Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Hawa wa hapa kwetu hawajui hayo, ukiwazingua wanakuchekecha. Kazi yako kwisha
 
kama PROFESSA MZIMA (LIPUMBA) walimfanya vile na haki zake zote anajua, sie bangusilo tutathubutu?
 
wadanganye waote manundu kwa police wa bongo labda kwa wenzetu wa ulimwengu wa kwanza
 
Akija Askari polisi mmoja,.then akakiuka.hayo ya juu, hawezi nichukua.
 
Hayo umeongea kwa upande wa raia but think on other side of the coin, na wenyewe wana katiba yao inaitwa "police guide order" ogopa kukutwa.
 
nahitaji kujua haki zangu niwapo barabarani na chombo cha moto, kiwe gari au pikipiki. maana hapa tunaonewa sana,
je ni sahihi kuacha gari kituoni kama sina fine!?

je ni sahihi traffic kuongozana nami ndani ya gari tunapoelekea kituoni!? endapo ntakataa kusign notification ya polisi, ni sheria gani hufuata baada ya hapo!? maana kuna siku walitaka niweka lock-up kisa nimegoma sign notification (ofcorse walitaka kunionea tu bila sababu ya msingi nami sipendi onewa).

natakiwa lipa fine ndani ya muda gani!? ni sahihi kumwachia traffic Driving License yangu!? Ni sahihi kuacha gari au leseni kwa traffic kisa nataka nkalipe fine mwenyewe kituoni!? (siviamini vitabu vyao, nahisi magumashi ni vingi)

ukishayajibu haya ntauliza mengine.
 
kama PROFESSA MZIMA (LIPUMBA) walimfanya vile na haki zake zote anajua, sie bangusilo tutathubutu?

Tatizo sio sheria mkuu, mfumo wetu wa kudai haju una tatizo.

Kwa polisi wa Tanzania huwezi kumuuliza kwanini amekukamata, au kwanini anakusachi, ukijaribu kumbishia hata kwa maelezo kama mleta mada alivyoelezea utaingia kwenye matatizo tu.

Kuna watu wanapigwa hadu wanapoteza maisha na wengine kusababishiwa ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kubishana na polisi au ujinga wa polisi wa kutotambua mtuhumiwa halisi wakati wa jaribio la kumkamata mtuhumiwa.

Hivi kama polisi amekupiga au amekudharirisha bila sababu ya msingi utamfanya nini? Maana huwezi kwenda kumshtaki polisi bila kupitia kwa polisi tena ambapo kimsingi naona ni kupoteza muda tu.
 
wadanganye waote manundu kwa police wa bongo labda kwa wenzetu wa ulimwengu wa kwanza

mkuu nilishawah kukamata na polisi maswal niliyoulizwa ni ajabu...af ndio ujifanye unazijua haki zako ndio balaa kabisa
 
Kabla haujamshauri raia kuyajua hayo.tungehangaika neno jeshi liondolewe kwenye mafunzo ya upolisi.chombo hicho kiitwe hivi, KIKUNDI CHA WATUWANAOWAONGOZA WATUHUMIWA KWENDA KUJIBU MASHTAKA MAHAKAMANI KWA KUWABEMBELEZA.lakini kwa kuwa mafumzo tu yamekaa kikuda huwezi kuta askari anakupetipeti.

We jaribu kuomba kitambulisho huku mtu kavaa uniform na unajua fika kuna ishu umeibaranya uone kitakachotokea mbele ya wanao.

Wenzio wakiishajua wameharibu mahali huwa wanakuwa wapole.isiwe taabu.
 
Akija Askari polisi mmoja,.then akakiuka.hayo ya juu, hawezi nichukua.

Akikupuuza wakaja wengi utajilaumu kwanini hukumsikiliza yule mmoja yakaisha.bora wanajeshi watakudunda wakuache unalia hapo.
Hawa wanakudunda, kituoni wanakupeleka, na kesi wanakuongezea (umempiga askari) ndio.

Kama unakaza kaza mwanzo mwisho mpaka wakimbie, kama unaweza lakini.
 
Kwanza kabisa polisi wenyewe wangefundishwa nakuelekezwa kabla hawajatumwa kuteleza amri wanazopewa
 
Akikupuuza wakaja wengi utajilaumu kwanini hukumsikiliza yule mmoja yakaisha.bora wanajeshi watakudunda wakuache unalia hapo.
Hawa wanakudunda, kituoni wanakupeleka, na kesi wanakuongezea (umempiga askari) ndio.

Kama unakaza kaza mwanzo mwisho mpaka wakimbie, kama unaweza lakini.

Polisi aje kijinga bila kufata sheria zao, aje kutak kunipekua kwangu bila kibari au utaratib maalum…? Anikamate bila warant wakati sipo kwenye kosa nitajihami aisee,, akiomba back up ya wajinga wenzie waje tu, watakuta kun back up yang somewhere pia...kama law enforcers wanavunja sheria unawachap mtakutan mahakamani.
 
Tatizo sio sheria mkuu, mfumo wetu wa kudai haju una tatizo. Kwa polisi wa Tanzania huwezi kumuuliza kwanini amekukamata, au kwanini anakusachi, ukijaribu kumbishia hata kwa maelezo kama mleta mada alivyoelezea utaingia kwenye matatizo tu.
Kuna watu wanapigwa hadu wanapoteza maisha na wengine kusababishiwa ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kubishana na polisi au ujinga wa polisi wa kutotambua mtuhumiwa halisi wakati wa jaribio la kumkamata mtuhumiwa.
Hivi kama polisi amekupiga au amekudharirisha bila sababu ya msingi utamfanya nini? Maana huwezi kwenda kumshtaki polisi bila kupitia kwa polisi tena ambapo kimsingi naona ni kupoteza muda tu.

Nikwambie kitu kizuri maisha yako yote.

Penye ukweli uongo hujitenga.

Ukiishakamatwa na polisi kimakosa.yaani wewe sio mtuhumiwa, usilete upinzani hata kidogo tulia, kubari kuwa una bahati mbaya siku hiyo, na hivyo unajua polisi wetu walivyo wakurupukaji-relax.wakati utafika tu wa wewe kuwa huru.ukijitikisa tu kwa namna yoyite ile umekwisha.

Embu kaangalie prof wetu mzee lipumba alivyopelekwa kwenye gari halafu linganisha na wale jamaa zake waliokuwa wanaleta upinzani kwa mapoti walifanywaje?.akili nyingi mbele huwa giza.
 
Polisi aje kijinga bila kufata sheria zao, aje kutak kunipekua kwangu bila kibari au utaratib maalum…? Anikamate bila warant wakati sipo kwenye kosa nitajihami aisee,, akiomba back up ya wajinga wenzie waje tu, watakuta kun back up yang somewhere pia...kama law enforcers wanavunja sheria unawachap mtakutan mahakamani.

Ah.kama unaweza kuwachapa wote ni visuri sana.

Maana mie ninavyojua.akirudi jamaa mmoja kulipoti kuwa jamaa kagoma kuja kituoni.ndio lile sentensi fupi UTII WA SHERIA BILA SHURUTI unakuwa umewahakikishia kulikataa, wanakuja.

Kama unaiweza vita haaya simama, ila hapo hamna wa kulaumiwa.
 
Wakija wanakuta back up yang imejipanga, waki mwaga mboga namwaga ugali. Alone siwezi wakija kundi
 
Police wa Tz nadhani hawajui sheria vizuri,au km wanazijua basi kuna kitu nyuma ya pazia ndio mana wapo hivi walivyo pindi wanapotimiza wajibu wao..
 
Police Wa Tanzania Ni Majambazi Kabisa,huwezi Kuwahoji Haki Zako Wanakuua Tena Kikatili Kabisa,yuko Wapi Mwangosi? Wako Wapi Wale Vijana Wahangaikaji Wa Mahenge? Hii Si Nchi Salama Ya Kuishi Kabisa.
 
Hizo zote hapo ni wajibu wa mtuhumiwa kuhoji ila ukae ukijua utakufa kifo cha aibu sana hadi Shetani mwenyewe atakushangaa! hawa jamaa waskie tu kwa UKAWA usiombe yakukute!
 
Back
Top Bottom