The Worst
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 6,108
- 21,140
Napenda nieleweke mimi sipo against na yeyote kusaidiwa na toka mwanzo humu zilipoletwa arifa Jay ni mgonjwa na serikali imejitolea kumtibu tupo tuliohoji wangapi wamesaidiwa kwa njia hiyo?point hasa ikiwa kwamba inaeleweka maradhi ya figo yanahitaji gharama kubwa na kwa status ya Jay akiwa kama mbunge mstaafu (wakati huo) alikuwa na nafasi kubwa bado kutumia kile ali-earned huko kwenye siasa kisha hicho cha serikali kikaenda kuboresha vitengo vya figo kuwapunguzia maumivu walio maskini.Kukonda ndio ishara ya afya yake kuimarika. The guy was overweight na hiyo linaweza kuwa ilichangia hayo maradhi kumpata. Mungu aendelee kumponya kwani alikuwa artist mzuri sana. Nasikia Samia kafuta bili zote za matibabu yake!
Personally sikusema asisaidiwe ila hii inazua mikingamo mingi sana,ninapo-type hapa kuna katoto ka Kisambaa (four years) kalizaliwa na matatizo ya kichwa kikubwa na utosi kutokauka baba yake ni maskini huko kwao Tanga kazi yake ilikuwa kurina asali mtoto amefariki juzi jumamosi alfajiri huyu bwana alishauza kila kitu kupambana mwanae apone ila kafa pale MNH kapewa bill Tsh 2,470,000/= kawaambia hana wamemwambia maiti ya mwanae hawampi hadi apeleke angalao Tsh 700,000/= hapo bado gharama za mazishi hajaandaa hiyo nauli tu ya kumtoa Buza kwenda Muhimbili alikuwa naomba kwa watu.
Tunaweza tukaona ni jinsi gani maisha yanafanywa kuwa magumu,anyway basi kama uwezekano wa bills kufutwa upo iwe ruhusa mtu mgonjwa wake akifariki apewe mwili akamsitiri maiti wake asahau machungu ila ajabu Tanzania hii tajiri anasamehewa maskini anakomeshwa.