Kiuhalisia uongozi ni kujitoa kwaajili ya wengine, na wala siyo kunufaika kutoka kwa wengine. Uongozi ni kuwasaidia unaowaongoza, siyo wanaokuongoza wakusaidie wewe kutengeneza maisha. Ndiyo maana nchi zilizoendelea, huwezi kuona maskini anagombea uongozi. Maskini atawezaje kuwasaidia maskini? Kwetu maskini wanahangaika kuupata uongozi ili waondokane na umaskini, ndiyo maana wakiupata uongozi, wanageuka kuwa majizi.