Joyce Kiria: Mwanamke kumhudumia mwanaume ni ujinga

Baba Kisarii

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2024
Posts
1,844
Reaction score
3,089
Anafunguka mwanaharakati.....

"Ni mjinga mwanamke ambaye anampikia mume wake, anamfulia nguo🤮 achia mumeo hizo kazi kwani yeye hana mikono? mbona wanawake tunakuwa wajinga hivyo, tutaelimika lini? zama za kumpikia na kumfulia mwanaume zimepitwa na wakati"- Mwanaharakati, Joyce Kiria

Natoa pole nyingi kwa mwanaume yeyote aliye na mke kama huyu mwanaharakati.
 
Huyu mwanamke ni ithibati tosha kuwa unaweza mtoa mtu toka ushambani ila ni ngumu kuutoa ushamba ndani ya mtu.

Ameshindwa kutofautisha 'feminism' (anao jinasibu nao) na ulimbukeni. She is trying too hard ku prove kuwa she is no longer a housemaid (si kwamba ni jambo baya kuwa beki 3) lakini anaishia kudhihirisha ulimbukeni wake tu in the process.

Kiria will always be a village housemaid at heart.
 
ni kweli haswaaa mwanaume mwenyewe km uyo wako ambaye kashaleft group kitamboooooo tuu
 
Kwa hiyo mama yake ni mjinga?Kwa sababu nina hakika alikuwa anapika.
Huu ujinga kwa visingizio vya kuiga usataarabu na maadili ya kimagharibi bila kujua undani wa hizo tamaduni.
Naishi Sweden Nchi ambayo inadaiwa imepiga hatua kubwa kwenye falsafa ya usawa wa kijinsia lakini wanawake ndio wanapika na kufanya kazi nyingi za ndani kwa asilimia kubwa sana.
Hakuna mfumo wa housegirl Sweden.
Huyu binti amepotea kimaadili.Nimeoa huku na mke wangu anapika bila tatizo lolote.
 
Kichaa huyu
 
Huyu mama ana pointi asikilizwe
 
Hizo kucha ndefu.. chooni anaendaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…