Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Ubongo wa mende kama wako ndio unaotufanya tunateseka kama Taifa, yaan wewe kuongea kiingereza ni deal sanaaa kuliko message aliokuwa akiifikisha? Waingereza wangapi tena viongozi wanaboronga kiswahil na huleti uzi hapa? Acha ujinga bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwani kiingereza ndio elimu ya mtu au lugha tu kama kichaga,
natamini sana serikali itamke waziwazi kuwa kiswahili kitumike ktk shughuli zote za serikali na kiingereza kitumike tu kama lugha ya ziada maaana watanzania tumeleweshwa na kiingereza hadi mtu akikosea kwa bahati mbaya basi tayari unaaanza kuuliza juu ya elimu yake kama iko sawa!!

naiomba serikali yetu kupitia waziri wa habari tangazeni kiswahili kiwe ni lugha rasmi ya shughuli za serikali ikiwemo Mahakamani ambapo bado kinayumika zaidi kiingereza wakati wanao kijua wachache.tuache ukoloni

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikupe pole kwa ndoto zako za mchana
 
Wasema nina uelewa mdogo sana, then unasema nikivuka malawi dogo anachunga ng'ombe lakini anaongea kingereza vizuri hivyo anafaa kuwa Raisi, mbona kama hujui unachoongea mkuu? Yani unafafanisha PhD holder aliyesomea kwa lugha ya kingereza na mtu anayeongea kingereza toka kwenye nchi wanayotumia hiyo lugha?
So mimi na wewe nani uelewa wake ni finyu??
Hivi unatetea huyo waziri kutokujua kingereza au unasema kuwa anakifahamu?
Mwisho PhD yake kafanya kwenye nchi wanayotumia kingereza na siyo China wala Germany kama hukuwa na taarifa
Na yule pale hakuwekwa kwa sababu ni anajua au hajui kiingereza. Wewe level yako ya uelewa ni ndogo sana hivyo hata dhana nzima ya PhD hunayo. Ungekuwa unajua japo kidogo vitu hivi vya kitaaluma usingezumza huu upupu. Unapoandika thesis hasa kwa level hizo Master or PhD ziko ambazo supervisors wala hawahitaji Kiingereza chako bali presentation ya mawazo na findings zako. Ndiyo maana kabla ya difference hapo ndo unashauriwa sasa kupeleka thesis yako kwa mtaalum wa lugha kuifanyia edition kwa maana ya upangaji wa grammar nk. Kama kiingereza ni kigezo kwa levels hizo basi na lugha nayo ingekuwa inasahihishwa. Lkn pia kuna Master na PhD zinasomwa kwa lugha tofauti tofauti japokuwa wewe umekariri kiingereza tu. Kuna watu wanaenda soma Ujeruman, Portugal, China nk ambao hujifunza lugha za nchi hizo na kisha kusoma levels hizo. kwa wewe mwenye uelewa mdogo utahoji tu kwa nn hajui kiingereza vizuri wakati ana PhD. Kiingereza ni lugha tu kama kimakonde na ukitaka kujua hilo vuka hapo malawi utakuta dogo yupo porini anachunga kamaliza primary lkn anapiga kiingereza kwa mjinga kama wewe ukimuona utasema huyu nchini kwetu anafaa kuwa Rais wa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Level gani hiyo ambayo tunasoma kwa kiswahili? Nadhani hujui unachoongea wewe. Swala la mimi nikawe waziri limefikaje hapa au kuna mtu kasema atoke kwenye uwaziri? Pathetic
we utakuwa ma matatizo kichwani tz tunasoma kwa kiswahili au unataka kuleta ligi tu basi nenda wewe kawe waziri wa elimu tukuone unavyoongea english

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni lugha iliyokuja na meli mbona Taarifa za hukumu kwenye mahakama zenu zinaandikwa kwa hiyo lugha ?, mbona hamjawahi kuikataa ?!, na ndio maana mnaandikiwa hukumu ambayo hata hamuwezi kuihoji kwa sababu imeandikwa kwa lugha isiyo yenu, mahospitalini kote umewahi kukuta Daktari anaandika kwa Kiswahili ?.
Hivyo vigezo vyako haviuondoi ukweli kwamba hatuna utamaduni wa kuongea kingereza tangu utotoni.

Huyo waziri ni sehemu tu ya watanzania wengi ambao majumbani hawana utaratibu wa kuongea muda wote kingereza tofauti na hawa watoto wa kizazi cha sasa wanaosoma hizi shule za kisasa.

Tuliosoma bure enzi za Nyerere kingereza ni mtihani kwani hatukulelewa katika mazingira ya kingereza muda wote tofauti na Kenya, Afrika ya kusini na Nigeria.
 
Kati ya hawa mawaziri Wahutu ni Mpango pekee yake ndio huwa anatema yai lakini huyu mama na Kigwa na wenzake ni bure kabisa
Mkuu imhotep inawezekana hata wewe ukipewa hizo nafasi kubwa ukatakiwa utoe mhadhara mbele ya umati ukajikuta unazichanganya past na present tense, hilo lugha huwa hatuiongei mtaani wakati wa kununua maua au nyanya sokoni.

Tofauti na Kenya, Nigeria na South Africa, tunakosa kujiamini kwani hatuna utamaduni wa maongezi ya kingereza ya kila siku.
 
Hiyo Phd yake lugha aliyotumia kuipata ni kingereza, kushindwa kuzungumza kingereza vizuri ni lazima tuwe na mashaka research na thesis alizifanyaje?
Angekuwa Mrusi au mchina ingeeeweka lakini kaipata kwa Kingereza
Vyuo hutumia idara za lugha kuwasaidia wanafunzi wenye matege ya lugha kunyosha kazi zao.
Ni huduma inayolipiwa na mhusika. Hata mitaani kuna huduma hii.
Tusisahau msimamizi pia humsaidia mwanafunzi wake kuweka lugha vizuri.
 
Binafsi huwa naamini ni rahisi zaidi kuzungumza lugha yoyote ile kuliko kuandika endapo utakuwa ktk jamii ambayo lugha husika hutumika. Kinachoniogopesha kuhusu hawa wasomi wetu baadhi yao hasa hasa waliofika ngazi ya uzamivu (PhD) kama huyu mama ni kushindwa kuzungumza lugha anayoitumia kila siku kwa ufasaha.

Kwa hadhi yake kama waziri, mtafiti na mtaaluma nina uhakika kwa siku ktk masaa 8 ya kazi si chini ya masaa 3 hutumia lugha ya kiingereza kuwasiliana na wadau mbali mbali ktk sekta ya elimu. Hofu yangu kubwa ni je hata uwezo wake kiutendaji unafanana na uzungumzaji wa lugha kiingereza?
 
Binafsi huwa naamini ni rahisi zaidi kuzungumza lugha yoyote ile kuliko kuandika endapo utakuwa ktk jamii ambayo lugha husika hutumika. Kinachoniogopesha kuhusu hawa wasomi wetu baadhi yao hasa hasa waliofika ngazi ya uzamivu (PhD) kama huyu mama ni kushindwa kuzungumza lugha anayoitumia kila siku kwa ufasaha.

Kwa hadhi yake kama waziri, mtafiti na mtaaluma nina uhakika kwa siku ktk masaa 8 ya kazi si chini ya masaa 3 hutumia lugha ya kiingereza kuwasiliana na wadau mbali mbali ktk sekta ya elimu. Hofu yangu kubwa ni je hata uwezo wake kiutendaji unafanana na uzungumzaji wa lugha kiingereza?
Mkuu una Hoja ya msingi sana, yaani huyu ndie waziri wetu tena wa elimu !!.
 
Hizi Fitina Jamani, huyo Mama amekukosea nini?
Fitina Hazijenga Mzee wa Heru Juu . Elimu siyo kuongea kiingereza.
Ni zwazwa huyo waziri wenu, ni heri hata wale wanafunzi waliowafukuza pale Udom mwaka ule wakiwaita vilaza, hivi nani kilaza kati wale wanafunzi na ndalichako na magu ?
 
Back
Top Bottom