Joseph Kasheku (Musukuma): Nitapeleka hoja binafsi bungeni kudai kila mkoa ununue ndege zake za kufanya biashara

Joseph Kasheku (Musukuma): Nitapeleka hoja binafsi bungeni kudai kila mkoa ununue ndege zake za kufanya biashara

Mbali ya kuongelea kununua ndege kaongea pia haoni umuhimu wa kujenga mavituo ya mabasi maana anaona imekuwa kama mikoa inashindana kujenga mavituo,akapendekeza kuepusha vituo vya mabasi kujaa ingeruhusiwa magari kusafiri usiku
 
Mnao pita pita huko Duniani tusaidieni,

Hivi ndege siku hizi bei zake zimerudi kwenye "Yu Tong".....!
Hapana. Bei yake na ya bajaji nadhani ya bajaji ni kubwa zaidi. Halafu, kujenga kiwanja cha kutua na kurukia ndege haifikii kujenga kituo cha mabasi yaendayo mikoani kutoka darisalama.
Acha tuyanunue madege kwanza, viwanja kila mkoa baadaye tutavijenga hayo madege yakiwa njiani kuja nyumbani
 
Ukiwa ccm na hapohapo wewe ni msukuma basi athari za ulaji wa kende za ng'ombe kwa wingi hujitokeza hadharani na kuonyesha kiwango cha upopoma uliopo kichwani.
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph aka musukuma amesema atapeleka hoja binafsi bungeni ili kila mkoa umiliki ndege zake za kibiashara.

Musukuma amesema hoja yake bungeni itabainisha namna ya ndege hizo zitakavyofanya biashara ili kuwepo na ushindani wa halali wa kibiashara baina ya mkoa na mkoa.

Maendeleo hayana vyama!
hapo hakuna mbuge
 
Musukuma amesema hoja yake bungeni itabainisha namna ya ndege hizo zitakavyofanya biashara ili kuwepo na ushindani wa halali wa kibiashara baina ya mkoa na mkoa.


Kwa kipato kipi cha watanzania

UMMY NA WAZEE BUKOBA_0.jpeg.jpg
 
Kweli huyu ni darasa la saba. Badala ya kulilia mapato ya mkoa sasa yajikite kujenga mahitaji ya jamii yatika mikoa husika. Yeye anataka kila mkoa ununue ndege. Anafikiri kununua ndege ni kama kununua pipi ? ATCL wanatosha.
Unafikiri shida ni ugumu au urahisi wa kununua ndege kama pipi? Shida ni hayo mawazo kwamba kila mkoa uwe na ndege zake. Yaani amekaa akawaza akaona ni wazo zuri na litawafaa watanzania hivyo likapiganiwe bungeni. Hapa napiga picha wakati amemaliza kuwaza Ile morali mtu unayopata ukipata idea nzuri mpya. Asibezwe mpaka asikilizwe and all in all ni mwakilishi wa wananchi ngoja hoja ikajadiliwe bungeni.
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph aka musukuma amesema atapeleka hoja binafsi bungeni ili kila mkoa umiliki ndege zake za kibiashara.

Musukuma amesema hoja yake bungeni itabainisha namna ya ndege hizo zitakavyofanya biashara ili kuwepo na ushindani wa halali wa kibiashara baina ya mkoa na mkoa.

Maendeleo hayana vyama!
Kweli wabunge wengine ni kichekesho mwisho watapeleka muswada wa kuwa kila Mkoa uwe na Rais wake
 
Back
Top Bottom