Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Jua haki yako unapokamatwa na Polisi

Tatizo sio sheria mkuu, mfumo wetu wa kudai haju una tatizo. Kwa polisi wa Tanzania huwezi kumuuliza kwanini amekukamata, au kwanini anakusachi, ukijaribu kumbishia hata kwa maelezo kama mleta mada alivyoelezea utaingia kwenye matatizo tu.
Kuna watu wanapigwa hadu wanapoteza maisha na wengine kusababishiwa ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kubishana na polisi au ujinga wa polisi wa kutotambua mtuhumiwa halisi wakati wa jaribio la kumkamata mtuhumiwa.
Hivi kama polisi amekupiga au amekudharirisha bila sababu ya msingi utamfanya nini? Maana huwezi kwenda kumshtaki polisi bila kupitia kwa polisi tena ambapo kimsingi naona ni kupoteza muda tu.

Sio lazima kupitia polisi ili kufikisha suala lako mahakamani. Tunapitia polisi ili kukamata mtuhumiwa tu lakini kesi inaweza kufunguliwa bila kupita polisi na hasa kama polisi wenyewe wanahusika.

I stand to be corrected.

Tiba
 
Sio lazima kupitia polisi ili kufikisha suala lako mahakamani. Tunapitia polisi ili kukamata mtuhumiwa tu lakini kesi inaweza kufunguliwa bila kupita polisi na hasa kama polisi wenyewe wanahusika.

I stand to be corrected.

Tiba

Asante kwa kunirekebisha na kuniongezea elimu, ila hapo kwenye kuwahoji polisi ni kujitafutia matatizo.
 
Pia kama unajua kuandika na kusoma.

Mhusika kuandika maelezo polisi ni haki ya msingi. Na sio kuandikiwa na polisi
 
Police wa Tz nadhani hawajui sheria vizuri,au km wanazijua basi kuna kitu nyuma ya pazia ndio mana wapo hivi walivyo pindi wanapotimiza wajibu wao..

Mkuu vifungu vipo waz vinavyowapa nguvu kufanya hvyo...cpa 14 pale panajieleza
 
Afisa polisi anaweza bila hati kumkamata..
(a)mtu yeyote ambaye anafanya uvunjifu wa amani mbele yake.
(b) mtu yeyote ambaye kwa masudi anamzuia afisa polisi aliye katika utekelezaji wa majukumu yake,au mtu ambaye ametoroka au anajaribu kutoroka kutoka mahabusu halali kisheria
(c)mtu yeyote ambaye atakuwa na kitu chochote kinachodhaniwa kwa sababu za msingi kuwa ni kitu kilichoibiwa au mtu anayedhamilia kutenda kosa kuhusiana na kitu hicho
(d)mtu yeyote atakayemkuta amelala au kizurula katika barabara kuu,yad,bustani au sehemu nyingine wakati wa usiku na ambaye anamdhania kwa sababu ya msingi kuwa ametenda kosa au anataka kutenda kosa au amebeba bila ruhusa halali silaha ya hatar au kifaa cha kuvunjia nyumba
(e)mtu yeyote ambaye hana sababu za msingi za kuamini kuwa hati ya ukamataji imeshatolewa.
g.mtu yeyote anayefanya tendo lolote linaloazimia kutusi nembo ya taifa au bendela ya taifa
h,.mtu yeyote anayemdhania ni mzurulaji
 
sasa mbona hizi sheria.zinakinzana zenyewe maana haki ya mtuhumiwa inakuwa finyu sana kwa sababu hapo juu tumeona mtuhumiwa anashauriwa kisheria kumhoji au kumuomba kibali toka.mahakaman cha kumkamata au kumuomba kitambulisho akuonyeshe au kumkagua polisi endapo kala polisi hajamkagua mtuhumiwa ....ni haki yake....sasa mbona huzi sheria zinakinzana sana
 
kwa mfano mimi niko barabaran natembea zen polic aloko doria ananitilia shaka kuwa pengine namadawa ya kulevywa hapo nilipo na polic huyo anaamua kunitia chin ya ulinzi haki yangu hapo kama mtuhumiwa ni ipi katika tukio hilo kablaya kwenda katika kituo chochote cha polic?
 
Upekuzi wa dharula...

Afisa polisi anaweza..
a..kumpekua mtu anayemshuku kubeba kitu chochote kinachohusiana na kosa au.
b)kuingia kwenye ardhi yoyote au katka jengo lolote chombo au gari ambamo anaamin kwa sababu za msingi kuwa kitu chochote kinahusiiana na utekelezaji wakosa
 
kwa mfano mimi niko barabaran natembea zen polic aloko doria ananitilia shaka kuwa pengine namadawa ya kulevywa hapo nilipo na polic huyo anaamua kunitia chin ya ulinzi haki yangu hapo kama mtuhumiwa ni ipi katika tukio hilo kablaya kwenda katika kituo chochote cha polic?

mkuu hapo huna haki kutokana na hizo sheria hapo juu.

hayo nimawazo na mtizamo wangu maana naona kama zinakinzana vile hapo.

daaa tatizo tunakataa na kuwa wagumu kukamatwa na hawa polisi kutokana na mambo yanayoendelea baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi.
kama una mali za dhamani na pesa aisee utapigwa na kuzingiziwa kesi yoyote ile ilimladi tu wakutoe pesa.
 
sheria inamlindaje mtuhumuwa katika mazingira.kqmq hayo tajwa juu?
 
Mkuu ni hawhawa polisi wetu kwenye hii nchi au unamaanisha nchi zilizoendelea?!
Unaambiwa mfumo wa jeshi letu ni wa kikoloni sasa sidhani kama yanawezekana hayo!
 
wewe jidanganye tu tena kipindi hiki walivyouwawa kama kuku yaani watakuburuza .kumbuka kila haki ina wajibu pia kila sheria inazo isipokuwa zake .akili za kuambiwa changanya na zako.

We jizingueee tuuu uoneee cha mtema kuniiii

kama PROFESSA MZIMA (LIPUMBA) walimfanya vile na haki zake zote anajua, sie bangusilo tutathubutu?

Hawa wa hapa kwetu hawajui hayo, ukiwazingua wanakuchekecha. Kazi yako kwisha

wadanganye waote manundu kwa police wa bongo labda kwa wenzetu wa ulimwengu wa kwanza

Kweli sisi waTanzania ni mambumbumbu kabisa...yaani mtu anajitahidi kunyumbulisha haki zako mbele ya dhuluma ya Polisi....unabisha kuwa hustahili hizo haki, na kawaida ya Polisi kunyanyasa watuhumiwa ndio unaona ni stahiki yako!:shocked:
 
WISE 2012

Kwa tanzania hivi vitu ni nadharia tu practically havifanyi kazi.Polisi wa tanzania wanachojua ni marungu, mateke na kukata mtama. Uliona video ya Lipumba na wanachama wake?
 
Kweli sisi waTanzania ni mambumbumbu kabisa...yaani mtu anajitahidi kunyumbulisha haki zako mbele ya dhuluma ya Polisi....unabisha kuwa hustahili hizo haki, na kawaida ya Polisi kunyanyasa watuhumiwa ndio unaona ni stahiki yako!:shocked:

soma vizuri, hatujabisha kuwa hizo ni haki zetu, tunachoonya ni ukweli kuwa hali halisi haiko hivyo mtu asije akatoka mikoani huko, au karudi toka Ulaya, akajidanganya.
 
Polisi aje kijinga bila kufata sheria zao, aje kutak kunipekua kwangu bila kibari au utaratib maalum…? Anikamate bila warant wakati sipo kwenye kosa nitajihami aisee,, akiomba back up ya wajinga wenzie waje tu, watakuta kun back up yang somewhere pia...kama law enforcers wanavunja sheria unawachap mtakutan mahakamani.

sasa hapo unakua na kesi ya kumpiga asikari na usiombe ukaenda kituoni jua umekwisha!
 
wewe jidanganye tu tena kipindi hiki walivyouwawa kama kuku yaani watakuburuza .kumbuka kila haki ina wajibu pia kila sheria inazo isipokuwa zake .akili za kuambiwa changanya na zako.

Ameshau kusema askari haruhusiwi kukuua!
 
(5.) Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

Kwa msingi huu basi, naweza kumwuua askari mwenye silaha ambaye anakiuka utaratibu wa kunikamata nikijua kwamba nikijikinga naye anapokiuka taratibu za kunikamata huku ana silaha anaweza kuniua.

Ahsante sana kwa kunifahamisha.
 
Back
Top Bottom