Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?
Mkuu bado point yangu iko pale pale kwamba huenda hawana uelewa unaotakiwa ukizingatia uzoefu na uelewa wa kazi unazidiana na kutofautiana kutoka polisi mmoja hadi mwingine kutokana na uzoefu wa kazi na muda waliodumu kazini. Ni sawa na kumpa dereva mpya mwenye leseni ya daraja D aendeshe lori kubwa lililobeba mzigo mzito na kumwambia asafirishe mzigo kwenda mbali, matokeo yake unayajua. Kijana yule wa polisi alikuwa na umri wa miaka 23, na kwa vyovyote utakuwa umejua uzoefu wake kwenye field za kipolisi ukoje.Mkuu naamini wanazifahamu sana ila unajua kule hufanya kazi kwa order wakiamini wako ya sheria sitaki kusema sana ila kumbuka yule mwandishi wa habari aliemiminiwa risasi akageuzwa butcher...Unadhani ni bahati mbaya tu ilitokea ile?
Polisi Wa Usalama Barabarani Anaruhusiwa Kisheria Kukagua Gari Yako Kama Inamakosa Kadha Wa Kadha. Kama Sehemu Alokusimamishia Ni Porini Na Unatia Shaka Na Maeneo Hayo Usisimame Bali Nenda Katoe Taarifa Kituo Cha Polisi Kilichopo Mbele Yako.Mkuu, hata mimi nina utata na taratibu za hawa jamaa wa barabarani, naongezea swali, je ni haki yangu kutompa traffic police anapoiomba/ ihitaji leseni yangu, je nikimuonyesha tu bila kumpa aishike nitakuwa nimetenda kosa?
Japo amepangilia vizuri lakini ameshindwa kujua askari anapokuwa kwenye uniform anaweza kukumata bila hata kitambulisho ili mradi kosa limefanyikaUsikute hata polisi mwenyewe hana uelewa na hizi taratibu, sasa ukimuomba kitambulisho anaona kama umemdharau.
Halafu pia sioni kama kuna uwezekano wa kumshtaki polisi aliyekudhalilisha, maana ndio yale ya kesi ya ngeredere anapelekewa nyani.Japo amepangilia vizuri lakini ameshindwa kujua askari anapokuwa kwenye uniform anaweza kukumata bila hata kitambulisho ili mradi kosa limefanyika
Lakini polisi wetu hawajui huio utaratibu wao wakifika ni "kaa chini" na kufuatiwa na virungu kisha wanakwambia utajibu mbeleThank you sweet heart
Asante sana, ingependeza kuandika kwenye magazine ili watu walio wengi zaidi wapate kitu.
- Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
- Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
- Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
- Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
- Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
GreatUSINYANYASWE WE NDUGU FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI WETU
( 1 )Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
( 2 )Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
( 3 )Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
( 4 )Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
( 5 ) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
( 6 )Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
( 7 )Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
( 8 ) Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
( 9 )Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
( 10 )Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
( 11 )Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
( 12 )Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
( 13 )Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
( 14 )Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
( 15 ) Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
( 16 )Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
( 17 )Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
( 18 )Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
( 19 ) Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
( 20 )Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
( 21 )Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
( 22 )Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.
Kutoka: Sheria Yakub Blog: USINYANYASWE NDUGU
Naona watu wengi mna mihemuko na hamfahama maana ya USALAMAAskari wetu hawafuati hizi sheria sio kwa kosa lao, hapa ntailaumu serikali, maaskari wanapata mafunzo ya ovyo,
Serikali yetu kama sasa hivi inakaribia kua ka ya kidikteta hili haliwezekani, kauli za "kamata kwanza tutafix baadaye" hizi sheria zitabaki kwenye karatasi tu.
Mfano hai wa 2tutafikatu ahsante kwa hii. Ukituletea na ya traffic itakuwa umetusaidia kutii sheria bila shuruti
Naona watu wengi mna mihemuko na hamfahama maana ya USALAMA
pale Kituoni na mahali salama kwa kujielezea na kuomba hifadhi km umeharibu URAIANI
Kuna siku rafiki yangu alipata pesa nyingi ghafla akanipeleka Grocery akaniambia niagize chakula na kunywa nitakavyo yeye yupo.
Kwa vile ana pesa nilifanya hivyo deni likafika zaidi ya 30,000/=
jamaa akasepa nyuma ya banda akiagiza nitajilipia
wahudumu kweli walidavua nikavumilia hadi nilipoona askari POLISI ambaye nilimuomba msaada anipeleke Dukani kwangu nikawalipe hao wahudumu, kufika Dukani nikakuta jamaa kafika na kukomba hela eti kuja nikomboa kumbe kalala mbele tena.
nilikopa jirani lakini ilibidi niende POLISI kufungua faili wakagoma kupata ushauri kwanza nako mm nikagoma bora nilalae hapo maana NITAUA
POLISI walinisaidia tukafanikiwa kumkamata tapeli wangu lakini aligoma kila kitu kulipa.