Joseph Haule (Prof. Jay): Sasa nipo Imara, Namshukuru Rais Samia, Mbowe, Watanzania na Familia. See you soon

Kukonda ndio ishara ya afya yake kuimarika. The guy was overweight na hiyo linaweza kuwa ilichangia hayo maradhi kumpata. Mungu aendelee kumponya kwani alikuwa artist mzuri sana. Nasikia Samia kafuta bili zote za matibabu yake!
Napenda nieleweke mimi sipo against na yeyote kusaidiwa na toka mwanzo humu zilipoletwa arifa Jay ni mgonjwa na serikali imejitolea kumtibu tupo tuliohoji wangapi wamesaidiwa kwa njia hiyo?point hasa ikiwa kwamba inaeleweka maradhi ya figo yanahitaji gharama kubwa na kwa status ya Jay akiwa kama mbunge mstaafu (wakati huo) alikuwa na nafasi kubwa bado kutumia kile ali-earned huko kwenye siasa kisha hicho cha serikali kikaenda kuboresha vitengo vya figo kuwapunguzia maumivu walio maskini.

Personally sikusema asisaidiwe ila hii inazua mikingamo mingi sana,ninapo-type hapa kuna katoto ka Kisambaa (four years) kalizaliwa na matatizo ya kichwa kikubwa na utosi kutokauka baba yake ni maskini huko kwao Tanga kazi yake ilikuwa kurina asali mtoto amefariki juzi jumamosi alfajiri huyu bwana alishauza kila kitu kupambana mwanae apone ila kafa pale MNH kapewa bill Tsh 2,470,000/= kawaambia hana wamemwambia maiti ya mwanae hawampi hadi apeleke angalao Tsh 700,000/= hapo bado gharama za mazishi hajaandaa hiyo nauli tu ya kumtoa Buza kwenda Muhimbili alikuwa naomba kwa watu.

Tunaweza tukaona ni jinsi gani maisha yanafanywa kuwa magumu,anyway basi kama uwezekano wa bills kufutwa upo iwe ruhusa mtu mgonjwa wake akifariki apewe mwili akamsitiri maiti wake asahau machungu ila ajabu Tanzania hii tajiri anasamehewa maskini anakomeshwa.
 
Huyu jamaa, naona bado hajapona vizuri.

Halafu mbona kakonda sana?

Wazee wa ramli chonganishi, vibuyu vinasemaje huko?

====

Salaam Ndugu zangu,
View attachment 2607620
Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai. Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi.

Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote, kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu, namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Mbowe, Wanachama na Viongozi wote Waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali.

Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili, hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ahsanteni sana.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa GJ na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea, Mungu awabariki sana.

Kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu, mke wangu, kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mlionipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana, Mungu ni mwema sana siku zote[emoji1317][emoji1317][emoji1317].

Ahsanteni,
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon[emoji3590][emoji3590][emoji3590][emoji3590]
Mungu Ni mwema sna mm naona kbsa afya yake inarudi vzr ataka sawa tu mzee wa mitulingaa

HV kygata umeshapata Kaz nn serekalin mnk uonekani kbsa kwenye uzi ule wa utumishi
 
Huyu jamaa, naona bado hajapona vizuri.

Halafu mbona kakonda sana?

Wazee wa ramli chonganishi, vibuyu vinasemaje huko?

====

Salaam Ndugu zangu,
View attachment 2607620
Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai. Hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).

Pili Kipekee namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi.

Asante sana Mama pamoja na serikali yako yote, kwani viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji.

Tatu, namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Mbowe, Wanachama na Viongozi wote Waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na serikali.

Zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili, hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ahsanteni sana.

Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu asanteni sana na sitowasahau.

Shukrani sana kwa Malisa GJ na Lyenda kwa kusimamia michango hiyo pamoja na vyombo vyote vya habari na social media nchini vilivyoshirikiana navyo kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM na vyombo vingine mbalimbali pamoja na Watumishi wa Mungu wote walioongoza ibada maalum ya kuniombea, Mungu awabariki sana.

Kuanzia Wachungaji, Mashekh na Mapadre wote wa kanisa langu Katoliki sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea Mungu awabariki sana.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru familia yangu, mke wangu, kaka zangu, dada zangu, wadogo zangu na familia yote ya Mzee Haule kwa ushirikiano mkubwa na upendo mlionipa.

Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana, Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻.

Ahsanteni,
Joseph Haule (Prof. Jay)
#MgodiUnaotembea
#SeeYouSoon❤️❤️❤️❤️
Mungu ni mwema kila wakati
 
Napenda nieleweke mimi sipo against na yeyote kusaidiwa na toka mwanzo humu zilipoletwa arifa Jay ni mgonjwa na serikali imejitolea kumtibu tupo tuliohoji wangapi wamesaidiwa kwa njia hiyo?point hasa ikiwa kwamba inaeleweka maradhi ya figo yanahitaji gharama kubwa na kwa status ya Jay akiwa kama mbunge mstaafu (wakati huo) alikuwa na nafasi kubwa bado kutumia kile ali-earned huko kwenye siasa kisha hicho cha serikali kikaenda kuboresha vitengo vya figo kuwapunguzia maumivu walio maskini.

Personally sikusema asisaidiwe ila hii inazua mikingamo mingi sana,ninapo-type hapa kuna katoto (four years) kalizaliwa na matatizo ya kichwa kikubwa na utosi kutokauka baba yake ni maskini huko kwao Tanga kazi yake ilikuwa kurina asali mtoto amefariki juzi jumamosi alfajiri huyu bwana alishauza kila kitu kupambana mwanae apone ila kafa pale MNH kapewa bill Tsh 2,470,000/= kawaambia hana wamemwambia maiti ya mwanae hawampi hadi apeleke angalao Tsh 700,000/= hapo bado gharama za mazishi hajaandaa hiyo nauli tu ya kumtoa Buza kwenda Muhimbili alikuwa naomba kwa watu.

Tunaweza tukaona ni jinsi gani maisha yanafanywa kuwa magumu,anyway basi kama uwezekano wa bills kufutwa upo iwe ruhusa mtu mgonjwa wake akifariki apewe mwili akamsitiri maiti wake asahau machungu.
Mkuu uchawi acheni Tena mnawanga au mlitaka kusikia prof jize amekufa ?

Swala Serikali kutoa Huduma mbovu Alina uhusiano na kuokoa maisha ya heavy weight Mc mgodi unaotembea
 
Wewe ni daktari wake mkuu? Na hata kama ni daktari wake amekuruhusu useme ugonjwa wake kwa jamii?
Yaani achqngiwe lkn ugonjwa wake usitajwe? Waliochangia kwenye uzi huu wanasema mwamba ana ukimwi uliosababisha Figo kufeli. Kama madai haya siyo kweli leta ya kwako
 
Sipendi kusema watu lakini mdomo wake umelika kwasababu ya pombe. Ujumbe hapa ukifika miaka 40 jitahidi achana na pombe za kuzidi, sukari, vyakula vya wanga, fanya mazoezi na medical check up!. Bila kuelezana ukweli na vitu vilivyo changia tatizo lakini hatuta tenda haki kutoa elimu ya afya. Pole sana Prof Jay
We jamaa hujawah kukaa na J hapa na hapa lip ya chini ya mdomo wa J ni huwa nyekundu since then nakumbuka mwaka 2012 niliwah kukaa nae maisha ya Masaki enzi hizo tukala kala vitu alikuwa na mkoloni tulipiga sana story... He is a very humble guy....
 
Yaani achqngiwe lkn ugonjwa wake usitajwe? Waliochangia kwenye uzi huu wanasema mwamba ana ukimwi uliosababisha Figo kufeli. Kama madai haya siyo kweli leta ya kwako
We ulichanga sh ngapi? Ukimwi mnao nyie TU familia zenu .
 
Tuambie wewe mwerevu unayejua. Badala ya kutushambulia tunataka kujua alikuwa anaumwa nn toa maelezo alikuwa anaumwa kitu gani!
Tuchukulie kwa mfano anaumwa ukimwi. What is the big deal? Wamekufa wangapi hapa wanaugua minyoo tu? Wengine hawana ukimwi wanakula vitu vichafu, wanaharisha mpaka wanakufa.
Anayedhani amesimama.....
 
Mkuu uchawi acheni Tena mnawanga au mlitaka kusikia prof jize amekufa ?

Swala Serikali kutoa Huduma mbovu Alina uhusiano na kuokoa maisha ya heavy weight Mc mgodi unaotembea
Bro!

Tafadhali weka mahaba pembeni changia ukiwa na akili huru za utu,maisha ya matibabu Tanzania ni mabaya sana usiombe yakukute hasa uwe huna hela.

Naandika haya mimi nimewahi kushuhudia mtu anakosa 500/= ya kununua paracetamol atulize maumivu ili ajue aende akafie wapi na yupo duka la dawa la serikali na hakuna anayemsikiliza,mimi sina roho mbaya kwamba sitaki Jay apone nazungumza uhalisia wa maisha ya Mtanzania wa hali ya chini yule asiyeijua leo yake ataiishi vipi.
 
S
We jamaa hujawah kukaa na J hapa na hapa lip ya chini ya mdomo wa J ni huwa nyekundu since then nakumbuka mwaka 2012 niliwah kukaa nae maisha ya Masaki enzi hizo tukala kala vitu alikuwa na mkoloni tulipiga sana story... He is a very humble guy....
Sure hawamjui prof Mimi nimekaa naye mwaka 2013 Hotel ya victoria Bukoba midomo yake ndo ilivyo it been a long time Pia issue ya midomo kuwa hivyo ni watu wengi Sana midomo miekundu. Na hawana ngoma.
 
Back
Top Bottom