Joti hana mpinzani kwenye tasnia ya uchekeshaji

Pia kuna jamaa naitwa MKOJANII ninnouma
Sure sumaku Ni hatari na kuna MKWERE
 
Jamaa ana kitu kinaitwa "awareness" Kwa kila anachokifanya , habahatishi .... Ukikuta ni mkulima , ni mkulima kweli na anayajua ya wakulima , ukikuta ni manager wa bank , anajua kila kitu kuhusu bank , ukikuta ni fundi garage au mama ntilie au muosha magar anakuwa anazijua term zote alaf anaziconvert kuingia kwenye commedy na haishiwi content ..... Huyu mwamba ni genius , wengine wanakuwa na angle moja Tu ya uchekeshaji thus why wanaishiwa maneno mapema sana
 
Yuko serious na anachokifanya, sio anafanya ilimradi
 
Kamuangalie Joti kwenye tamthilia ya Mwantum,
Utarudi kufuta kauli yako hiyo.
 
Sikujua kama kuna mtu huwa anamuona SUMAKU aisee. Kongole sana brother. Jamaa ana kitu sana ndani yake.
 
Hahaha Deogratius, mbwa! Aisee huyu fala hafai. Natoa kiingilio kbs roho nyeupe!
 
Okay ila Joti ni mtundu tu na vituko sio mchekeshaji wa daraja hilo analopewa.

Mfuatilie Victaza au Sumaku wa Mizengwe utajua Joti hajui.
Sumaku ni nani katika wale?
Mizengwe nawapenda sana kiukweli wale mabwana pamoja na yule binti stories zao zinamafunzo na kuchekesha pia, mnaweza kuangalia na familia nzima, hasa yule babu me hua ananifurahisha zaidi tena mwanae akiwa Mkwere yaani vituko.com
 
Eti mzee majuto jina lilimbeba?ulitaka abebwe na jina lako?hiyo ndo brand yake na sisi tusio na naongwa huyu ndio msanii namba moko kwa uchekeshaji,toka nasoma primary huyu mzee anavunja mbavu za watu mashuleni leo useme eti hana uhalisia,wa wap ww?uhalisia wa joti ni huko kuigiza ye mwanamke?
 
SUMAKU ni yule mtu mzima ukimtoa yule babu, Mkwere na Mkongo.
 
Mimi Joti..mpoki..Sumaku..nawakubali Sana lakini kwa uchekeshaji huu wa kisasa..namkubali yule jamaa wa cheka tu aliigiza kuhusu wasukuma..na Kuna clip anawaponda watu wanaotumia dawa ya mswaki inaisha lakini wanaitoboa na kukomba Kila kitu
 
Yupo mang'endo
 
Joti ni mkongwe na anafiti characters zote ila kwangu mimi hawezi kukaa namba moja,namkubali ila list yangu mimi hii hapa(top five)
1.kitale akitumia(mkude simba$bwakila hizi ndio character anazotumua)huyu jamaa yupo vizuri mno kuanzia viclip mpaka katika movie alizo direct yeye kuna sign unaweza cheka mpaka basi,au amuige lufufu sasa dah

2.Ringo,huyu mwamba hatumii nguvu sana kuchekesha ila ni kipaji maalum,

3.mkojani dah huyu jamaa anakuja vizuri sana,ukimsikiliza maneno yake lazima ucheke
4.joti
5.HD na katarina hii bond ilikua poa sana sijui wako wapi saizi,ila nilikua nawakubali sana
 
Mimi nimeongelea mimi wewe unaongelea sisi hapo ndio tofauti, nimesema mimi sijawahi kumkubali wewe unasema sisi tunamkubali sasa sijui unaongelea wangapi. kauli nimemkataa mimi na nimesema kuna watu wanampenda na kawaida tu kuwa na mashabiki na sio mashabiki. Joti ana character nyingi na mimi sipendi zote baadhi. Rai yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…