Joseph Mrindoko wa wachokonozi azichana vibaya shule za English Medium

Joseph Mrindoko wa wachokonozi azichana vibaya shule za English Medium

Sio dharau ndio ukweli halisi mwandalie mtoto elimu nzuri hata hizo English medium zinafaa sana tena ni cheap izo st kayumba ndio zinazotoa vijana wavuta bangi wakabaji walevi wa pombe za nimeyaona haya mana ata Mimi nilisoma kayumba miaka hiyo
Kwako elimu nzuri ni ipi?
 
Cha muhimu shule ziwe na waalimu wanaojua English vizuri kwa sababu siku hizi shule nyingi za English medium zinatoa watoto wa Std 7 hawajui kiingereza. Pia mzazi kabla hujampeleka mtoto huko hakikisha nyumbani unamuongelesha kiingereza sio akitoka shule ni kiswahili mwanzo mwisho. English ni lugha ya hela. Hata mchina anajifunza English.
 
Huyo jamaa ni mpuuzi.eti yeye anajua kila kitu..
 
Amezichana vibaya shule za English Mediums na kuwaita " mbumbumbu "Watanzania wanao jistress kusomesha watoto wao kwenye shule hizo.

Ameongea point nyingi sana nenda kamsikilize mwenyewe You Tube.

Moja kati ya nukuu yake anasema " Waafrika tunataka kuwa kama wazungu. Wazungu hawataki kuwa kama sisi.

Tumekuwa mbumbumbu kiasi cha kulipa pesa ili watoto wetu watengenezwe wawe kama wazungu.

Cha ajabu hao tunao taka wawatengeneze watoto wetu wawe kama wazungu sio wazungu wala hawajui chochote kuhusu wazungu na uzungu
Wazazi tuache kujifariji twende tukalipe ada hii miezi ya kulipa ada tusitafute sababu. Hizo kabla ya english medium elimu ilitufikisha wapi? Tuligundua nini. Hata ukiangalia maprofesa madaktari mahiri utagundua wamesoma elimu ya kizungu.

Leo hii madaktari bingwa tunawapeleka nje kwenda kupata elimu ya mzungu. Secta nyingine zinazohitaji wataalam vivyo hivyo. Angalia tulivyo nyuma kwenye Nafasi za kimataifa. Mataifa mengine wana watu wengi wanaoweza kufaulu hizo enterview za mashirika ya kimataifa.

Dunia imebadilika usidanganywe ukataka kutumia mbinu ya 1950 utajuta. Anaeongea hapa mtoto wake anapatiwa elimu nzuri (ya kizungu) then kesho atakutawala wewe, mtoto wako na mjukuu pia. Atakupangia kila kitu kwenye maisha yako
 
Wazazi wengi wenyewe hata kiingereza cha kuombea maji hawakijui.

Wakisikia english medium wanajua kuna elimu bora kuliko kwingine.

Mwisho wa kozi mtoto anahitimu hajui kuongea kiingereza vema inabidi akimbizwe tena mitaani kupatiwa english course ya pre form one, huko nako anaenda kubabaishwa na vijana wa form six failure wasiojua vema kuongea kiingereza.

Mzazi anaishia kutapatapa asijue wapi kuna elimu bora kwa mtoto wake wakati naye ni dunya tu shule alikwenda lakini akaishia kusikojulikana kama alisoma au hakwenda hata darasa moja
Mm niliona hz shule wazaz wengine hawakusoma wanaopeleka watt zao utasikia nawawekea msing mzur je yy mazaz aliwekewa huo msingi halafu wazaz wa kipato duni mostly ndo wanajikaanga huko hataree
 
Back
Top Bottom