa, idara ya utambuzi TPDF (Military Intelligence) vyote vinaliogopa kundi hili la task force

Swali kuu ni kuwa kundi hili linapata mamlaka na nguvu kutoka kwa nani, nani anawapatia vifaa, fedha na rasilimali watu ?

Na kwanini kundi hili likawa nje ya taasisi rasmi za ulinzi na usalama zinazojulikana ?

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama mzigo huu unakuelemea, ikiwa taasisi zote za ulinzi zinalifahamu kundi hili lakini vinaogopa kuchukua hatua.

Je ni kweli kundi hili haliwezi kufikiwa na kukamatwa na kuletwa mbele ya vyombo vya mahakama baada ya rais kupewa nguvu, na kelele zinazopigwa na wananchi na mayowe wanayopiga polisi kuwa kuna watu wasiojulikana, haya yote hayampi rais ujasiri kulikabili kundi hili ?
Ina maana hata Sativa aliyesema alifikishwa kituo cha polisi oysterbay na baadae kukutwa pori la Katavi haitoshi kujua nani anahusika na matukio hayo?
 

TAARIFA YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TABIA MBAYA ZINAZOHATARISHA USALAMA WA MAISHA YA WATANZANIA NA MALI ZAO

Ndugu wanahabari nimewaiteni hapa, kuwaombeni kwanza; muisaidie Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuwataarifu Watanzania wote na kuwaomba sisi sote tushirikiane kuunga mkono kwa dhati Rais wetu Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya za kukomesha tabia mbaya zilizozuka katika Taifa letu za kulawiti, kuteka, kunyanyasa na kuua Watanzania wenzetu.

Tunaye Rais mmoja tu sio wawili wala watatu tuliye mkabidhi Katiba ya nchi yetu ili aitumie kuongoza Taifa letu na kulinda na kuhakikisha usalama wa Watanzania wote na wageni halali wanaoingia katika Taifa letu, na pia kulinda mali zetu. Huu ni wajibu wa Kikatiba wa Rais wetu anautekeleza kwaniaba yetu tumuunge mkono bila maswali.

Pili: kupendekeza kwa Watanzania wote, wananchi na viongozi, kukubali kwamba Taifa letu si la wauaji wala la wahuni, ni Taifa la watu wanaoishi kwa kuzingatia Katiba ya nchi yetu na sheria zinazotokana na Katiba hiyo sisi sote tunao wajibu wa kufuata na kutii Katiba yetu na sheria zote zinazotokana Katiba hiyo, na ambazo hazikiuki Katiba. Hakuna nafasi wala ruhusa kwa raia yoyote wa nchi hii kuishi nje ya utaratibu huu. Huu ndio msingi wa amani, umoja, na maendeleo yanayo shirikisha wananchi wote kwa faida yao. Kwa maana hii, sisi Watanzania ni wastaarabu.

Tusiseme hatuwajui wahalifu hao, tunawajua. Wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wako ndani ya vyombo vyetu vya dola, wako makanisani na katika misikiti. Tunawajua, lazima serikali yetu iwajue. Kwahiyo Taasisi ya Mwalimu Nyerere inaomba tumsaidie Rais kupata taarifa sahihi kuhusu wabaya wetu hao ili achukue hatua stahili. Anavyo vyombo vya dola vyenye majukumu mahsusi ya kumpa taarifa za uhakika. Nchi yetu imeviwezesha kuwa na uwezo wa kutosha wa utaalamu na


Hawa nao wanabweka na kupiga kelele vilevile kama wengine....

Rais Samia Suluhu Hassan ameshasaidiwa kwa kuambiwa anachopaswa kufanya kwa mujibu wa katiba...

Mzee Butiku na taasisi yako, huyu Rais sisi wananchi tumeshamwambia aunde tume maalumu ya kijaji bila kuhusisha polisi wala TISS ambao nao ni watuhumiwa ili ichunguze mambo haya....

Kwani mnataka wananchi tumpe msaada upi zaidi ya yeye kutumia mamlaka yake ya kikatiba kutimiza wajibu wake....?

Mnataka wananchi tumsaidieje kwa mfano? Kwamba kila mwananchi abebe rungu na panga tuingie mitaani kuwasaka magaidi na majambazi hawa au....?

Rais hawezi kuwaagiza polisi na TISS haohao wanaotuhumiwa wajichunguze. Hili anapaswa kulijua kama anajipenda kweli....!!
 
Yaani jeshi la Polisi huwa linakuwa na majibu mepesi Kwa maswali magumu.

Eti ishu ya Lissu walidai eti mpaka dereva wa Lissu apatikane.
Na wakasema hawafanyii kazi taarifa za mtandaoni na kumtaka Lissu na dereva wake wafike polisi lakini tukio la kinyama la kada wa CDM wametoa taarifa kwa kurejea source za mitandaoni. Mtu yeyote anayeamini wanasiasa wanaosema nchi ina amani warejee tukio la Lissu. Kama mtu mashuhuri kama Lissu anapigwa risasi mchana kweupe tena kwenye eneo la serikali linalolindwa na hakuna hatua zilizochukuliwa jiulize vipi kwa mwananchi wa kawaida. Amani ipo kwa watawala na wote walioshikamana na ccm.
 
Na wakasema hawafanyii kazi taarifa za mtandaoni na kumtaka Lissu na dereva wake wafike kituoni lakini tukio la kinyama la kada wa CDM wametoa taarifa kwa kurejea source za mitandaoni. Hicho chombo akipatikana rais mzalendo asiyeendeshwa na mihemko ya hofu ya uchaguzi na madaraka hawezi kukiacha kama kilivyo lazima kifumuliwe.
Tangu IGP Mangu amestaafu imekuwa changamto sana
 
Kwa wale waliosomea Cuba tu ,
Naomba ufafanuzi kidogo kwa kile alichokisema Mzee Butiku na kukusisitiza kwamba
Tunaye Rais mmoja tu wa Tanzania 🇹🇿
Hatuna maraisi wawili wala watatu tunaye mmoja tu !

Ambaye ndiye anayetakiwa na Katiba kuiendesha Nchi kwa mujibu wa Sheria na kuilinda Katiba ya Nchi kama alivyoapa kuilinda !

Je Taasisi yake Mzee Butiku imehisi wapo wengine huko pembeni ndio wanaoleta hizi Tafrani ???!!
 
Tusiseme hatuwajui wahalifu hao, tunawajua. Wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wako ndani ya vyombo vyetu vya dola, wako makanisani na katika misikiti. Tunawajua, lazima serikali yetu iwajue.
Tunawajua ndio na this time tutadili nao! Hakuna damu itamwagika kizembe tena! Watalipa! Wao au wengine
 
Wakati Sheria ya Usalama wa Taifa inafanyiwa marekebisho Mwaka Jana pale Bungeni, Mhe. Lissu aliipigia sana Kelele lakini bahati mbaya hakupata sapoti ya kutosha.

Kwa kifupi hao Jamaa wamepewa Mandeti kubwa ya kufanya na kutenda mambo mengi ya gizani pasipo kuhojiwa huku Wakilindwa na Sheria hiyo mpya.

Tukiendelea kunyamaza wataendelea kutesa na kuwapoteza watu hadi wote tuishe
 
Back
Top Bottom