Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu
Inashangaza sana mtu kama Sugu alieanza kuikanyaga ardhi ya Kaburu kabla ya vijana wengi wa Tanzania hawajawa na akili ya kufika huku, ameshindwa kusoma alama za nyakati ambazo bila chenga wala mizengwe zinaonesha fika kwamba awamu hii ni zamu ya Lisu iwe mvua au liwe jua.
Mimi nafikiri hata kama ni chawa wa mwenyekiti lkn kwa jinsi upepo unavyoelekea yeye angejifanya hana upande ili Lisu atapochaguliwa waweze kufanya kazi pamoja.
Sasa kwa namna yoyote ile ikiwa Lisu atachaguliwa kuongoza Chadema, nina imani Sugu atashindwa kufanya nae kazi vizuri mwenyekiti wake mpya, na kwa vile ashaonesha kumpinga wazi wazi mwenyekiti wake mtarajiwa basi ninahisi pengine huko mbele atafanya maamuzi ya kukimbilia CCM ili akachaguliwe kuwa naibu waziri wa michezo na utamaduni, huku Mwana FA ambae anashika nafasi hiyo kwa sasa, huenda atapandishwa cheo na kuwa waziri kamili.
Kuna kila dalili kuwa Mbowe akishindwa atawatelekeza wote waliompambania na kuendelea na biashara zake zinazompatia ugali, hivyo Sugu atakosa mtu wa kumshika mkono chamani na kuamua kutimka bila kufukuzwa.