Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Joseph Butiku: Vyombo vya Ulinzi na Usalama visijifanye havijui mambo yanayoendelea nchini

Kundi kama hili kule Uganda ya Amini lilikuwa likiongozwa na Maliyamungu sasa hapa sijui linaongozwa na nani?!
Kuna mtu yupo Dar ana asili ya Arusha ndiye steering wa hiyo movie.

CHADEMA wanamdharau lakini yupo Dar kwa kazi maalum ya kuwamaliza na wengine wanadhani ni rafiki Yao kumbe ndiye mhandisi wa haya mambo.
 
Mbona taarifa nyingi

Vyombo vya ulinzi vipewe nafasi vifanye uchunguzi vilete taarifa

Wameshasema wanachunguza sasa jamii itulie isubiri taarifa

Matamko yanatosha sasa

Usiwatetee. Inawezekana kuna elements within ambazo zinahusika. Ndio maana hawa senior citizens wanatoa kauli kama hizi.
Kuwa chama cha upinzani haina maana ni kuwa adui. Kukesha mitandaoni kupiga porojo za siasa haina maana ni threat kwa wanaoongoza.
Kuuana ni kitu kibaya na yeyote anayefanya hivyo, uzoefu unaonyesha atalipia tu. Mwenyezi Mungu hajawahi kulala wala kusinzia. Na hakuna kati yetu ambaye maisha yake ni bora kuliko mwingine.
Sote tumekuja na tutakwenda. hata kama tunawaonea na kuwadhulumu wenzetu tunavyotaka. Ipo siku yetu. Every dog has its day, waingereza wanasema.
 
TAARIFA YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TABIA MBAYA ZINAZOHATARISHA USALAMA WA MAISHA YA WATANZANIA NA MALI ZAO

Ndugu wanahabari nimewaiteni hapa, kuwaombeni kwanza; muisaidie Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuwataarifu Watanzania wote na kuwaomba sisi sote tushirikiane kuunga mkono kwa dhati Rais wetu Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya za kukomesha tabia mbaya zilizozuka katika Taifa letu za kulawiti, kuteka, kunyanyasa na kuua Watanzania wenzetu.

Tunaye Rais mmoja tu sio wawili wala watatu tuliye mkabidhi Katiba ya nchi yetu ili aitumie kuongoza Taifa letu na kulinda na kuhakikisha usalama wa Watanzania wote na wageni halali wanaoingia katika Taifa letu, na pia kulinda mali zetu. Huu ni wajibu wa Kikatiba wa Rais wetu anautekeleza kwaniaba yetu tumuunge mkono bila maswali.

Pili: kupendekeza kwa Watanzania wote, wananchi na viongozi, kukubali kwamba Taifa letu si la wauaji wala la wahuni, ni Taifa la watu wanaoishi kwa kuzingatia Katiba ya nchi yetu na sheria zinazotokana na Katiba hiyo sisi sote tunao wajibu wa kufuata na kutii Katiba yetu na sheria zote zinazotokana Katiba hiyo, na ambazo hazikiuki Katiba. Hakuna nafasi wala ruhusa kwa raia yoyote wa nchi hii kuishi nje ya utaratibu huu. Huu ndio msingi wa amani, umoja, na maendeleo yanayo shirikisha wananchi wote kwa faida yao. Kwa maana hii, sisi Watanzania ni wastaarabu.

Tusiseme hatuwajui wahalifu hao, tunawajua. Wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wako ndani ya vyombo vyetu vya dola, wako makanisani na katika misikiti. Tunawajua, lazima serikali yetu iwajue. Kwahiyo Taasisi ya Mwalimu Nyerere inaomba tumsaidie Rais kupata taarifa sahihi kuhusu wabaya wetu hao ili achukue hatua stahili. Anavyo vyombo vya dola vyenye majukumu mahsusi ya kumpa taarifa za uhakika. Nchi yetu imeviwezesha kuwa na uwezo wa kutosha wa utaalamu na

Tutamsaidiaje rais wakati yeye ni mtuhumiwa namba moja. Ilikuwaje akamrudisha Bashite madarakani wakati ana tuhuma nzito za kushiriki utekaji na mauaji? Haipendezi wazee kama wewe kuwa chawa
 
Tutamsaidiaje rais wakati yeye ni mtuhumiwa namba moja. Ilikuwaje akamrudisha Bashite madarakani wakati ana tuhuma nzito za kushiriki utekaji na mauaji? Haipendezi wazee kama wewe kuwa chawa
Umemuelewa Mzee Butiku?

Kuna mtu anayetakiwa kusaidiwa bila ya kuelemewa? Someni katikati ya hoja yake badala ya kusoma kimsisimko.
 
Unajiabisha kuita taarifa ya Mzee Butiku kuwa ni taarifa za barabarani. Labda uwe humjui Mzee Butiku na nafasi yake kwenye vyombo vya Ulinzi na usalama vya nchi hii.

Mtu wa barabarani anaweza kuwa Mzee Butiku?
Wakiishafanya mambo yao ya aibu kuteka kutesa na kuua watu hukimbilia kwenye media kama JF na kujitekenya na kuchelekelea huku wakiandika ujinga mtupu.
 
Kundi kama hili kule Uganda ya Amini lilikuwa likiongozwa na Maliyamungu sasa hapa sijui linaongozwa na nani?!

Huyu mtu Maliyamungu wa Tanzania na wenzie, inatakiwa apatikane, hata kwa kutolewa 'sadaka' si kwa kuuawa bali wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa baada ya vyombo rasmi vya ulinzi na usalama kupewa meno kuwakamata ili amiri jeshi mkuu asalimike na fedheha hii kwa taifa, ijulikane kama je viliundwa na mtangulizi kiasi rais aliyepo anagwaya kuvikabili.

Lakini umma wa ndani tayari kupitia kelele za wananchi zinampa mamlaka rais awashughulikie kwa mujibu wa sheria Maliyamungu na wavuta bangi wenzie wote waliopo katika Task Force.
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amewaomba watanzania kushirikiana kupinga vitendo vibaya vya ulawiti, kuteka na kuuawa kwa watanzania vinavyoendelea nchini.

Amesema taifa letu si la wauwaji na wahuni, bali wananchi wanaishi kwa kufuata na kutiii katiba na sheria na wahalifu wanajulikana.

Amedai vyombo vya ulinzi na usalama vina nyenzo za kutosha kubaini wahalifu, na viongozi wa vyombo hivi wasituambie kwamba hawajui kinachoendelea nchini.
Wizara ya Mambo ya ndani ifumuliwe. Kuna wahunu wengi pale
 
Huyu mtu Maliyamungu wa Tanzania na wenzie, inatakiwa apatikane, hata kwa kutolewa 'sadaka' si kwa kuuawa bali wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa baada ya vyombo rasmi vya ulinzi na usalama kupewa meno kuwakamata ili amiri jeshi mkuu asalimike na fedheha hii kwa taifa, ijulikane kama je viliundwa na mtangulizi kiasi rais aliyepo anaagwaya kuvikabili.

Lakini umma wa ndani tayari kupitia kelele za wananchi zinampa mamlaka rais awashughulikie kwa mujubu wa sheria Maliyamungu na wavuta bangi wenzie wote waliopo katika Task Force.
Wanazi wengi walokuwa wakitekeleza kazi za Adolf Hitler wengi wamekuwa wakikamatwa wakiwa wazee hata umri wa miaka 100 ni lazima wafikishwe mahakamani.

Hivyo ipo siku moja watapatikana.
 
TAARIFA YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TABIA MBAYA ZINAZOHATARISHA USALAMA WA MAISHA YA WATANZANIA NA MALI ZAO

Ndugu wanahabari nimewaiteni hapa, kuwaombeni kwanza; muisaidie Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuwataarifu Watanzania wote na kuwaomba sisi sote tushirikiane kuunga mkono kwa dhati Rais wetu Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya za kukomesha tabia mbaya zilizozuka katika Taifa letu za kulawiti, kuteka, kunyanyasa na kuua Watanzania wenzetu.

Tunaye Rais mmoja tu sio wawili wala watatu tuliye mkabidhi Katiba ya nchi yetu ili aitumie kuongoza Taifa letu na kulinda na kuhakikisha usalama wa Watanzania wote na wageni halali wanaoingia katika Taifa letu, na pia kulinda mali zetu. Huu ni wajibu wa Kikatiba wa Rais wetu anautekeleza kwaniaba yetu tumuunge mkono bila maswali.

Pili: kupendekeza kwa Watanzania wote, wananchi na viongozi, kukubali kwamba Taifa letu si la wauaji wala la wahuni, ni Taifa la watu wanaoishi kwa kuzingatia Katiba ya nchi yetu na sheria zinazotokana na Katiba hiyo sisi sote tunao wajibu wa kufuata na kutii Katiba yetu na sheria zote zinazotokana Katiba hiyo, na ambazo hazikiuki Katiba. Hakuna nafasi wala ruhusa kwa raia yoyote wa nchi hii kuishi nje ya utaratibu huu. Huu ndio msingi wa amani, umoja, na maendeleo yanayo shirikisha wananchi wote kwa faida yao. Kwa maana hii, sisi Watanzania ni wastaarabu.

Tusiseme hatuwajui wahalifu hao, tunawajua. Wanaishi miongoni mwetu na katika kaya zetu, wako ndani ya vyombo vyetu vya dola, wako makanisani na katika misikiti. Tunawajua, lazima serikali yetu iwajue. Kwahiyo Taasisi ya Mwalimu Nyerere inaomba tumsaidie Rais kupata taarifa sahihi kuhusu wabaya wetu hao ili achukue hatua stahili. Anavyo vyombo vya dola vyenye majukumu mahsusi ya kumpa taarifa za uhakika. Nchi yetu imeviwezesha kuwa na uwezo wa kutosha wa utaalamu na

Spika alidai hakuna utekaji. Alifoka sana.
Alisema watu wanatekwa na wachawi
 
Ndicho alichokisema Mzee Butiku. Na nimependa anapowalaumu waandishi wa habari kupenda kutafuniwa Kila kitu.
Mzee Butiku ana busara sana na anawafahamu waandishi wetu wa habari na tabia zao hivyo amezungumza kwa level yao.

Hawezi kufunguka sana maana kitachoandikwa kesho chaweza kuwa ni kitu kingine.

Ila Mzee Butiku na mzee Warioba, Jenerali Ulimwengu na Issa Shivji na watu makini sana na wana hazina ya maarifa.

Kawapa homework wamtafute waziri Masauni wamhoji na hii ndo opportunity kwa Mr Odemba kuitumia.
 
Mbona taarifa nyingi

Vyombo vya ulinzi vipewe nafasi vifanye uchunguzi vilete taarifa

Wameshasema wanachunguza sasa jamii itulie isubiri taarifa

Matamko yanatosha sasa
Kama haya yanayo endelea vyombo vya usalama hawajui basi ita fika siku wahuni wata ingia Ikulu bila wao kuwa na taarifa na wata sema wana chunguza hao wahuni wameingia je Ikulu.
Best option Waziri, IGP, Dg wa Tiss na Waziri wake watuachie ofisi zetu Rais aweks wagu wenye weledi wa ulinzi na usalama wa nchi.
Pia Mh. Rais asidharau ujumbd wananchi walio mpa Masauni jana.
Kama hata juizulu kwa hiari yeue na IGP basi Rais ambae ndio mwajiri wao awatengue kwenye nafasi zao
 
Wanazi wengi walokuwa wakitekeleza kazi za Adolf Hitler wengi wamekuwa wakikamatwa wakiwa wazee hata umri wa miaka 100 ni lazima wafikishwe mahakamani.

Hivyo ipo siku moja watapatikana.

Kweli vilikuwepo vikundi vya vijana wa chama cha NAZI cha Hitler na mamluki wa kigeni ndani ya GESTAPO SS waliofadhiliwa na kuratibiwa na machawa wa Hitler ambao waliogopwa na Polisi pia kuogopwa na jeshi rasmi.

Hili kundi la TASK FORCE la paramilitary la watu wasiojulikana Tanzania litakuwa limeundwa kwa mtindo huo huo wa GESTAPO na SS

The SS (Schutzstaffel) was a major paramilitary organisation under Adolf Hitler and the Nazi Party in Nazi Germany.

Mkuu wa Usalama wa Taifa Bw. Suleiman Abubakar Mombo ambaye amepata kuwa muambata katika ubalozi wa Tanzania mjini Brasil Brazil kama atatumika vizuri na hayumo ktk kuratibu, atakuwa amepata uzoefu mzuri wa Latin Amerika ya ilivyokuwa chini ya Junta ya madiktekta wa kijeshi walivyoweza kudhibitiwa magenge yao ya kutishia watu kwa ukatili, vifungo feki, kupotezwa na kuuawa.

Hivyo ikiwepo nia njema basi vyombo vyetu rasmi vya ulinzi na usalama vikipata sapoti ya amiri jeshi mkuu (rais JMT), sapoti ya chama kongwe kupitia Katibu Mkuu wanaweza kabisa kukisambaratisha kikosi hiki cha watu wanaosemekana wamepewa jina la Watu Wasiojulikana lakini ambao wanajulikana ila wanaogopwa vikali. Hatujui sababu ya kuogopwa na serikali.

TOKA MAKTABA :
Brasilia, Brazil

Bolozi wa Tanzania nchini Brazil awasilisha hati za Utambulisho
June 27, 2017, 11:28 pm

Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Brazil Mhe. Michel Temer, Tarehe 26 Juni, 2017. Rais Temer alisifu jitihada za Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupigana na umasikini na kuleta maendeleo kwa wananchi. Brazil imeihakikishia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kufanikisha miradi mbalimbali ya ushirikiano.

Mhe. Rais Michel Temer na Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil Mhe. Aloysio Nunes Ferreira Filho (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, watatu kutoka kulia ni Mama Balozi Jane Nchimbi, Bw. Frank J. Mhina, Afisa Ubalozi na Mkuu wa Utawala; na Bw. Suleiman Abubakar Mombo (the Plenipotentiary Minister of the Embassy) yaani Afisa Mwandamizi wa Ubalozi.

Balozi Dkt. Nchimbi na Mama Balozi Jane Nchimbi, wakisindikizwa Mara baada ya kumaliza kuwasikisha hati za Utambulisho kwa Rais
 
Back
Top Bottom