Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku amesema Wahalifu wanaofanya vitendo vya utekaji na mauaji wanajulikana na kwamba wengine wamo hadi kwenye Vyombo vya Dola huku akiwataka Wananchi kushirikiana na Serikali kuwafichua na wanapobainika wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo September 10,2024, Mzee Butiku amesema “Sisi Watanzania ni Wastaarabu, tusiseme hatuwajuwi Wahalifu hawa (wanaofanya mauaji na utekaji) ukweli ni kwamba tunawajua, wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wapo ndani ya Vyombo vyetu vya dola, wapo Makanisani na Misikitini, narudia tena tunawajua na hapa ni lazima Serikali yetu iwajuwe”

“Taasisi ya Mwl Nyerere inaomba tumsaidie Rais Samia kupata taarifa sahihi kuhusu wabaya wetu hawa ili achukue hatua stahiki, anavyo Vyombo vya Dola vyenye majukumu mahsusi ya kumpatia taarifa za uhakika, Nchi yetu imeviwezesha Vyombo hivyo kuwa na uwezo wa kutosha wa utaalamu na uwezo wa vitendea kazi, Viongozi wa Vyombo hivyo wasituambie kwamba hawajuwi kinachotokea, wanajua, wasituambie kwamba wanamuogopa Rais, wasimsingizie, wote tumsaidie Rais wetu, tusiogope”

“Vyombo vya usalama ni Binadamu tu kama wewe Mwandishi na huenda miongoni mwetu humu wapo wengine kwasababu usalama ni Watu wengi, kila Mtanzania kwa mujibu wa Katiba yetu ni Mtu wa kuhakikisha kwamba Taifa hili linalindwa, Vyombo vya usalama ni Watu kama sisi, la kwanza kabisa si wote lakini wamo wachache wanaofanya hivyo (vitendo vya uhalifu kama uuaji na utekaji) lakini tunachosema kuhusu Vyombo vya usalama ni kwamba lazima wawajibike hasa Viongozi wao”
 
Lakini Tanzania HATUNA waandishi wa habari tena haswa baada ya ujio wa hizi redio za kishikaji. Unakuta mtu anatangaza ila haelewi anatangaza ama anaelimisha nini jamii, anajikuta anaongea na kupiga story as if yuko kijiweni na marafiki zake. Redio binafsi zimeua kabisa tasnia ya habari na muziki wetu wa maana (dansi).
 
Lakini Tanzania HATUNA waandishi wa habari tena haswa baada ya ujio wa hizi redio za kishikaji. Unakuta mtu anatangaza ila haelewi anatangaza ama anaelimisha nini jamii, anajikuta anaongea na kupiga story as if yuko kijiweni na marafiki zake. Redio binafsi zimeua kabisa tasnia ya habari na muziki wetu wa maana (dansi).
Muda mwingi Wanaongelea mambo yanayo wavutia wao
 
Huyu mtu Maliyamungu wa Tanzania na wenzie, inatakiwa apatikane, hata kwa kutolewa 'sadaka' si kwa kuuawa bali wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa baada ya vyombo rasmi vya ulinzi na usalama kupewa meno kuwakamata ili amiri jeshi mkuu asalimike na fedheha hii kwa taifa, ijulikane kama je viliundwa na mtangulizi kiasi rais aliyepo anaagwaya kuvikabili.

Lakini umma wa ndani tayari kupitia kelele za wananchi zinampa mamlaka rais awashughulikie kwa mujubu wa sheria Maliyamungu na wavuta bangi wenzie wote waliopo katika Task Force.
Mkuu nimekufuatilia namna unavyotiririka, kwa hakika unayajua mambo mengi ambayo members wengi humu hatuyajui na tunabaki kuyabishania.

Hii Task force hii ni kinyago alichokifinyanga Rais kwa mikono yake na sasa kimeanza kumtisha na kweli anakigwaya, kama ni kweli mambo yanayofanywa nacho Rais atakua hayajui.

Haiwezekani kundi hilo liteke watu na kufanya mauaji ya kufuru na Rais asijue ama asijulishwe!

Hapa kuna mawili: aidha Rais anajua kindakindaki kinachoendelea na kuna baraka zake na ama kama yanayofanyika hayana baraka zake na hajulishwi basi hiyo Task force itakuwa ni genge lisiloshikika kwa nguvu kubwa walizonazo kuliko nguvu za Amiri jeshi wao mkuu.

Chain of command za majeshi yote zinavyofanya kazi, amri kubwa ya kupoteza maisha ya watu, haiwezi kuasisiwa katikati na kushushwa chini kutekelezwa bila kuwa na baraka za kiongozi mkuu.

Na kama kutakuwa na utekelezaji wa dharula, basi taarifa lazima apelekewe Amiri jeshi mkuu Asp.

Hili tamko la Rais kutaharuki juu ya kutekwa na kuuawa kwa kiongozi wa Cdm, raia linatuacha njia panda kutokana na kile alichokitamka, ambacho kwa kawaida za mamlaka yake hakiwezekani kuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom