Joti hana mpinzani kwenye tasnia ya uchekeshaji

Joti ndio anachekessha,lakini nataka ujue sanaa ya uchekeshaji ina vitu vingi ndani yake wasivyovijua wengi. Vizuri ujue,kile kitakachokuchekesha sana wewe,mimi kinaweza,ikawa kawaida tu. Namkubali sana Brother K
 

Namkubali Joti vya kutosha. Ila nakubaliana na ww kwamba kwenye stand-up comedy za kuvaa kawaida na kutema madini watu wavunje mbavu bado hatujaona uwezo wake. Mpoki alijaribu, shida yake vijembe vingi anachekesha kwa kukandia watu!

Joti zaidi kwenye mambo ya kujibadilisha na ukatuni anaweza.
 
Mzee Majuto bila make-up yoyote ukimuangalia tu kabla hajaongea unawez kucheka. Kuna yule mwingine Mzee Jangala.
 
Okay ila Joti ni mtundu tu na vituko sio mchekeshaji wa daraja hilo analopewa.

Mfuatilie Victaza au Sumaku wa Mizengwe utajua Joti hajui.
Joti hajui.
Mkuu ukiona mtu Yuko juu hasa katika masuala ya entertainment basi ujue hajabahatisha .... Iko hivi kipaji huwa kinaanza level ya chini , mtu anaanza kujulikana na watu wanamuelewa, asipoishiwa mbinu na content pamoja na ushawishi atahamia level ya Kati , hapa pia watu wengi zaidi watamuelewa , vivyo hivyo kama hataishiwa ubunifu ,mbinu na content atahamia level ya juu au national level ... Hapa Taifa zima wanamuelewa anakuwa amevuka vikwazo vingi na amedhihirisha hvo....

Joti yupo level ya juu right now , kapita level zote , kafanya commedy nyingi Sana na bado watu Wana hamu ya kuona kazi zake cse wanamini atakuja na kitu kipya....

Ni rahsi kumshindanisha joti na hao unaowasemea may be wamekuja juu Sana lakni still wapo kwenye initial stage , bado hawajapita middle na kufikia level za juu...wengi huwa wanaishia njiani Kwa kuishiwa content na watu kuona hawana ubunifu tena....
Hata makampuni hayakurupuki Tu kumpa kazi mshikaji , jamaa ni mbunifu kwenye tangazo unaona kabisa mshikaj kalitendea haki

bado hawajafika hao kuwalinganisha na joti , mda utafika data zitasoma tutawalinganisha naye na sio kazi rahsi , wakaze
 
Nakubaliana na wewe katika brand positioning ni kitu ambacho Joti kawashinda wenzake. Management yake na yeye wanapiga kazi na inaonekana hawa wengine wamelala mbali ya talents zao.

Ila tukizungumzia katika talent ya kuchekesha yeye sio bora zaidi
 
Andunje, huyu mwamba yupo vzr sannaaa, nafatilia sana comedy zake..
 
Mkongwe tu halafu tuseme anafit kwenye character mbalimbali ,

Hilo la kuwa mchekeshaji namba moja kuna Nalimi Joseph halafu kuna fundi anaitwa Idriss hapana Chezea mkuu
Iddris full miyeyusho..full mizinguo..kwakifupi ni kero ni kama alivyokua masanja mkandamizaji tu..hovyo kabisa
 
Iddris full miyeyusho..full mizinguo..kwakifupi ni kero ni kama alivyokua masanja mkandamizaji tu..hovyo kabisa
Katika watu ambao sielewagi hata wanafanya nn basi ni Idris
 
kufanya roles tofauti fresh na kukaa miaka yote hii huku akiwa na impact hata kwa kizazi hiki cha youtube.
Naamini anastahili heshima kubwa sana
 

mtu si lazma awe bora katika kila kitu mkuu, hata mr bean hafanyi stand up comedy na bado anaheshimika kutokana na aina yake ya comedy
 
Joti akiwa mlinzi ndio balaa, nafikiri neno zuri ungetumia ni “Kiraka” jamaa anaziba gap lolote lile na anatambaa nalo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…